Mazingira yaliojenga msimamo mkali wa madaktari... Utamu wa ngoma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazingira yaliojenga msimamo mkali wa madaktari... Utamu wa ngoma!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jackbauer, Jul 3, 2012.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hebu tujadili kwa kina bila hisia kali.
   
 2. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,279
  Likes Received: 10,465
  Trophy Points: 280
  posho ya mbunge yaongezeka kwa asilimia 15.liwalo na liwe!
   
 3. I

  Imaima Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana macho lakini hawaoni! wanamasikio lakini hawasikii na sababu kubwa ni kuwa Mungu kaamua kuwaangamiza! mwisho wa haya hauko mbali. ukiona usiku umeendelea tambua kuwa mchana umekaribia
   
 4. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,279
  Likes Received: 10,465
  Trophy Points: 280
  pamoja na watumishi wachache tukionao katika sekta ya afya lakini hatuoni thamani yao.huu ni udhalimu.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 5. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  serikali ikiongozwa na jk inataka tuamini kuwa eti madaktari wanadai posho tu,kitu ambacho si kweli.mazingira ya vituo vyetu ni mabaya sana na hakuna wa kulisemea hili zaidi ya wale wenye uzoefu na mazingira hayo madaktari wakiwemo.wale tuliowachagua kutusemea pale mjengoni wamebaki kupeana mipasho tu kwa kuwa wanatibiwa india.
  Ni ukweli usiopingika kuwa tumewekeza kidogo sana kwenye sekta ya afya kwa sababu hatuoni kuwa ni productive huku tukisahau mkulima hawezi kulima iwapo afya yake ni mbovu,pia tumesahau kuwa maendeleo hupimwa kwa kuangalia mfumo wa afya uko vipi.

  Vipaumbele vya nchi hiivimeelekezwa katika starehe tena za viongozi tu.
  Fedha zimeenda kuhudumia wabunge,mawaziri na makatibu wakuuhuku tukiwasahau wananchi wafanyakazi na wakulima.

  Tumejenga matabaka katika nyanja zote kwani hata wale wenye elimu bora ni watoto wa vibopa tu.

  Kila siku tunasema hatuna hela pale madai ya huduma za jamii yanapozuka mfano afya,elimu n.k

  tunasifika katika kuuza madini lakino kipato chake hatukioni!huu ni usaliti kwa wapenda haki na maendeleo nchini.

  Viongozi na washirika wao wamejaa viburi ile mbaya kwa sababu tumewanyamazia kwa muda mrefu.

  Naamini kuwa jambo kubwa huanza na dogo, mgomo wa madaktari ni sehemu ya mambo makubwa yaliyoko mbeleni.

  Songeni mbele madaktari kwa kuwa kila mpenda haki yuko nyuma yenu.
   
 6. oba

  oba JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Point of correction; kusomea udaktari si bure, kuna rafiki yangu anakatwa 70000 kila mwezi kulipa mkopo wa elimu ya juu, na madaktari wengine ni mashahidi, kama wapo humu jamvini watakubaaliana na mimi
   
 7. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,167
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  dentist binti jk ni mdeni bodi ya mikopo. Yumo kwenye list
   
 8. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,167
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Jk akiwa kwny sherehe 1 kule botswana aliwaomba wa tz wanaofanya kazi kule warejee nyumbani
   
 9. Medical Dictionary

  Medical Dictionary JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,053
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  mkuu naomba kuuliza..kikao cha jumuiya ya madaktari ambacho kilitangazwa kuwa kitafanyika leo vipi kilifanyika..?
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Unazungumza vitu gani hapa.. Unajua gharama ya kuupata Udaktari kiasi kwamba unatumia Tsh 70,000 kama malipo na gharama?. Kwanza wenzako huko ncje mnakopenda sana kutumia mifano,kuomba tu nafasi ya kusoma hutozwa Usd 100 hadi 150 na hairudi, hii ni kupokea ombi lako leo wewe waja na hizo Tsh 70,000.

