Mazingira ya kisiasa kwa awamu hii ya sita yanaashiria furaha ya Watanzania kuongezeka zaidi

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
588
1,000
Ninakumbuka kuwa huwa kuna Taasisi zinapima furaha ya wananchi kwa kila nchi. Kuna wakati yule Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar-es-Salaam aliyepita Prof. Mukandara aliwahi kuongea kwenye Kongamano la Mwl. Nyerere kuwa furaha kwa wananchi wa Tanzania imepungua kwa kiasi Fulani.

Sasa hizo Taasisi za kupima furaha ya wananchi wa nchi ikiwepo kuangalia feedback ya utafiti wa Prof. Mukandara wakilifanyia kazi jambo hili kwa Tanzania tutarajie matokeo yatakuwaje?

Hebu tujimwage
 

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,644
2,000
Ila kuna watu wanafurahi huku wakiwa na mtazamo hasi kuwa watakuwa na likizo ya kulipa kodi kikamilifu. Baadaye watagundua kuwa walikosea sana! Hapo ndipo watakapoandamwa na msongo wa mawazo na furaha yao bandia kutoweka! Kuna watu wamemsoma vibaya mama na wanatikisa kiberiti, hasa wafanyabiashara!
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,653
2,000
Furaha itakuwa imerejea kwa kuwa utawala wa sheria utakuwa umerejea nchini

Kwa kuwa katika awamu ya 5 chini ya utawala wa mwendazake, alijenga mfumo ambao wale wateule wake walikuwa na "impunity" ya kutoshtakiwa kwa kosa lolote la jinai litakalofanyika
 

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
588
1,000
Furaha itakuwa imerejea kwa kuwa utawala wa sheria utakuwa umerejea nchini

Kwa kuwa katika awamu ya 5 chini ya utawala wa mwendazake, alijenga mfumo ambao wale wateule wake walikuwa na "impunity" ya kutoshtakiwa kwa kosa lolote la jinai litakalofanyika
Kweli kabisa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom