Mazishi Naibu Meya Morogoro yasitishwa, mwili warejeshwa mochwari

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
SINTOFAHAMU ya mazishi ya aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, marehemu Isihaka Sengo imesababisha mganga mkuu wa manispaa hiyo, Ikaji Rashid kuwatawanya waombolezaji nyumbani kwa marehemu mpaka mwili wa mrehemu utakapofanyiwa uchunguzi wa kitabibu.

Utata huo ulijitokeza punde baada ya Mganga Mkuu Manispaa ya Morogoro, Ikaji Rashid kufika nyumbani kwa marehemu majira ya mchana jana na kuwakuta ndugu na jamaa wakijindaa kwenda kuzika kisha kuwataka kusitisha zoezi hilo na mwili kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa uchunguzi.

Mganga huyo alisema, baada ya ofisi yake kupata taarifa kutoka hospitali aliyokuwa akitibiwa kwa mara ya mwisho kuna viashiria vya marehemu kuwa na maabukizi ya virusi vya Corona (COVID-19).

“Serikali inasitisha mazishi hadi itakapotangazwa vinginevyo na mwili unakwenda kuhifadhiwa chumba cha maiti, mwili huu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na hapo tutachukua sampuli leo (jana) na kuzituma Dar es Salaam kwa uchunguzi,”alisema Mganga Rashid.

Source, TimesMajira

Soma >>>> Diwani wa kata ya Kiwanja cha Ndege, Morogoro Afariki dunia,

========

April 28, 2020
Morogoro, Tanzania

Mkuu wa Mkoa : Mwili wa Naibu Meya uzikwe mara moja

Mkuu wa Mkoa Morogoro : Serikali haiwezi kusubiri majibu ya maabara, Naibu Meya alike mara moja



Source : millard ayo
 
Mwili tayari ulishafika nyumbani, mgonjwa alihudumiwa kama mgonjwa wa kawaida, mgonjwa alikuwa na ukaribu na watu wanaomzunguka.

Serikali imeamua kutotangaza, what does it mean? Tubaguane kwa sababu hatujui nani kakutana na nani muda gani, nani anatakiwa kuwa karantini ila hayuko.
 
Maombi ya siku tatu naona hayakusaidia, tulikua tunawacheka mabeberu kua wao wanatumia sayansi sisi tunajifanya tunamjua mungu aliyeletwa na haohao mabeberu wakati wa ukoloni. Mziki tumeanza kuusikia sasa. Endeleeni kuomba badala ya kujikinga.

Nashangaa kila mtanzania nayempigia simu nyumbani huko namuuliza hali vipi anajibu tuombe mungu tu, hivi dini ya mkoloni imewageuza matahira? Huku nje kila nayemtafuta ananiambia anakaa ndani anavaa na mask, akitoka nje anahakikisha anakua mbali na watu, kweli kuna matabaka ya akili duniani, huyu mungu wa waafrika huyu amegeuza watu wamekua wavivu mno wakifikiria kila kitu atawafanyia, stupid africans
 
Pathetic! Hivi kupima COVID19 ni mpaka Dar?
Jana nimeona kwenye taarifa ya habari Aljazeera

Wanayansi wa Senegal,ndio Senegal nchi iliyoko Afrika ya Magharibi wameanza kutengeneza kifaa Cha kupia Covid19 kilicho fanana na kile wanachotumia wanawake kupima uja uzito,kwahiyo kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua na kujipima

Wanyaruanda nao Hawako nyuma,wametengeneza Ventilation yao mwenye badala ya kuagizia nje ambayo Bei yake ni €170000 kwa kila moja

Swali la kichokozi, wasomi na Wanasayansi wetu wako wapi,au ndio wanakimbilia kuwa wanasiasa na kuacha fani zao??
 
Jana nimeona kwenye taarifa ya habari Aljazeera

Wanasansi wa Senegal,ndio Senegal nchi iliyoko Afrika ya Magharibi wameanza kutengeneza kifaa Cha kupia Covid19 kilicho fanana na kile wanachotumia wanawake kupima uja uzito,kwahiyo kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua na kujipima

Wanyaruanda nao Hawaii nyuma,wametengeneza Ventilation yao mwenye badala ya kuagizia nje ambayo Bei yake ni €170000 kwa kila moja

Swali la kichokozi, wasomi na Wanasayansi wetu wako wapi,au ndio wanakimbilia kuwa wanasiasa na kuacha fani zao??
Walimu ni bora ila madakatar nao ni kisangaaaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atembee kama DUME LA NYANI huku akisema tumevishinda vijimafua,sisi ni nyani hatuwezi kufa kwa vijimafua.Tumekaa na malaria,ukimwi miaka na miaka sembuse haka! kweli sisi tumetoka kwa manyani!!
Acha woga wewe Nani kakuambia wanaccm wanapata corona??
Wewe utakuwa mwanaccm mjinga-mjinga au Ile kauli ya magufuli tusitishane umeisahau? Sisi wanalumumba hatuwezi kupata corona pia tembea kifua mbele

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
Mwili tayari ulishafika nyumbani, mgonjwa alihudumiwa kama mgonjwa wa kawaida, mgonjwa alikuwa na ukaribu na watu wanaomzunguka.

Serikali imeamua kutotangaza, what does it mean? Tubaguane kwa sababu hatujui nani kakutana na nani muda gani, nani anatakiwa kuwa karantini ila hayuko.
Rafiki, hapa usisubiri kutangaziwa. Fanya 1+1=2. Kwisha!
 
Back
Top Bottom