Mazishi ya Mapadri watatu wa kanisa katoliki jimbo la Same waliokufa ghafla yanafanyika leo

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
Mazishi ya Mapadri watatu wa kanisa katoliki jimbo la Same ambao vifo vyao vilipishana kwa siku moja moja yanafanyika katika Seminari ya Chanjare wilayani Mwanga muda huu.

Viongozi wa waandamizi wamehudhuria akiwemo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira

Historia ya vifo vyao

Akizungumza na waandishi wa habari ofisa mawasiliano wa Kanisa Katoliki Jimbo la Same, Padri Joseph Mlacha, alisema mmoja alifariki akiwa katika mafungo; mwingine akiwa katika uchunguzi wa matibabu na wa tatu ni baada ya kupata taarifa za vifo vya wenzake wawili.

“Kwanza, Padri Michael Kiraghanja alifariki dunia Aprili 11 usiku, Maua Kilema akiwa kwenye mafungo. Habari za kifo chake zikawafikia watu mbalimbali wakiwamo maaskofu, mapadri na waamini kwa jumla,” alisema.

Alisema Padri Kiraghanja alikuwa katika hali ya kawaida lakini ghafla alijihisi vibaya na alitumia dawa za kupunguza maumivu na kwenda kupumzika ambapo alifariki dunia akiwa usingizini.

Padri Mlacha alisema uchunguzi wa awali unaonyesha alifariki dunia kwa maradhi ya kisukari.

“Wakati tukiwa katika maandalizi ya mazishi ya Padri Kiraghanja tukapata taarifa ya kifo cha mwingine Arobogasti Mndeme wa Parokia ya Kirangare aliyefariki Aprili 12 katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyoko mjini Moshi alikokuwa amelazwa,” alisema.

Alisema Padri Mndeme alilazwa hospitalini hapo kwa uchunguzi wa kawaida baada ya kufanyiwa upasuaji akiwa na maradhi ya saratani ya utumbo mpana.

Alisema Padri Ulbadius Kindavari wa Parokia ya Bwambo, kifo chake kilitokea Temeke jijini Dar es Salaam.

“Huyu hatuwezi kutoa taarifa kamili kuhusu kifo chake, ila habari tulizopata ni kuwa alifariki baada kupata mshtuko kutokana na taarifa za vifo vya mapadri wenzake wawili,” alisema.


Pia soma > Mapadri watatu wa Kanisa Katoliki jimbo la Same, wamefariki dunia ndani ya saa 72

11.jpg

22.jpg

33.jpg
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,307
2,000
Nime elewa kwamba wamekufa, lakini sijaelewa nini sababu yaku kufa kwa pamoja/kwa kupishana siku moja kila mmoja....
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,307
2,000
Huyo Kiraghinja alikuwa anasumbuliwa na sukari, mwingine alikuwa amelazwa KCMC akisumbuliwa na kansa na huyo watatu yeye ndie wanasema ni ghafla.
Sasa hapo kwenye ghafla ndipo hasa panapo nitatiza Sana, maana aliekufa ghafla ndie aliekua amejiandaa kwenda kuwazika wenzake kwa mujibu wa maelezo.
 

jozzeva

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
2,202
2,000
Kila nafsi itaonja umauti haijalishi lini na wapi na nini chanzo cha kifo,Wapumzike kwa Amani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom