Mazingira ya Uchaguzi Serikali za Mitaa miaka 53 ya Uhuru ni aibu!

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,672
2,000
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ndiye mwenye dhamana ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)alitangazia Umma kwamba Maandalizi yamekamilika na kila kitu kipo tayari. Je Maandaalizi ndo haya? Je kuna haja ya kuendelea kuwaamini Viongozi wetu kwa kila wanancho kisema?

Pinda alitanabaisha kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao ni kipimo cha uimara wa vyama vya siasa na ndio unaoweka jiwe la msingi la vyama vya siasa kujiandaa kufanya vizuri katika Uchaguzi Mkuu mwakani. Je, kwa mazingira haya kuna nia ya dhati kabisa ya kuviwekea jiwe la msingi vyama vya siasa?

msimamizi msaidizi wa kituo cha kupigia kura Kitongoji cha Mkwajuni kwenye Kijiji cha Miono wilaya ya Bagamoyo Faustina Oforo akisubiria wapiga kura wa uchaguzi wa vitongoji, vijiji na mitaa uchaguzi uliofanyika jana
 

Attachments

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Itabidi ifike mahali Wenyeviti wa mitaa pamoja na wajumbe wake wachaguliwe pamoja na wabunge na Rais ,kuondoa kero hizi na piakuufanya uchaguzi huu uwe huru na wa haki.Vinginevyo kuna siku bomu litatulipukia tu.Sababu kwa sasa uvumilivu wa watanzania umeanza kutoweka.

Serikali inatakiwa ianze kuona wakati umepita wapende wasipende itabidi watoe UHURU kamili kwa watanzani kujichagulia viongozi wawatakao.
 

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,250
Pia tunaitaji mabadiliko ya sheria ya Pingamizi na kufanya zisitumiwe vibaya kuweka mazingira ambayo hayataruhusu kuwepo kwa mgombea mmoja kupita bila kupigwa tunataka mfumo wa ushindani na siyo ushindi wa mezani hatuwezi kurudi tena kwenye mfumo wa chama kimoja ambapo ccm inajaribu kuturudisha kwa nguvu kwa kushirikiana na tume ya uchaguzi kwa kuamua pingamizi siku moja kabla ya uchaguzi this is insane.

Pendekezo:
ili kutokaribisha hali hii lazima pingamizi ziwekwe mapema na kuamuliwa ndani ya wiki moja baada ya pingamizi kuwekwa.
kuwapa nafasi chama usika kuleta mgombea mwingine kama wakipenda badala ya aliyeondolewa.
kupiga marufuku mtu kuondolewa kwa technical issues kama kuandika mwanaume badala ya kuchecki boksi hapa cha msingi ni kitu kinaitwa intent kwa maana ya je tunaelewa mgombea anaaminisha nini?.
mgombea aondolewe pale inapothibitika kukosa sifa za msingi kama kuwahi kufungwa, mauaji, suala la umri na lazima mhusika alete ushahidi kuthibitisha hayo.

huu ni uvunjifu wa demokrasia kwa kuwanyima wananchi kushiriki ktk kutumia haki yao ya kuzaliwa na kidemokrasia kwa kulazimisha kufuta uchaguzi kwa makosa ambayo hayana msingi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom