MAZISHI ya Hayati Mohamed Ali (Bob) Nyanga Makani, Juni 13,2012

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071
Wakuu

Kesho Juni 13, 2012, Mpambanaji Kamanda Mohamed Ali (Bob) Nyanga Makani, atawekwa katika nyumba na makazi yake ya milele, katika Kijiji cha Negezi huko Kishapu, Shinyanga.

Atazikwa katika kiunga ambacho baba yake, Ali Makani alizikwa. Ni katika eneo hilo hilo pia, ndugu zake wengine kama Zwalo Makani walilazwa wapumzike milele. Atawekwa pembeni yao.

Heshima za mwisho kwa wakazi wa Mji wa Shinyanga na vitongoji vyake zilizoanza tangu saa 8 mchana hadi saa 11 jioni, zilihudhuriwa na maelfu ya watu. Wanashinyanga wamemuaga mpendwa wao, ambaye naye aliwapenda sana wakati wa uhai wake.

Kwa kweli njia nzima wakati tukitoka Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli baada ya msafara uliosindikiza mwili wa Hayati Mohamed Ali (Bob) Nyanga Makani ukijumuisha wanafamilia, ndugu, jamaa, marafiki na viongozi na watendaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutua, ungeweza kuona wananchi kandokando ya barabara walivyokuwa wakishuhudia safari ya mwisho ya mpendwa Bob.

Msafara wa CHADEMA uliongozwa na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Said Arfi (MB), pamoja naye walikuwa ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Musa Yusuf, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika, Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Siale, Ofisa wa Habari Tumaini Makene.

Viongozi wengine, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Tanzania Visiwani, Said Issa Mohamed, Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylivester Kasulumbayi, Ofisa wa Uenezi, Erasto Tumbo walifika baadae wakati tayari mwili wa marehemu ukiwa Uwanja wa Shycom ambako kabla ya heshima kutolewa, zilitangulia dua kwa marehemu kutoka dini za madhehebu mbalimbali, ambapo Shehe wa Mkoa wa Shinyanga alitangulia kuwafungulia mlango wenzake wa dini zingine.

Kesho viongozi wakuu wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti Kamanda Freeman Mbowe (MB na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni), Katibu Mkuu, Dkt. Wilibrod Slaa, Naibu Katibu Mkuu Bara (Naibu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni), wajumbe wa Kamati Kuu, Grace Kiwelu, Ezekia Wenje, Peter Msigwa na wengine watajumuika na wnaanchi wa Shinyanga katika maziko ya Bob.
 
Ahsante kwa taarifa mkuu, Negezi (Ukenyenge) ni nyumbani kama ID yangu ilivyo ukiuliza wenyeji watakupa zaidi!! sikujua kama kamanda Bob alikuwa wa nyumbani!! RIP kamanda Bob. We will miss you!
 
wazee wetu walitujenga kujua tu wewe ni mtanzania, hakukuwa na sababu ya kujuana kwa babila, RIP Bob

Ahsante kwa taarifa mkuu, Negezi (Ukenyenge) ni nyumbani kama ID yangu ilivyo ukiuliza wenyeji watakupa zaidi!! sikujua kama kamanda Bob alikuwa wa nyumbani!! RIP kamanda Bob. We will miss you!
 
Bob umetutangulia, Tunaendelea kupambana, Tutaikamilisha ndoto yako... Bob Pumzika kwa Aman Bob, na mwanga wa milele ukuangazie
 
Mungu amlaze mhali pepa peponi Kamanda wetu Mohamed Ali (Bob) Makani.
Kumuenzi yafaa tuungane na makamanda waliobakia kupitia M4C katika ukombozi wa nchi yetu mkoloni mweusi.
 
Back
Top Bottom