Mazishi ya marehemu Yohana Mpinga aliyekufa Ndago - Singida yafanyika

Kama babaye marehemu ni CHADEMA basi yawezekana wauaji ni CCM. Hayo ya msibani kuwa wapo wanaosema ni majungu lakini wewe nini maoni yako kwamba Mwigulu amehusika kuratibu mauaji?
 
Mazishi ya marehemu Yohana mpinga aliyeuawa na vijana wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA yanafanyika hivi punde katika kitongoji cha Kibaya kijiji cha Songambele kata ya Ndago wilaya ya Iramba.

Mkuu wa mkoa, naibu katibu mkuu CCM tanzania bara john Chiligati na mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba na wanaCCM wengi wamejitokeza.

Watu ni wengi sana.

Waombolezaji wanasema waambie jamaa wa upande wa pili waje kuzika. Hawapo hapa hata mmoja.

marehemu alikuwa katibu wa vijana wa ccm wa kata ya ndago


wabunge takribani 7 hadi 8 hivi wa CCM walikuwepo.

CDM haijatuma mwakilishi kama CCM wanavyofanya kwenye misiba ya CDM, kwa mfano wa Regia Mtema, Wangwe na Bob Makani.

Source: Mimi mwenyewe.
Nadhani unahitaji kufikiria kwa mapana zaidi juu ya kutokuwepo viongozi wa cdm. Hivi ccm walimtuma nani kuwawakilisha ktk mazishi ya mkiti wa chadema kule Arumeru? unatakiwe ujue nature ya kifo chake ndo inayofanya yote hayo yafanyike.
 
RIP Yohana Mpinga,
Ila hili liwe fundisho kwa wale wanaopenda kutumwa tumwa na mwiguulu na naape, siku nyingine msikubali mtauwawa bure! ZOMBAa na BUCHOo mpoo? msipoacha ipo siku na nyinyi yatawafika!
 
RIP yohana mpinga, najua haikuwa matakwa yako kuanzisha fujo zilizo gharimu maishaa yako, ni mapenzi ya mwigulu kutumia njaa kali ya wananchi kuwanunua walete fujo. damu yako itamlilia milele

aliemuua ni mnyika,mwita mwikwabe na wafuasi wa chadema.
 
CDM haijatuma mwakilishi kama CCM wanavyofanya kwenye misiba ya CDM, kwa mfano wa Regia Mtema, Wangwe na Bob Makani.

Source: Mimi mwenyewe.

Kwenye msiba wa mwenyekiti wa CHADEMA Arumeru, aliyekatwa shingo na shoka CCM walimtuma nani? Nyamongo walimtuma nani? Yule kijana aliyeuliwa Igunga CCM walimtuma nani? Na kwa nini watu hawa wamekufa, whether ni mwana CCM au CHADEMA?
 
Kujua undani wa hiyo mambo apo Iramba jiulize; (1) wanairamba (kama walivyo wachama kwingineko) wanauchungu gan na Mwigu kiasi cha kushambulia mkutano tena kwa mawe bila 'addition motive behind.'Singida ni sehemu ya kistaarabu haijawah kuw na sifa ya vurugu. Kwa nini leo na kwenye mkutano wa cdm(2) kama kweli ni kashfa za kuwafanya wafuasi warushe mawe mbona mpaka sasa suala hilo linasuasua kuchukua mkondo wa kisheria dhidi ya watuhumiwa wa kashfa.(3) sera na uzungumzaji wa cdm huwa unafanana kote wanakopita,iweje kwinginekn ambako ni majimbo yaliyoko chin ya ccccmm hapakurushwa mawe au fujo zngne za muundo huu.
 
Du hii nchi ilipofikia ni pabaya sana, ccm wako tayari kuua mwenzao ili tu waisingizie chadema kama walivyommwagia tindikali yule kijana wa igunga
 
mwigulu nchemba kama umesababisha fujo hizo damu ya yohana isitoke kichwani mwako na utasumbuka mpaka siku yako ya mwisho umewadanganya watoto wetu kwa uroho na tamaa ya madaraka
 
Shauri yake na kiherehere chake. Yeye alidhani Mwigulu Chemba akili yake iko sawa hadi amuamini akafanye fujo! Matunda ya Mwigulu eti Mwanauchumi daraja A wa BOT ndiyo hayo na ndiyo maana uchumi wetu unaoza kila siku kama wanauchumi daraja A walioko BOT ndiyo aina ya CHEMBA
 
Hizi siasa gani jamani?. Yaani inafikia hatua ya watu kukodi mamluki wa kuvuruga mikutano ya vyama vingine kwa kuwa tu watu hao hawana ajira, hawana kipato na wamelipwa ujira wa chini kabisa wakati wanakuwa subjected to paying of ultimate price (losing life).

Siasa ni uvumilivu kama wewe ngozi yako ni laini jitoe, unajua katika siasa za Tanzania hakuna kijana aliyepo katika siasa leo hii aliyejijengea chuki na dharau toka kwa vijana wenzake kama Mwigulu Nchemba, Nchemba amekuwa na mindset ya backward akili kama za wazee wastaafu wa CCM ambao wanadhani kuwa wao ni bora na wanastahili zaidi ya watanzania wengine. Yaani unamuagiza mwenzako akafanye fujo na kuchochea hasira za watu waliokuwa wametulia katika mkutano wao ili wewe unufaike na madhara yatakayotokana na vurugu hizo?. Ukweli ni kwamba CDM haikuanzia mikutano Ndago, mbona huko kote walipopita hakuuwawa hata sisimizi?.

Nimehuzunika sana na kifo cha Yohana Mpinga kama ndugu yangu wa damu. Yaani tumeishiwa hoja mpaka kufikia kuanza kutumana kwenda kuchokoza watu?, Mimi ninaamini kabisa kuwa kama CDM kingekuwa chama cha vurugu basi kifo cha mwenyekiti wa CDM Arumeru ndugu Msafiri kingeshuhudia viongozi wengi wa CCM wakifuata toka kwa vijana wenye hasira. Lakini busara za CDM za kutuliza vijana wao zimeonekana kana kwamba ni mtaji ambao CCM imeisha upoteza. Matukio ya Maswa wakati wa uchaguzi wa 2010, Igunga na Arumeru yamedhihirisha kuwa CCM inajigeuza kuwa militant party.

Nina hakika kabisa kama polisi wangekuwa impartial kwenye kuteleza majukumu yao yaani hakuna kulinda mtu yeyote awe wa CCM au wa wapi basi kifo cha Yohana na wengine wengi vinge epukika.

I hate Mwigulu Nchemba's mind set of exploiting the poor for their political gain.
 
Nafikiri Mwigulu fani ya siasa itamtupa sasa hivi. Na mbaya zaidi itamtupa vibaya maana hata huko BOT hataweza kurudi tena hata kama kachukua likizo ya bila malipo.

Waswahili husema kuwa ni kama ana 'Gundu' -mdudu anayetumia harufu yake mbaya kama kinga ya kujilinda na maadui. Ninajua strategically amekabidhiwa mikoba ya January Makamba bungeni baada ya January kuukwa uwaziri, ila ameingia na gia mbaya sana. Gia ya kutumia uhuni kupata political advantage. Vyovyote watakavyofanya ni kuwa lawama zote ni kwa Mwigulu, hao waliowakama walikuwa wanajilinza, mbaya zaidi hawakutumia visu wala silaha ya moto bali wametumia sialaha kama zile walizokuwa wanashambuliwa nazo. Hata kama wataset magazeti yote yaandike wanavyotaka wao na polisi wageuze kibao wanavyotaka wao,watanzania wanajua who is the monster in Tanzania, CCM is!.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom