Mazingira yanayoruhusu mke kumbambikizia mume watoto

Je, mwanaume atajisikiaje kugundua kuwa mtoto aliyedhania ni wake kumbe si wake? na hasa ukizingatia alitengeneza uhusiano na mtoto huyo?

Kwa wale wa enzi zetu, tulielezwa kuwa na wewe inakuwa siri yako ya kufa nayo, as longer as mtoto anaendelea kukuita baba! Ila kama limelipuka na mtoto kaelezwa, unakubaliana na hali!!

Mateso ni kwa ajili ya binadamu na hilo sasa linakuwa zigo lako.....

Kijijini kwetu kuna jamaa alikwenda kufanya kazi mjini, alikuwa anakuja mara moja moja likizo. Aliporudi baada ya kustaafu akakuta mke wake ana watoto 2 (may be na zaidi) ambao si wake.. Kwa mwanekano na ushahidi wa mama yake....Mzee wa watu amelea na kusomesha + kuoza!! Hadi sasa watoto wanamjua ndiye baba yao!! ....Kwa Waafrika tulio wengi, KITANDA HAKIZAI HARAMU!!! Labda kama hawa vijana wa dot com watakuja na version mpya!!
 
Unajua kila crime unaifanya wakati unajua kuna risk ya kushikwa. Unalazimika kufanya kutokana na mazingira ya wakati huo

ikitokea ikajulikana kweli wanamme huumia sana, tena sana lakini hapo napo busara ya mwanamme kuwakubali au kuwakataa ndo hupimwa.

Ila inaonekana kuwakataa watoto huwa inawaumiza zaidi kuliko wanaoamua kuwakubali. Sijafanya kauchunguzi kujua ni kwa nini

hata kwa watoto huwa ni pigo hasa anapokuwa kwenye umri wa kutambua yanayotokea around yeye.

Je, mwanaume atajisikiaje kugundua kuwa mtoto aliyedhania ni wake kumbe si wake? na hasa ukizingatia alitengeneza uhusiano na mtoto huyo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom