aafu police wenyewe hawana hata haaaya jana usiku baaada ya taaarifa ya habari ya arusha ilifuata taaarifa ya habari kuhusu makazi yao yaaani wanaishi nyuumba zina ufa hadi mtoto mdogo anaweeza pita.shime shiime wana jf.Hivi sheria za Polisi Tanzania zaruhusu kuua raia? Kimbari yanukia
Ndugu wananchi wenzangu tunaopigania uhuru wa kweli wa nchi yetu ya Tanganyika, poleni sana. Serikali haramu ya CCM katika jiji la Arusha imeua waajiri wake (wananchi), imewajeruhi, kuwadhalilisha, kuwatesa, kuwapiga mabomu ya machozi, kuwarushia maji washawasha, kuwakera, kuwakimbiza hovyohovyo, kuwafarakanisha na familia na ndugu zao, kuwasababisha wasiendelee na kazi zao za kujipatia kipato, na kuwadharau. Imewaweka korokoroni viongozi halali wa wananch, na leo nasikia itawafikisha mahakamani.
Wakati kwenye thread nyingine tunahabarishana kinachojiri na kujieleza hisia zetu, nimeona nianzishe hii thread kuomba na kuelekeza yafuatayo;
1. Tuoneshe heshima yetu ya dhati kwa kuwaenzi wale waliokufa katika harakati hizi za siku ya kwanza ya kudai uhuru na ukombozi wa kweli wa nchi yetu Tanganyika (hata kama ni polisi alikufa). Ndugu, jamaa na marafiki zao watafarijika sana kuona kwamba wamepoteza ndugu zao ambao wanathaminiwa na wananchi wote. Kwanza walio arusha wafuatilie kwa kina details za waliokufa watupatie. Pili, watutangazie tarehe za mazishi kwa kila mmoja wao na eneo/mkoa ambapo maziko yatafanyika. Tatu, chadema wafungue bank account ili tupitishe michango yetu humo kuwafariji waliofiwa. Hii ina maana kama aliyekufa ni bread earner wa familia basi watoto wake wapelekwe shule na mambo kama hayo.
2. Waliojeruhiwa na kulazwa hospitali watambuliwe na kuorodheshwa kwenye tovuti maalumu ya uhuru wa kweli wa Tanganyika (ianzishwe). Kisha walio arusha na wale wanaoweza kusafiri kuelekea huko wawatembelee hawa majeruhi na kuwafariji. Michango yetu pia itumike kugharamia matibabu yao. Wapewe cheti maalumu cha kutambua mchango wao katika kudai uhuru wa kweli ya nchi yetu Tanganyika, ili hata vitukuu vyao viwe na ushahidi wa kujivunia.
3. Kwenye picha za jana, niliona baadhi ya wakina mama wachache sana pale uwanjani. Nilisisimka! Naomba watafutwe nao waorodheshwe na kutambuliwa kwa namna ya pekee. Hawa ndio wanawake wanaojua uwezo wao, siyo wale wanaosubiri kuwezeshwa ndipo waweze. Pia kwenye picha niliona wabunge wanawake wa Chadema na Mke wa Rais wa Ukweli wa Tanganyika, itafurahisha kama watatambuliwa kwa namna ya pekee pia
4. Wapinganaji wenzetu wamekamatwa na polisi na watafikishwa katika mahakama. Tunaomba pia tuchangie gharama za kesi na kujikimu kwao na wale wanaoshuhulikia hili tatizo
5. Tuanzishe kalenda ya ukombozi na kudai uhuru wa Tanganyika, ikianzia tarehe 5 January 2011. Chadema waanzishe kitengo cha kurekodi kumbukumbu za matukio na vitendo vyote kila siku ili vije kutumika kuandika historia ya kweli ya ukombozi wa nchi yetu. Taarifa hizi ziwe wazi kwenye tovuti ili kuepusha kuchakachuliwa kama ccm walivyochakachua histori ya tanzania
6. Kila mmoja wetu katika eneo alilopo, achangie na kugharamia harakati za wananchi wanaounga mkono mapambano ya kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye mikono ya hawa makuwadi, matapeli, majambazi, na wauaji. Eneza habari mtaani kwako, kazini kwako na hata mahali popote unapotembelea. Watu wengi bado wana imani kwamba serikali yetu ni tukufu na hawajui matatizo makubwa ya utawala huu uliopo madarakani sasa hivi.
Sina mamlaka wala wadhifa wa kutoa tamko, bali ni mawazo yangu tu
Mkuu tutafuatilia ili kupata data kamili za watu waliokufa ila kwa vyovyote lazima wapewe heshima yao kwani walijitoa mhanga kwa mustakabali wa nchi yetu. Nafikiri wana JF watapata taarifa kabla ya saa 12 kwamba wamekufa wangapi. Tatizo lililopo ni kwamba Kamanda wa polisi Andengenye hataki kuonana na waandishi wa habari na pia hospitalini hakuna ushirikiano.
mwenye taarifa kamili tafadhali atujuze ni watu wangapi wamafariki huko Arusha na hali ikoje sasa
I am not a Politician, but a proffesional Soldier. I am therefore, man of few words and I have been brief through my proffesional career.
Mmmmmh hata makuwadi wa wake za watu sasa wanajiita Proffessional Soldier..?Wewe unatumiwa tunakuona sasa unataka kuzuga nini?
BBC Swahili wanasema watu 10, AFP 2, hlafu sijui wapi tena 4, jamani ni vigumu kufuatilia na kwa jinsi navyojua serikali yetu wanaweza kuwa wamekufa hata zaidi ya hapo na mkaambiwa ni wawili ama mmoja