  Sikieni nyie Madaktari mmesomeshwa bure kwa malengo yetu ya Kitaifa toka mwaka 1968. Nalo ni kupata wadaktari wa kutosha ktk kupambana na adui Maradhi hivyo vita hii inatakiwa Uzalendo kwanza na sii fedha maana kama kweli mnataka tuende kibepari basi kila daktari akubali kurudisha gharama zote zilizotumika kumsomesha halafu tufuate market rate ya madaktari..

  Tunafahamu uzembe wa serikali hii na wala sii Kikwete tu bali toka Mwinyi japokuwa Nyerere aliweka malengo ya kitaifa toka mwaka 1968 lakini ilipofika mwaka 1992 kutangazwa kwa Azimio la Zanzibar kila kitu kimekuwa Chukua Chako Mapema. Uzembe huu wa serikali pamoja na mfumo mbovu wa kuweka dhamana ya dira yetu kitaifa mikononi mwa mafisadi ndio sababu kubwa ya sisi kushindwa kuendelea. Kuna habari nyingi sana za ufujaji fedha ktk wizara, idara, Jumuiya na Hospital zetu, toka tender za vyakula, uniform, na hata uagizaji wa madawa zinatia aibu kubwa hata kusimulia..

  Mtu anaona amepata deal kubwa Muhimbili wakati anajua fioka analiibia Taifa lakini mwepesi kulalamikia JK wakati haikuanza jana. Watanzania wenzangu tuwe makini na turudi ktk basic, tusichafuliwe na jinsi hawa viongozi wetu wanavyopora mali zetu badala yake sisi tuwe makini zaidi na kuwaumbua ipaswavyo.

  Kazi kubwa ni kutafuta chama mbadala na kukiweka madarakani, chama ambacho kiko tayari kurudisha malengo ya Utawala bora ni pamoja na kupambana na maadui wetu wakubwa watatu. UMASKINI, MARADHI, na UJINGA. Kwa kutambua hivyo tumchague kiongozi ambaye anaweza kutuongoza sisi wananchi ktk mapambano hayo na sii vinginevyo kiasi kwamba swala la mishahara liwe kukidhi mahitaji yetu muhimu na sii kuweka madai makubwa kwa sababu viongozi wetu wanapewa. Haiwezekani hivyo basi Ya Egypt na Tunisia ndilo jibu pekee ya kumaliza mgogoro wote.

  Dawa pekee ni sisi wananchi kusisitiza kukata mishahara ya viongozi iwe chini ya wataalam. Nina hakika kama Mbunge atapokea 700,000 na daktari 900,000 sidhani kama tutakuwa na ubishi huu, lakini hatuwezi kuongeza mishahara ya watu iwafikie wabunge iwe ndio kigezo cha malipo bora kwa kazi ambayo sisi wenyewe tunasema Wabunge hawasitahili sasa tunaogopa nini kusema wabunge washushiwe mishahara!

  Tuandamane, tufanye mikutano na kadhalika kupingana na wanasiasa hawa wanaotumaliza tukiwa hai bado. Haya ya kuwapa magari na nyumba wakati tunashindwa hata kununua dawa na vifaa, wanawake na watoto wetu wanakufa ktk kuzaa - Haikubaliki. Maana zamani tukisema Mimba sio Ugonjwa lakini sii leo hii tena.. Mimba ni nusu ya kifo!
  Tutaweza vipi kupambana na adui huyu kwa tamaa kama hizi?
   
 11. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hata mimi nalipa hiyo hela.isitoshe wazazi wangu wanalipa kodi na pia baba yangu amerushwa hela yake ya kustaafu east africa community.nina hasira sana na hawa madhalimu.
   
 12. Mwananchi Mtanzania

  Mwananchi Mtanzania Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Toka mgomo huu ulipoanza, nimekua nikijiuliza maswali mengi kadiri siku ziendavyo. Lazima nikiri kwamba na mimi nilitumbukia katika mtego wa kulaumu upande mmoja wapo kabla ya kujiuliza vizuri... Ama baada ya kutafakari kwa kina, nikagundua kwamba kwa vyovyote vila itakavokua, tunaoathirika ni sisi wananchi, bila kujali tunaunga mkono madaktari au serikali.


  Nilianza kujiuliza hivi: Hawa wanasiasa wanaotupiana mpira, mara CHADEMA, mara CCM, bila kujali vyama vyao, wanatibiwa wapi kwa kawaida? Hawa kwani hawana madaktari maalum ambao wanawalipa binafsi? Hivyo basi, huyu kiongozi anayesema fukuza, hakutani na daktari wake binafsi ambaye huenda anatugomea sisi wananchi? Mimi mwananchi wa kawaida ambaye sijuani na daktari na wala sina pesa, nani atanitibia?


  Je, nikisema serikali ifukuze madaktari wote, nani atanitibia? Nikisema pia wagome, kwani nikienda hospitali wataniuliza kama nawaunga mkono ili wanitibie? Au ndio yale ya "naunga mkono mgomo", lakini kwa sababu mimi sina jamaa daktari, au sio daktari, basi sina wa kunitibia. Lakini wao wanasema wananisaidia, ilihali wananiacha nateseka na wao wakitibia ndugu na marafiki zao!


  Baada ya kuangalia hali yangu na hao viongozi wa siasa, bila kujali vyama vyao, nikajiuliza maswali mengine: Je, miongoni mwa madaktari wanaogoma, hawana wateja wao binafsi ambao ndio hao hao mawaziri wanaowatuhumu kufisidi sekta ya afya? Je, mawaziri hawa wakienda katika clinics zao binafsi wanawagomea? Je, ni kweli kwamba madaktari wote wanaoshiriki mgomo, hakuna hata mmoja ambaye aliwahi kwa njia moja au nyingine kushiriki katika kufisidi sekta ya afya, iwe kwa kuiba panadol au vifaa vya malaki au hata mamilioni? Je, na wao wanahaki ya kusema kwamba wanagoma kwa sababu ya ukosefu wa vifaa?


  Sikuishia hapo tu... nikajiuiza tena: vipi sisi wenyewe, ambao tunashangiia au kushabikia ama serikali kufukuza madaktari, au madaktari kugoma: Hakuna miongoni mwetu walioshiriki kuziibia hospitali zetu? Je, ni haki, kwa mwananchi mwenzetu, ambaye naye ameshiriki kufisidi hospitali, kunyoosha kidole, au kushabikia akisema serikali ifukuze, au madaktari wagome, wakati huyo naye ni sehemu ya tatizo?


  Bado nikajiuliza maswali zaidi: Hivi tunaposikia serikali na madaktari wameshindwa kuafikiana, tunayachukua hivyo hivyo tu, au tunauliza kwa kina ni kwa nini wameshindwa? Tunaposikia serikali au madaktari wanasema wako tayari kwa majadiliano, tunawauliza ni hatua gani wanazichukua kwa ajili ya majadiliano, wakati upande mmoja unaendelea kufukuza na mwingine unaendelea kugoma? Tunapozikosoa taarifa zao, ni kwa sababu tumeamua kuchukua upande mmoja, au tunajua madhara ya mgomo huo kwetu sisi?


  Maswali haya mengi yamenileta katika swai moja muhimu... Sisi wananchi, tusio wanasiasa, wala tusio madaktari au walau na ujamaa na daktari - tumekua tunatoa maoni yenye kuleta suluhu, au yenye kuchochea mgogoro? (bila kujali uko upande gani)


  Watanzania wenzangu, katika hili, tunahusika wote. Kwa wale wanaosema madaktari wasigome, wasiishie tu hapo, watafakari sababu za matatizo ya sekta ya afya. Na kwa wale wanaosema wagome, wajiulize swai moja tu: Je, sababu kwamba ukosefu wa huduma bora kwa miaka kadhaa umesha sababisha vifo fingi, ni kisingizio haswa cha mgomo ambao na wenyewe pia unasababisha vifo na mateso?


  Mimi na wewe tunafanya nini ili kurudishiwa huduma ya afya? Tuendelee kupiga siasa? au tutoe maoni ya suluhu?
   
 13. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,266
  Likes Received: 1,197
  Trophy Points: 280
  Jamani ambacho hamuelewi ni nn?ma dr hawaangalii maslah yao tu,huo ni upotoshaji uliofanywa na serikali.....by the way enzi za mwalimu ma dr walisoma bure,bt nowdays mbona wengi tu wanajilipia,na wengine ndo kwa mkopo
   
Loading...