Mazingira ya kazi kwa wanaharakati Tanzania ni magumu, HRW

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu nchini Tanzania umesema katika mwaka 2019, watetezi wa haki za binadamu nchini humo walifanya kazi za utetezi katika mazingira magumu zaidi.

Tansania Daressalam Polizeieinsatz nach Gerichtsurteil (DW/S. Khamis)

Kulingana na ripoti wa shirika la Human Rights Watch kuhusu hali ya haki za binadamu mwaka uliopita, miongoni mwa wanaharakati walifunguliwa kesi za kimkakati pamoja na vitendo 71 vya uvunjifu wa haki zao.

Katika ripoti hiyo ya saba kutolewa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC umezitaja kwa kina kesi tisa za kimkakati zilizofunguliwa mwaka 2019 kama miongoni mwa vielelezo pamoja na matendo 71 dhidi ya watetezi wa haki za binaadamu.

Vitendo vya ukiukwaji wa sheria pamoja na haki za binaadamu ikiwemo kukamatwa kinyume cha sheria, vitisho, uminywaji wa uhuru wa kujieleza pamoja na kufunguliwa kesi zisizo na msingi, yametajwa kwenye ripoti kuwasakama watetezi huku baadhi ya wahusika wa vitendo hivyo ni vyombo vya dola na watu binafsi.

Onesmo Ole Ngurumwa mratibu wa mtandao huo amesema kuwa, matendo hayo ya ukiukwaji wa haki kwa kundi hilo muhimu kwenye jamii yameonekana kuongezeka huku baadhi ya sheria zinaonekana kutoa mwanya kwa kwa watetezi kurudi nyuma katika kutekeleza majukumu yao:

Waandishi habari Tanzania wapitia unyanyasaji

Baadhi ya vyombo vya habari Tanzania vimetozwa faini au kufungwa, waandishi wamenyang'anywa vitendea kazi na kusimamishwa.

Baadhi ya vyombo vya habari Tanzania vimetozwa faini au kufungwa, waandishi wamenyang'anywa vitendea kazi na kusimamishwa.

Ripoti hiyo inaonesha jinsi waandishi wa habari hapa nchini wanavyopitia unyanyasaji mkubwa wakati wakitekeleza majukumu yao, kutozwa faini kwa vyombo vya habari bila kuzingatia taratibu, kunyang'anywa vitendea kazi na kusimamishwa au kufungiwa kwa baadhi ya vyombo vya habari. Jumla ya matukio 36 ya aina hiyo imeripotiwa, idadi ambayo imepiku miaka iliopita.

Kwa upande wake, nazo asasi za kiraia zinaonekana kuathirika pakubwa kutokana na sheria kandamizi ambazo zinatoa mamlaka makubwa kwa msajili, ambapo katika kipindi hicho Mashirika yasiyo ya Kiserikali yapatayo 158 yalifutiwa usajili kwa kile kilichotajwa kutokuzingatia masharti ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali marekebisho ya mwaka 2019:

Mtandao huo umeitaka serikali kutambua kazi za watetezi kwa kutengeneza mazingira wezeshi, kurekebisha Sheria walizozitaja si rafiki katika utendaji kazi, zikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015, Sheria ya Vyombo vya Habari 2016 na Kanuni za Maudhui Mtandaoni 2018 ili kustawisha utendaji kazi wa watetezi wa haki za binadamu nchini.

Chanzo: DW
 
Ndo maana halisi ya hii kazi km hamuwezi mtupe sisi muone kazi.

Kunyanyaswa ndiyo zetu hatuogopi na tunapenda nyie mnaweka watu waoga km hawa unategemea nini?

Susi tunapiga tunafukua mitaro impact inaonekana hatuogopi wans nyooka! Tuuu hstuoopi mnaweka tuvitoto hivo
 
Mleta mada nipe contact mi nishuke hapo muone moto.
Asjari wenyewe hao hawana elimu fikirishi
 
Leo nimemsikia mwenyekiti wa bavicha taifa ndugu john justin pambalu...kweny video clip

Kazungumzia ishu za kubambikiwa kesi kwa wakosoaji wa serikali ya JPM

Akitolea mfano ishu ya Mdude chadema....

Nikiwa na mdogo angu AKANAMBIA ivi nanukuu...

"Huyu john pambalu anao wazazi kweli...hivi hatamani kufikisha umri wa wazazi wake"

Ofcorse Kuna kujifunzaaa Sana kwenye hizi harakati.

Walio karibu na pambalu wamwambie

Natamani waziri wa Kazi,Ajira na vijana angekaa na wadau mbali mbali kutafuta suluhu ya ajira kwa vijana.

Maana graduate wamekua wengi na hawana ajira... Ni bomu na ndio watakua wakosoaji wakubwaa.
 
Back
Top Bottom