Mazishi ya kifahari ndani ya tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
4170266.jpg


MAZISHI YA ASKARI WA BWANA YESU KRISTO MAJOR NASSON JOHN KITUTA AMBAYE NDIYE MMOJA WA WAANZIRISHI WA JESHI LA WAKOVU HAPA TANZANIA (THE SALVATION ARMY).

MAZISHI YA ASKARI WA BWANA YESU KRISTO MAJOR NASSON JOHN KITUTA AMBAYE NDIYE MMOJA WA WAANZIRISHI WA JESHI LA WAKOVU HAPA TANZANIA (THE SALVATION ARMY)

Azikwa kifahari kama viongozi wa serikali ya Nyerere.

Mmoja wa wanzilishi wa shirika la kikristo la Salvation Army hapa nchini Major Nasson Kititu mwenye umri wa miaka 83 alizaliwa mwaka 1926 june 6 na amefariki dunia tarehe 26 februari katika hospitali ya Mikocheni, na kuzikwa katika shamba lake lililopo Kongowe Dar es Salaam,

Alipata Kujiunga na Jeshi la wokovu mwaka1948 akiwa chunya alifunga ndoa na mke wake 'Maria Kititu' mwaka 1950 katika wilaya ya chunya mkoani mbeya,mwaka wa 1951 aliitikia wito wa kumtumiki mungu kama mchungaji akamua kwenda katika chuo cha uchungaji cha jeshi la wokovu Nairobi.

Baada yakumaliza mafunzo ya uchungaji alianza kazi kama Luteni wa Jeshi la wokovu kanisa la Igunga 1952 hadi 1955

Katika mazishi yake kulikuwa na mvua nyingi ilinyesha kuashiria kuwa alikuwa mtumishi wa mungu mamia ya waumini wakiwemo majirani ndugu jamaa walihudhulia katika mazishi ambayo hakiki yalikuwa kama ya mtu mmoja wa kifahari kabisa na yenye heshima kuu kama mtumishi wa mungu yakiwa yameongozwa na COLONEL HEZEKIEL MAVUNDLA ambaye ni kiongozi wa Mkuu wa makanisa ya Salvation Army Tanzania. ambaye ni raia wa South Africa.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4170266&&Cat=1
 
Kumbe salvation army wanakuwa na vyeo vya kijeshi kabisa! Very interesting...

Alale pema, amina
 
R.I.P mzee wetu. Ukifka huko kama kuna maombi naomba uiombee sana Tanzania, tuwe serious na nchi yetu!!! Na viongozi wetu wawe wazalendo zaidi!!!
 
Katika mazishi yake kulikuwa na mvua nyingi ilinyesha kuashiria kuwa alikuwa mtumishi wa mungu mamia ya waumini wakiwemo majirani ndugu jamaa walihudhulia katika mazishi ambayo hakiki yalikuwa kama ya mtu mmoja wa kifahari kabisa na yenye heshima kuu kama mtumishi wa mungu yakiwa yameongozwa na COLONEL HEZEKIEL MAVUNDLA ambaye ni kiongozi wa Mkuu wa makanisa ya Salvation Army Tanzania. ambaye ni raia wa South Africa.



:confused:Fafanuaa hiyo sentensi !!!!

RIP mzee.
 
Kwanza natoa pole kwa wafiwa wote,bwana alitoa na bwana ametwaa,jina la bwana lihimidiwe.

Pili,nimepata uhakika wa kua kweli hilo ni jeshi kamili,mana lina vyeo MITHILI ya vile vitumiwavyo na majeshi ya nchi ila sina uhakika wa malengo ya kuundwa kwake(JESHI LA WOKOVU) kua ni yaleyale ya ulinzi?kama ndio ulinzi wa vitu gani?

Any way Mwenyezi Mungu anajua zaidi.Ila swali la msingi ni;
Kila dini ikiamua kua na jeshi(lipewe jina lolote liwalo)je itakubalika?na haitaleta Mushkeli?

Naomba kuwasilisha.
 
propaganda tu za "mwanajeshi" wa huyo marehemu! hiyo casket kwenye picha naona wamedownload somewhere...kwenye link waliyoweka pia hakuna picha!! the only interesting story kwangu ni kuwa hawa jamaa wana vyeo vya kijeshi!! lol
 
AMETOKA KWA UDONGO AMERUDI KWA UDONGO, AZIKWE KWA JINSI YOYOTE HAKUNA KITACHOMSAIDIA , BALI NI MATENDO YAKE MEMA ALIYOYAFANYA PALE ALIPOKUWA HAI, NDIO YATAMSAIDIA MBELE YA MUNGU......... tuache ufahari katika misiba.
 
RIP Major wa Jeshi la Wokovu. Haijalishi jeneza liwe la dhahabu tupu na kaburi liwe la almasi tupu, thamani ya mtu ni pumzi yake.
 
mh! inawezekana hii picha wamedownload ............................
R.I.P
 
RIP Mzee Nasson
Kumbe Mvua ikinyesha wakati wa mazishi ni ishara kuwa alikuwa mtu aliyependwa na BWANA. Tujitahidi kuwa watu wema ili mvua zinyeshe wakati wa maziko yetu
 
:confused:Fafanuaa hiyo sentensi !!!!
RIP mzee.
Katika mazishi yake kulikuwa na mvua nyingi ilinyesha kuashiria kuwa alikuwa mtumishi wa mungu

Kuna jambazi liliuwawa huku Mbagala hivi karibuni na siku ya mazishi yake kulikwa na mvua zilizoambatana na ngurumo na radi! Huenda na yeye alikuwa mtumishi mwadilifu wa Mungu .......!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom