Mazishi ya baba yake Selasini kuwa vita kati ya CHADEMA na CCM?

Jumanne Mkota

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,917
1,660
Wanabodi Salaam,

Habari za kusikitisha hizi Jamani. Baba wa Mbunge wa Rombo ambaye pia ni diwani wa CCM Halmashauri ya Rombo yupo Mochwari. Mwenyez Mungu amempumzisha. Magamba ya Mkoa wa Kilimanjaro yakiongozwa na Katibu wao wa Mkoa Steven Kazidi yanapanga kuyafanya mazishi haya kisiasa tena siasa za nani ziadi kati ya CCM na CDM.

Wameagiza makatibu wao wa Wilaya waje na wafuasi wengi kadiri itakavyowezekana kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro na wilaya jirani za mikoa ya Tanga Arusha na Manyara. Wanamshirikisha mtoto mwingine wa Marehemu Masumbuko Lamwai ili kufanikisha aibu hii wao wakijua kuwa ni ufuniko dhidi ya CDM. Waomblezaji hao watavaa sare za Chama chao. Lengo lao kubwa ni ili viongozi wa CDM watakaokuja washindwe kufurukuta na pia wakose pa kukaa. Lengo hasa wanasema itapendeza zaidi Mbowe na Slaa kukaa mgombani.

Habari hii nimeipata ndani kabisa ya moja ya vikao vya kamati za siasa vya wilaya mbili za Moshi Mjini na Moshi vijijini ni habari za uhakika nafuatilia kwa karibu wilaya zingine.
 
bangi zako usilete hapa wenzako wamefiwa wewe unawashwa na uchadema aibu gani hiyo
marehemu amekufa akiwa mwanachama na tena kiongozi wa watu kupitia CCM sasa wewe unatekenywa na ninin?
 
Dah! inasikitisha sana kusema kweli!!! Kwanini magamba wasimuachie mtoto wa marehemu akaamua anataka mazishi ya mzazi wake yaweje? Chuki mpaka kwenye vifo/mazishi!? Kweli nchi imefikia mahali pabaya sana.

Wanabodi Salaam,

Habari za kusikitisha hizi Jamani. Baba wa Mbunge wa Rombo ambaye pia ni diwani wa CCM Halmashauri ya Rombo yupo Mochwari. Mwenyez Mungu amempumzisha. Magamba ya Mkoa wa Kilimanjaro yakiongozwa na Katibu wao wa Mkoa Steven Kazidi yanapanga kuyafanya mazishi haya kisiasa tena siasa za nani ziadi kati ya CCM na CDM.

Wameagiza makatibu wao wa Wilaya waje na wafuasi wengi kadiri itakavyowezekana kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro na wilaya jirani za mikoa ya Tanga Arusha na Manyara. Wanamshirikisha mtoto mwingine wa Marehemu Masumbuko Lamwai ili kufanikisha aibu hii wao wakijua kuwa ni ufuniko dhidi ya CDM. Waomblezaji hao watavaa sare za Chama chao. Lengo lao kubwa ni ili viongozi wa CDM watakaokuja washindwe kufurukuta na pia wakose pa kukaa. Lengo hasa wanasema itapendeza zaidi Mbowe na Slaa kukaa mgombani.

Habari hii nimeipata ndani kabisa ya moja ya vikao vya kamati za siasa vya wilaya mbili za Moshi Mjini na Moshi vijijini ni habari za uhakika nafuatilia kwa karibu wilaya zingine.
 
Mimi huwa naanza kuingiwa na wasiwasi na baadhi ya watu! Hivi huyu mzee wa watu akizikwa na wavaa kijani milioni moja atafufuka? Akizikwa na CDM wote Tanzania atafarijika zaidi? Mi nafikiri busara hapa ni kuweka itikadi za kisiasa pembeni na kumsindikiza Mzee wetu katika safari ya mwisho hapa duniani. Nyie njooni tu! Vaeni khaki, kijani, blue, red whatever! Hata msipovaa! Lengo ni moja tu KUJUMUIKA NA FAMILIA YA MAREHEMU KATIKA KIPINDI HIKI! R.I.P Baba.
 
Badala ya kutumia tukio hili kuongeza uhasama, CCM na Chadema wanaweza kutumia mkusanyikohuo kujenga utamaduni wa kufanya siasa bila kupigana kwa sababu kifo hiki cha Mzee kinaonyesha kuwa watanzania tu watu wamoja
 
jamani hii ni JF?tunafanya masihara hata na msiba?

Mazishi ya baba yetu hayawezi kuwa vita ya kisiasa hata kidogo.Mh Selasini na Lamwai wana upeo mkubwa sana kwenye hizi shughuli za kijamii na ndio wanaoratibu suala lote la Msiba. Nawahakikishieni kuwa mazishi yatakuwa shwari na itifaki itazingatiwa mwanzo hadi mwisho. Naomba suala hili lisiendelee kuwaumiza vichwa tuwaachie wanafamilia kwani wamejipanga kisawasawa.
 
Mnageuza matatizo ya watu kuwa mtaji wa kisiasa ee?subirini laana yake sasa.
 
Back
Top Bottom