Mazingira yanayoruhusu mke kumbambikizia mume watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazingira yanayoruhusu mke kumbambikizia mume watoto

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 6, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Katika pita pita zangu na uzee huu nimekutana na mengi; yapo ya kusikitisha, kuchekesha na mengine ya kuudhi. Yapo mazuri na mabaya na mengine ya ukichaa kabisa. Lakini kati ya ambayo nimekutana nayo kwa muda na katika mazingira tofauti (bongo na nje) ni hili ambalo mwanamke anajikuta katika mazingira ambayo analazimika kumbambikizia mtu mimba. Na wengine huenda kaburini na siri hiyo kuu ambapo mtoto au watoto wanaweza kufikiri fulani ndiye baba yao kumbe ni mtu mwingine kabisa.

  Lakini wengine wanajikuta wanalazimika kumbakizia mtu mtoto kwa sababu ukweli au mtu ambaye kweli anahusika wanajua asingepewa hadhi hiyo ya kuwa baba. Sasa najiluliza ni kweli kabisa mazingira kama hayo yapo kama inavyodaiwa au wakati mwingine ni woga labda kama wangeamua kumwambia mhusika ukweli labda angeelewa na kukubaliana nao. Lakini, kama mhusika hatoambiwa ukweli itakuwaje kama baadaye waje kukutana na kufall in love au watoto wao kukutana kumbe ni ndugu?

  Maslahi ya mtoto katika mazingira hayo yanakuwa wapi?
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Katika mambo ya animal reproductive biology, partner wa kuzaa naye lazima awe na vigezo muhimu ikiwemo sifa ya kuwa baba au mama wa watoto wako.

  Na inapotokea mtu au mnyama akawa na nafasi ya kuchagua, automatically, the best candidate will be given the first priority... Katika hili, maslahi ya mtoto ni secondary au hayana nafasi kabisa hadi hapo puzzle itakupokuwa imepata suluhu!

  Kama nilivyowahi kusema, not every ejaculation deserves a name and similarly, not every man has the husband or father qualities!!

  Babu DC (1947)!
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Ntarudi baadae MMK maana kamba zako huwa sio za kuzishobokea kitoto, mtu unahitaji kufikiri kabla ya kuchangia. Ntarudi baadae!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo DC, una maana ni kweli kuna mazingira ambayo yanahalalisha mwanamme kubambikiziwa mimba au mtoto? na wanawake huwa wanalifikiria jambo hilo hawakurupuki?
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Absolutely,

  Lipokuja suala la nani anaweza kweli kuwa baba wa mtoto, wenzetu wako very strategic!!

  Na ndiyo maana kuna hadithi kibao za wanawake single kuwaomba au kuwategeshea baadhi ya wanaume wawazalishe hata kama biashara itaisha baada ya hapo!!

  Kuna dada mmoja mzungu alimwambia rafiki yangu kwamba huko kwao (Belgium), wanawake wanachagua sana watu wa kuzaa nao. Hakuna dada yeyote asingependa kuzaa na star (in academics, business or sports ect.) ila pia hakuna ambaye yuko tayari kuzaa na lofa.....Rejea utani wa wapare na wachagga.......!!!
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Halafu MMM,

  Kuzaa na mtu na mambo ya kujirusha + ngono ni vitu tofauti kabisa...Hata vigezo vyake vinatofautiana sana, especially kwa dada zetu!!
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Kwa manamke kubambikiza mtoto kuna sababo tofauti tofauti za kimazingira, baadhi ni
  1. Uko kwenye ndoa, unapiga mechi ya mchangani, unanasa mimba, inabidi umbambikize mme kuficha aibu na kulinda ndoa.

  2. Mwanamke ulikuwa na wapenzi zaidi ya mmoja na ukakutana nao katika ovulation period hiyo hiyo afu unapata ujauzito, inakuwa vigumu kujua ni wa nani. Hii huwa ni complecated maana hadi kwa msaada wa DNA. Kwa case hii anayekuwa weak anabambikwa ujauzito

  3. Mwanamke anakuwa kwenye mahusiano zaidi ya mtu mmoja, afu anapata ujauzito inabidi ambambike mwenye maslah mengi kwa ajili ya future ya mtoto.

  4. Wakati mwingine unambambika mtoto mtu kulipa kisasi kwa aliyowahi kukutenda.
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa vile haya yametoka kwa mdau nambari wani, mie siongezi neno...Ila kuna ka-ukinzani kidogo kati ya Na3 na Na4. .....Anachaguliwa aliye weak kwa jambo gani???
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  hata kwa wanamme ni the same, ndo maana mwataka oa wanawake decent ili wawe mama wa watoto zenu.
  Na mara nyingi mwanamme akiona kampa mimba kicheche suluhisho la kwanza huwa anamwambia akatoe maana hataji kujiassociate na low specie

   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ni kweli ila kuna baadhi ya wanaume ambao hawajali kama mbegu zao zimendondoka kwenye miiba au mwamba....Wanatimua na kumwachia mama wa watu mzigo...Mfano mzuri ni yule Boss wa Geshi letu la Maafande na maid wake!!
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  unakuta unawanamme wanne, afu wote unapiga nao mechi ovulation moja.
  Mara nyingi type hizi huwa vicheche na wanamme huzikataa mimba. Anaenda kwa wa kwanza akikataa anamfuata wa pili akikataa anamfuata wa tatu akikataa anamfuata wa nne.
  Wote wakikataa anaamua kula sahani moja na yule ambaye anaona ni weak kwake au atakubali kirahisi.

  Hiyo ya nne huwa full kisasi, napata mimba kwa mtu mwingine, nakuja kukutega just one day, then nakukabidhi zigo lako. Afu mie naenda vuta mshiko kwa walionituma public figures

   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Sitakimbilia kwenye conclusion
  vifua vya wanawake vina mengi
  ila hii DNA teknoloki imetuharibia kabisa
  watu wanabambikwa skendo and pipo get paid

   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwenye suala la ngono na watoto....Mhhh...vingekuwa extendible, hivyo vifua vingetanuka kama balloon za kujaza kijijii kizima!!
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Lakini ni kwa muda gani mwanamke anaweza kutunza hiyo siri?
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wengi wanakufa nazo...Ukipata bahati ya kuwa na ndugu wa namna hiyo, na pia akawa na bahari ya kuugua hadi kufikia mahali akajua kuwa amefika ukingoni, basi unaweza kuambiwa.

  Mara nyingi wanaenda nazo kwa Muumba!
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  hii inategemea na how smart a woman is?
  Wengine wanasave for life time, wengine hadi watoto wanakua kiasi cha kuweza kujitegemea.

  We call it IT (Individual Talent)

   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nafikiri wanawake wa bara (mikoani) ndio wana hizi tabia..

  Mkuu mwanamke wa pwani (mwambao) kila mtoto babake anajulikana tu..

  At least wanaweza kujimwaga (hawana vitu vingi vifuani mwao)
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Ubara na upwani hausaidii.

  Wao wabara sisi wapwani
  wao wapwani wa visiwani sie sio wa visiwani
  wao wa kakazini karibu na kenya sie wa karibu na msubiji

  wangapi wapwani wanalea mamluki tena kati ya mme wa mtu na mke wa mtu

   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Je, mwanaume atajisikiaje kugundua kuwa mtoto aliyedhania ni wake kumbe si wake? na hasa ukizingatia alitengeneza uhusiano na mtoto huyo?
   
 20. M

  Malova JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  nimejifunza mengi hapo
   
Loading...