Mazishi ya Wapigania Uhuru wa TZ huko Arusha waliouawa kidhalimu 5 January 2011

Asante sana, jamani tusipooze madai ya uhuru mpya wa TZ kwa faida yetu na vizazi vyote
 
Maoni yangu nitayaelekeza kwako Gurudumu. Itambue talanta yako ya uongozi na kuiboresha kwa manufaa yako na ya wengine. Watu wenye fikra za mfano wako ni nadra kuwapata. Shukrani za dhati kwako kwa kuanzisha mwendo. I salute you!

Lazydog

I salute you too ladydog, my sincere appreciations
 
Kuna Watanzania wenzetu wenye mapenzi mema na nchi hii ambao wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa na Polisi katika maandamano ya amani huko Arusha. Wengi tuliunga mkono maandamano hayo ila kwa vile tuko mbali na Arusha hatukuweza kuhudhuria hivyo hatukuwa na wenzetu kimwili ila tulikuwa pamoja kimoyo.
Baada ya dhahma ya jana kuna watu waliojeruhiwa ambao kulingana na umasikini tuliowekezewa na serikali ya CCM uwezo wa kujitibu kwao ni mgumu,kwa nini Chadema isianzishe haraka mfuko wa kuwasaidia wahanga wa maandamano hayo kwa utaratibu maalumu ili kuwaonyesha kuwa maumivu waliyopata Chama kinayatambua.
Mfuko huo uwe wazi kuchangiwa na Watanzania wote wenye mapenzi mema na walioguswa na unyama uliofanywa na polisi huko Arusha. Hili nalo litakuwa pigo lingine kwa CCM.
Na hayo mazishi ya hao walio uawa yafanyike kwa heshima zote za Chama na yawe ya kishujaa.
 
naunga mkono hoja............mapinduzi ndio yameanza jana basi tusilale mpaka kieleweke,ikiwezekana yaandaliwe maandamano mengine ya kupinga kitendo cha selikali na jeshi la polisi walichokifanya jana.......
 
Kwani Chadema hawatembelei hapa janvini leo? Mbona hatupati majibu wala maelekezo?

Nadhani zipo sababu za msingi hali kuwa jinsi ilivyo. Nimetembelea Twitter ya CHADEMA na hakuna twitts za mwaka huu, hii inaonesha bado kuna changamoto ya njia iliyo rahisi kuwasiliana na umma - but there is hope.

Pengine ungependa kuweka post yako kwenye Facebook ya Dr. W. Slaa n.k?!
Sehemu nyingine zipo pia ambapo response yaweza kuwa nzuri tu. Blogs zinasomwa na watu wengi.
 
Nakubaliana na wazo lako kaka. Hakika maafa yaliyowafika wenzetu yanatugusa jamii yote ya Watanzania. Binafsi naamini ningekuwa jijini Arusha ningekuwa miongoni mwa wahanga.

Tuko mbali na ndugu zetu wa Arusha ila kiroho tuko nao pamoja. Fikra, mawazo na hisia zetu ni sawa na ndugu zetu wa arusha. Dhamiri zetu zimeumizwa, zimeteswa, zimejeruhika the same way na watu wa Arusha.

Uanzishwe mfuko huo wa maafa nasi tulio mbali tupate kuchangia gharama za matibabu kwa majeruhi, pamoja na maziko ya ndugu zetu waliotangulia mbele za haki. Napendekeza mfuko huo uitwe "MFUKO WA MAAFA WA CHADEMA 2011"
 
For your information, ukienda kwenye FB ya Dr. W. Slaa utaweza kuchuja post uone za Dr. pekee ukipenda.

Bofya "filters"

Dr W. S - FB.JPG
 
Kitila Mkumbo upo, unachukua notes lakini?

Nakubaliana na hili moja kwa moja, waliokufa kwenye "line of duty" lazima wakumbukwe. Nashauri CDM kuanzisha mfuko wa kusaidia walioathirika moja kwa moja na vifo hivyo. Maana mke/mume, watoto (kama wako shule lazima tuhakikishe tuna facilitate kuhitimu kwao).

Kitila ni PM mimi napledge 300,000 Tsh kuanzisha huo mfuko.
 
mm sichangi na niko kinyume kutumia jamiiforums kuchanga kwa watu waliopingana na serikali

ss la kufanya ni kutuma ujumbe mkali na karipio kwa waliosababbisha haya, ambao ni uongozi wa chadema kuwatumia wananchi kwa maslahi yao

Hakuna aliyekwambia kuchangia kama huoni umuhimu wa kufanya hivyo.
 
Kuna Watanzania wenzetu wenye mapenzi mema na nchi hii ambao wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa na Polisi katika maandamano ya amani huko Arusha. Wengi tuliunga mkono maandamano hayo ila kwa vile tuko mbali na Arusha hatukuweza kuhudhuria hivyo hatukuwa na wenzetu kimwili ila tulikuwa pamoja kimoyo.
Baada ya dhahma ya jana kuna watu waliojeruhiwa ambao kulingana na umasikini tuliowekezewa na serikali ya CCM uwezo wa kujitibu kwao ni mgumu,kwa nini Chadema isianzishe haraka mfuko wa kuwasaidia wahanga wa maandamano hayo kwa utaratibu maalumu ili kuwaonyesha kuwa maumivu waliyopata Chama kinayatambua.
Mfuko huo uwe wazi kuchangiwa na Watanzania wote wenye mapenzi mema na walioguswa na unyama uliofanywa na polisi huko Arusha. Hili nalo litakuwa pigo lingine kwa CCM.
Na hayo mazishi ya hao walio uawa yafanyike kwa heshima zote za Chama na yawe ya kishujaa.

na pengo aongoze mazishi
 
Naunga mkono hoja, tulio mbali tunaomba account namba ili tuweke kidogo tulichonacho ili tusizikose hizo baraka. Wenzetu wamechangia damu na maisha yao, vyote hivyo vina thamani sana kwa Taifa hili changa.
 
Sio lazima, hatuangalii dini ya mtu, tunaheshimu uzalendo ulioonyeshwa na wenzetu kwa maslahi ya nchi nzima

unamaanisha nini unaposema nchi nzima? kwani arusha inawakilisha nchi nzima? hayo ni maono yako fniyu kwa taarifa yako hiyo migogoro yenu ya kulazimisha, wengine haituhusu kama huamini fuatilia mikoa mingine utaona jinsi watu wanavyoendelea kula gud time!
 
Kwa kuwa sasa viongozi wetu wako huru, naomba watupe maelekezo kuhusu mawazo yaliyo kwenye thread hii
 
Back
Top Bottom