Naomba kujua mazingira ya kazi EGPAF

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,194
5,339
Hawa EGPAF wamekuwa wakitangaza kazi sana mpaka sasa najiuluza je hawa wanafund kiasi gani hicho au mazingira ya kazi siyo mazuri kiasi kwamba labda wafanyakazi wanaondoka kila wakati. Mwenye taarifa zaidi juu ya mazingira ya kazi kama mafunzo, mishahara basi atujuze .

Nawasilisha
 
Mazingira ya kazi katika International NGOs huwa ni mazuri sana na pia hawa jamaa wana-Expand office zao nadhani ndio maana wanatangaza nafasi nyingi za kazi, nadhani mdau jipange ikitokea umeitwa kwenye interview utaona benefits zao, pia nadhani kutokana na ofisi zao nyingi kuwa mikoani na watu wanapendelea kufanya kazi zaidi hapa mjini, matokeo yake wakipata za hapa mjini wanahama kutoka mikoani kuja town.
 
hawa jamaa inaonekana pesa ipo ila wanafungua ofisi mikoani kwa kasi ofisi yao ipo masaki maeneo zamani ilipokuwa karibu hotel njia ya kukatiza kwenda CCBRT.
 
Ila ni mashirika mengi huwa wanatangaza nafasi za kazi nyingi.........Je kuna haja ya kuhoji mbona MoF kila mwaka wanatangaza nafasi zaidi ya 200, je mazingira ya kazi na maslahi yanakuaje? mimi binafsi nadhani Uhondo wa ngoma ni kuingia na kuicheza.....ikitangazwa ya fani yangu lazima nitie maguu nijue kunani?
 
You are right.
Inasemekana undugu umejaa sana.
Boss wa juu amekuweka shemeji yake ambae anajaza ndugu zake mwanzo mwisho.
Anambribe HR ili awaingize ndugu yake.
Wanafanyakazi wa EGPAF wanasema hali ni tofauti sana na zamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ofcourse ni undugu na kujuana tu. Simshauri mtu kuomba kazi EGPAF labda kama anajuana na wakubwa. Mfano wanataka mtu wa branch ya singida kwenye interview wataita watu wa mikoa ya mbali ilihali mtu wanae teyar hapo hapo. Interview inakua kama gelesha kuzuga tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa EGPAF wamekuwa wakitangaza kazi sana mpaka sasa najiuluza je hawa wanafund kiasi gani hicho au mazingira ya kazi siyo mazuri kiasi kwamba labda wafanyakazi wanaondoka kila wakati. Mwenye taarifa zaidi juu ya mazingira ya kazi kama mafunzo, mishahara basi atujuze . Nwasilisha
Mkuu,
Kama huna kazi omba,
Hayo mengine utakutan nayo hukohuko na utafanya maamuzi ukiona wewe inafaa,
Ila kama kazi unayo,
Basi endelea kutafuta taarifa yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo Shirika nasikia sasa hivi ni kama Chagulaga tu, watu kuvuana vyupi kwa kwenda mbele, waliopo wapo sababu mishahara wanapata na wengine hawana pa kuenda. Kihistoria limewahi fanya kazi nzuri na kubwa huko nyuma lakini sasa hivi inawezekana lipo hatua za mwisho za uhai wake.

Hilo shirika limepoteza mwelekeo nahisi watakuwa hawana kitengo cha HR hawa jamaa maana si kwa kuyumba huku au kwa watu kuajiriwa kiolela kwa rushwa za pesa na ngono.

Wangepigwa ban tu kama wenzao SAUT sijui kwanini bado lipo wakati hata ripoti na kazi zao nyingi ni za magumashi.
Ukiliangalia hili shirika ndiyo utagundua wafadhili na serikali hawapo seriaz bali wamelala
You are right.
Inasemekana undugu umejaa sana.
Boss wa juu amekuweka shemeji yake ambae anajaza ndugu zake mwanzo mwisho.
Anambribe HR ili awaingize ndugu yake.
Wanafanyakazi wa EGPAF wanasema hali ni tofauti sana na zamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You are right.
Inasemekana undugu umejaa sana.
Boss wa juu amekuweka shemeji yake ambae anajaza ndugu zake mwanzo mwisho.
Anambribe HR ili awaingize ndugu yake.
Wanafanyakazi wa EGPAF wanasema hali ni tofauti sana na zamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitafutie shirika ambalo halina hayo mambo. Maana hayo mambo ndiyo misingi ya Uafrika na Utanzania wenyewe.
Anzia serikalini, vyama siasa, na kila mahali
 
Mimi ninao ushahidi. Nikileta hapa hatua gani zitachukuliwa au nitaonekanaa mmbea tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina uhakika kama ungekuwa na ushahidi ungeshaupeleka sehemu husika au ungeuweka hapa.

JF siyo sehemu ya kubeza kuweka ushahidi wako, humu hadi rais wa nchi, mawaziri, wakuu wa usalama na wasaidizi wake wengine wote wanaingia humu na mambo mengi ambayo yaliwekwa JF yalifuatiliwa na kufanyiwa kazi.

Sema watu wa aina yenu ndiyo ambao mmeiua JF, kwa kuogea na kuibua vitu bila ya ushahidi. Ukiweka ushahidi wenye kueleweka hata mods wataupandisha huu uzi na kuuweka sticky ili uwe visible kwa kika mtu.
 
Umeniudhi hapo ulipogusia hilo la kunyanduana, Ulitaka watu wasipo nyanduana maofisini wakanyanduane wapi? Kama siyo kunyanduliwa huko maofisini asilimia kubwa ya ndoa zingesha vunjika.
Aisee jamaa, hili shirika hivi sasa sio kabisa nasikia limepokonywa funds na mkoa wa Tabora.
 
Aisee jamaa, hili shirika hivi sasa sio kabisa nasikia limepokonywa funds na mkoa wa Tabora.
Hayo sisi hayatuhusu, kupokonywa haina maana kuyapa nguvu uliyoyasema mpaka hapo utakapothibitisha vinginevyo.
Inawezekana ni kweli wamepokonywa, lakini ikawa wamepokonywa kwa mujibu wa Makubaliano au masharti waliyopewa na wafadhili wao.

Hatukatai swala la whistle blowing, lakini Kuna mambo ya kimsingi mngeweza kuyaambatanisha ili whistle blowing isiwe na nyepesi hivyo yenye muonekano wa kimbea.

Kuna watu wangapi out there wanaumizwa na tabia hizo huko maofusini lakini ninyi mnaopata nafasi za kuweza kupaza sauti mnayaongea na kupaza sauti zenu kiwepesi wepesi na kusababisha tuhuma zote zionekani ni za kipuuzi na matokeo yake watu wanaendelea kuumia.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom