Mazishi ya Bob: CCM na CHADEMA vitapita lakini Tanzania itabaki kuwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazishi ya Bob: CCM na CHADEMA vitapita lakini Tanzania itabaki kuwa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Jun 13, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Leo tarehe 13 June,2012 ni siku ambayo wanachadema na wakazi wa mkoa wa shinyanga hawatoisahau, siku ya mazishi ya kipenzi chao hayati Mohamed Ally Nyanga Makani.Ni siku ambayo ilikutanisha kada mbalimbali kwa itikadi tofauti na misimamo ya kichama tofauti.Ni siku ambayo siasa iliwekwa kando na watu wote kuzungumza umoja wa kitaifa.

  Bob Makani amekwenda,hatutamuona tena lakini maneno,falsafa na vitendo vyake vitaendelea kubaki kwenye mioyo ya wapenda amani wa Tanzania, ikiwa ni kudumisha mshikamano na umoja wa kitaifa kwa falsafa yake ya nawapenda.

  Hotuba mbalimbali kutoka pande zote zilielezea wasifu wake kama kiongozi aliyewapenda na kuwatumikia watu wote bila kujali rangi,dini na itikadi za kichama.Mbali na hotuba hizo,hotuba iliyowagusa sana watu na kuwaacha watu wakiitafakari kwa kina ni hotuba iliyotolewa na mh. Mbowe mwenyekiti wa CDM taifa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.Maneno yake ya majonzi yalibeba ujumbe mzito juu ya amani na mshikamano kwa taifa letu.

  Kamanda huyu alifika mbali sana kiasi cha kusema mshikamano ulionyeshwa leo usiishie hapa,na kesho yake mnyukano ukachukua mkondo wake katika harakati za kisiasa kuelekea kushika dola.Amani ya Watanzania ni muhimu kuliko CCM na CDM,CDM na CCM vitapita lakini Tanzania itabaki pale pale.

  Maneno haya ya mh. Mbowe yawe changamoto kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu,maneno haya mara nyingi yamekuwa yanasisitizwa na hayati Bob Makani,Watanzania tusikubali kugawanywa kwa minajili ya kidini,kikabila na kikanda kama propaganda chafu zinazojaribu kupandikizwa na watu waliochoka siasa za kistaarabu.Kwa mantiki hii msiba huu uwe changamoto na mtaji wa rasilimali amani ambayo wengi wanaililia.

  Mwisho,tujifunze mengi mema aliyoyafanya mzee wetu huyu,tuwe wazalendo wa kweli na kuipigania nchi yetu mama Tanzania katika kudumisha amani ,ndio njia pekee itakayo weza kuimarisha uchumi,lakini tunda hili la amani likidondoka na uchumi wetu pia utaangamia.Upendo na uzalendo iwe ndiyo mhimili mkubwa katika ujenzi na maendeleo ya taifa hili.Mungu ibariki Afrika ,Mungu ibariki Tanzania.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kichwa cha Habari Hakieleweki na Hii habari tumeisha sikia; let him rest in PEACE; OH LORD!!
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Kumuita Bob Makani "Mohammed Ally" ni sawasawa na kumuita Muhammad Ally "Cassius Clay". Tacky and disrespectful.
   
 4. n

  nsami Senior Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye nyekundu nimepapenda zaidi asante sana kamanda yetu mbowe Mungu akujalie umri mrefu!
   
 5. B

  Bob G JF Bronze Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Bob Makani Mungu ilaze mahala pema peponi Amen
   
 6. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hilo ndilo jina lake halisi,Bob ni nick name tu.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Una hakika?

  kule Tanganyika Law Society register yao inatumia nickname nayo?

  Tena karibu wenzake wote wametumia initials kwa majina yasiyo ya mwisho, yeye kaamua kuandika "Bob Nyanga Makani" in full as if alikuwa hataki utatanishi wowote kuhusu jina lake.

  Huyu Mzee alikuwa mwanasheria, alibadilisha jina lake legally. Kama mnamuheshimu heshimuni uamuzi wake huo.

  Angalia namba 131 http://www.tls.or.tz/pdf/rolls.pdf


   
 8. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Usiku mwema wakuu!

  Rest in peace bob.
   
 9. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hilo ndilo jina lake la dini,Bob alilipata alipokuwa mchezaji maarufu wa mpira wakati anasoma Tabora Low School,kama unabisha muulize mzee Mtei walisoma wote au Victor Metusela
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Mzee Mtei na Victo Metusela ndio wanaoamua somebody's legal name?

  Kama alilipenda sana hilo jina lake la dini sana mbona alichukua all the trouble to change his legal name?
   
 11. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  Hapo mmeniacha kidogo! And who is Victor Metusela?
   
 12. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Metusela ni muasisi cha CDM na mtu waliyefanya naye kazi bega kwa bega ndani ya CDM na nje ya chama ambao walifahamiana toka mwaka 1951.Pia Metusela ni mjumbe wa bodi ya udhamini wa CDM.
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimefurahi kujua jina lake asilia, maana hii inaongeza credit kwa CDM, Hasa wale waliopenda kuzungumzia mambo ya udini.
   
 14. F

  Froida JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mbowe ameongea neno la busara sana ,waroho wa kisiasa wasituvuruge kwa kutugawa kwa udini watuachie nchi yetu salama
   
 15. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Na kila mpenda amani atajua kuwa nchi hii ni yetu sote,hakuna mwenye mamlaka zaidi ya Watanzania wote.Pia nimpongeze JK kwa kumshushua katibu mkuu wake aliyetaka kuuwadaa umma kwa propaganda chafu za kuligawa taifa kiukanda,na kusahau tunajivunia Utanzania wetu na si udini,ukabila wala ukanda
   
Loading...