Mazishi ya kikatili ni yepi: Kati ya wahindu wanaochoma mwili kuhifadi majivu, na Mnaozika kwa kufukia mwili kwa rundo la mchanga?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
7,218
2,000
Ustaarabu wa mazishi ulianza tangu enzi za mitume, walihifadhi miili ya wapendwa kwenye mapango ya mawe kistaarabu!

Utaratibu huo wa mitume umerithiwa huko Vatican, makao makuu ya kanisa katoliki, Ambapo Viongozi kama papa na makasisi wakubwa wa kikatoliki huhifadhiwa kistaarabu namna hiyo hadi leo!

Ukitembelea kanisa kuu mjini ROMA! Kuna makaburi yaliyojengwa (pre-casted) kwa ngazi kama mapango ya ngorofa kusubili maziko; kwa ajili ya kuhifadhi makasisi wenye vyeo vikubwa kwa wakatoliki mjini humo!

Utaratibu wa mazishi Ulianza kutofautiana kutoka imani moja kwenda nyingine baada ya mitume na manabii kuondoka!

Mfano ;
Wapo wanaochoma mwili wa marehemu ili wahifadhi majivu nyumbani kama vile album ya ukunbusho (Wahindu)!

Wapo wanaotelekeza mwili wa marehemu uliwe na ndege kama ishara ya utakaso! (Baadhi ya kabila za China na wafilipino)

Wapo wanaozika kaburini kwa kufukia na rundo la kifusi cha mchanga! (Wakristu na waislam hususani Afrika na sehemu ya ulaya)

Wapo wanaotelekeza mwili wa marehemu kwenye nyumba ya msonge pembezoni mwa shamba hadi atakapooza! (Enzi za nyuma za Wamasai, wairaq na wamang'ati Mbulu) N.k

Kila Imani Inashangaa sana imani ya mwingine anavyozika kikatili!

Swali ni Je, imani gani inayozika kistaarabu?
 
All - Rounder

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
2,621
2,000
Ustaarabu wa mazishi ulianza tangu enzi za mitume, walihifadhi miili ya wapendwa kwenye mapango ya mawe kistaarabu!

Utaratibu huo wa mitume umerithiwa huko Vatican, makao makuu ya kanisa katoliki, Ambapo Viongozi kama papa na makasisi wakubwa wa kikatoliki huhifadhiwa kistaarabu!

Ukitembelea kanisa kuu mjini ROMA! Kuna makaburi yaliyojengwa kwa ngazi kama mapango ya ngorofa; kwa ajili ya kuhifadhi makasisi wenye vyeo vikubwa kwa wakatoliki mjini humo!

Utaratibu wa mazishi Ulianza kutofautiana kutoka imani moja kwenda baada ya mitume kuondoka!

Mfano ;
Wapo wanaochoma mwili wa marehemu ili wahifadhi majivu nyumbani kama vile album ya ukunbusho (Wahindu)!

Wapo wanaotelekeza mwili wa marehemu uliwe na ndege kama ishara ya utakaso! (Baadhi ya kabila za China na wafilipino)

Wapo wanazika kaburini kwa kufukia na rundo la kifusi cha mchanga! (Wakristu na waislam husani Afrika na sehemu ya ulaya)

Wapo wanatelekeza mwili wa marehemu kwenye nyumba ya msonge pembezoni mwa shamba hadi atakapooza! (Enzi za yuma za Wamasai, wairaq na wamang'ati Mbulu) N.k

Kila Imani Inashaa sana imani ya mwingine anavyozika kikatili!

Swali ni Je, imani gani inayozika kistaarabu?
Maziko huwa ni Imani na Miiko ya Watu na Koo zao na ukisema ni Maziko ya Kikatili si vyema sana sana utaonekana unadhihaki Tamaduni za Watu.
 
dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
7,218
2,000
Maziko huwa ni Imani na Miiko ya Watu na Koo zao na ukisema ni Maziko ya Kikatili si vyema sana sana utaonekana unadhihaki Tamaduni za Watu.
Asili ya wakiristu ni kuzika kwenye mapango hiyo ndiyo miiko lakini la kufukiana halikuwepo sijui walilipata wapi
 
dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
7,218
2,000
sisi ni wamavumbini na mavumbini tutarudi, hivyo maziko mengine yootee ambayo mfu arudishwi mavumbini ni batili….
Siyo kweli! ukisoma kitabu Mathayo!
Mwili wa Yesu ulihifadhiwa kwenye pango! Hayo mavumbi unayosema ya wapi!
Screenshot_20201218-120118.png
 
Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
10,271
2,000
Asili ya wakiristu ni kuzika kwenye mapango hiyo ndiyo miiko lakini la kufukiana halikuwepo sijui walilipata wapi
Mapango yalitumika kutokana na nature ya Israel kwa wakati huo,Lkn kumbuka hata Yesu alizikwa kwenye kaburi ikiwa na maana kuwa makaburi yalikuwa Yanachimbwa.
 
Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
7,099
2,000
Ukitelekezwa ndege wanafaidi, ukizikwa ardhini funza wako pale... kuteketeza kwa moto ni kuwanyima chakula viumbe ambao wewe uliwala!
 
papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
3,804
2,000
mkuu kurudi mavumbini inamaanisha kuacha kuwepo na si vinginevyo kumbuka kuna watu wamekufa majini nao pia wamerudi mavumbini
hizo zingine ni 'interpretation' zenu, under normal circumstances kila mwili wa mfu unatakiwa kurudi mavumbini….
 
dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
7,218
2,000
soma vizuri biblia uielewe wewee, ni kwanini mwili wa Yesu ulikuwa umeifadhiwa kwenye pango
???
Ndivyo walivyokuwa wakihifadhi miili kwenye mapango! Tena kwa Yesu walimuwekea na Jiwe kubwa kwenye pango! Ilikuwa ni utaratibu wao
 
run CMD

JF-Expert Member
May 31, 2015
1,985
2,000
hizo zingine ni 'interpretation' zenu, under normal circumstances kila mwili wa mfu unatakiwa kurudi mavumbini….
mkuu unamaanisha walikufa baharini na miili yao haijapatikana hawajarudi mavumbini?
 
GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
3,793
2,000
Ndivyo walivyokuwa wakihifadhi miili kwenye mapango! Tena kwa Yesu walimuwekea na Jiwe kubwa kwenye pango! Ilikuwa ni utaratibu wao
Ndomaana siku hizi watu wanajenga makaro wanamuweka na kuweka mfuniko wa zege bila kujaza mamchanga au?? Kwamba wanatengeneza pango lao hahhaaaaa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom