Mazingira ya JK yalivyoathiri Utendaji Kazi wake wa Urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazingira ya JK yalivyoathiri Utendaji Kazi wake wa Urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bams, Dec 31, 2010.

 1. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,606
  Likes Received: 2,990
  Trophy Points: 280
  Wataalam wa Saikoljia watanisaidia pia, lakini ni ukweli kuwa miaka ya mwanzo ya malezi yako, 3 mpaka 15, humtengeneza binadamu, na ndiyo ina uwezekano mkubwa wa kuelezea binadamu atakuwa wa namna gani atakapokuwa mtu mzima. Mtoto huangalia mazingira yake, watu wanaongeaje, wanafanya nini, wanaishi vipi, n.k. Mtoto anayesikia kila siku watu wakitukanana, akiona watu asubuhi wakinywa pombe na kucheza ngoma, akiona watu wanaombaomba, au akiona wazazi wake saa 12 asubuhi wanakwenda mashambani, n.k, uwezekano mkubwa ndivyo mtoto huyo atakavyokuwa siku atakapokuwa mtu mzima, hata kama si kwa 100%.

  Wengine wanaweza kufikiria kuwa nazungumzia kishabiki lakini siyo nia yangu. Waangalieni marais wetu, kuanzia Mwl. Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Mkapa na Jakaya Kikwete. Pamoja na kwamba walisoma, wameishi maeneo mbalimbali, wamesafiri nchi mbalimbali lakini kuna nafasi fulani utaona mazingira waliyokulia yakionekana katika maisha na utendaji wao wa kazi.

  Mwalimu alitoka Musoma, watu wengi wa Musoma huwa ni straight forward - kisu huitwa kisu, na panga huitwa panga. Mwalimu hakuwa na shida ya kueleza au kutamka anachotaka, iwe ni kizuri au kibaya. Sikiliza hotuba zake, ni zile zenye kuweka wazi msimamo wake bila kuzunguka au kuwa katika nafasi isiyoeleweka. Sikumbuki kusikia akitoa mfano wa chakula, ngoma, n.k. Kwa makabila mengi ya bara, chakula siyo jambo linalopewa umuhimu sana, wao alimradi tumbo limejaa, kumuwezesha kufanya kazi.

  Akaja Mzee wetu Mwinyi, huyu ni mswahili wa Unguja. Ukisikiliza hotuba zake mara nyingi usingekosa kumsikia mifano yake ya ubwabwa, pilau, biriani, visu vya kukatia mboga, nyanya, n.k. Kwa watu wa Pwani chakula kina heshima kubwa sana, mtu mzima kabisa anaweza kupewa rushwa ya pilau, na rushwa hiyo ikafanya kazi. Mwinyi hotuba zake nyingi alikuwa akitumia mifano ya chakula hata kwenye masuala makubwa kabisa ya kitaifa. Maneno yalikuwa mengi sana lakini matendo yalikuwa kidogo, na watu wengi kipindi chake walifanya kama walivyotaka - ruksa kwa kila kitu. Wapo waliomsema sana na kumdhihaki kwa maneno ya kejeli za kila namna, haikumpa shida sana hiyo. Watu wa Pwani ni watu wenye maneno mengi sana, na kwao maneno yanayotamkwa huwa hayana uzito wowote, awe anatukanwa au kufanyiwa kejeli kwao huwa ni sehemu ya maisha. Ndiyo maana kipindi cha Mwinyi watu waliona kuwa demokrasia ya kusema ilikuwa imeongezeka sana, wasingeweza kuthubutu kutamka maneno hayo hayo akiwepo Mwalimu Nyerere. Kwa watu wa bara kila neno hupimwa na kutafsiriwa, na hata katika maisha ya kawaida watu wanaweza wasielewane maisha yao yote kutokana na maneno fulani ya kejeli yaliyozungumzwa na mmoja dhidi ya mwenzie.

  Akaja Benjamin Mkapa, huyu japo sina uhakika na mazingira ya familia yake lakini ninachojua ni kuwa alisoma na kukulia mazingira ya Wamisionari wa Ndanda, ambao pia maisha yao hayana tofauti na watu wa bara, hawataki mtu awe ombaomba, wanasisitiza sana kuzingatia muda na kufanya kazi kwa bidii, na hupenda zaidi matendo kuliko maneno (ndiyo falsafa ya Biblia). Mkapa kila mara alisema anachukia sana kuomba. Mkapa alipokuwa Rais, ukimlinganisha na mtangulizi wake, alikuwa ni mtu ambaye alitaka kifanyike kitu anachotaka yeye kufanyika, haijalishi kama ni kizuri au kibaya alimradi kama yeye anaamini kuwa ni kizuri. Hotuba na matendo yake vilionesha wazi kuwa hakujali kama watu watampenda au kumchukia, bali yeye alijali anachotaka yeye kifanyike. Nakumbuka kuna wakati alitamka kuwa, 'Serikali itafanya kazi na wanaouchukia umaskini, wanaopenda umaskini itawaacha waendelee nao', hii ni kauli ya mtu asiyebembeleza.

  Hatimaye amekuja JK, Mkwere aliyekulia mazingira ya Pwani yenye tabia za uswahili. Makabila mengi ya Pwana, watu wake ni wenye maneno mengi sana, na aghalabu maneno hayo, mengi huwa ni utani na uwongo, na huwa hakuna uzito wowote katika yale yanayotamkwa. Watu wa Pwani unaweza kumtukana hata matuzi ya nguoni lakini wala isimsumbue sana, mwishowe kama una chochote, ukampa, yote huyasahau kabisa, na wewe huwa ni rafiki yake mkubwa. Hata humu kwenye JF, hata bila ya kuambiwa, unaweza ukajua yupi ni mtu wa Pwani na yupi ni mtu bara. Wanaendeshwa na msemo wa, 'Mkono mtupu haulambwi'. Tabia hiyo ni tofauti sana na makabila ya bara ambapo ukimkejeli mtu hata kama ni maskini, unaweza hata kumpa msaada akaukataa - akaona aheri aishi kwa shida kuliko kudharaulika. Hiyo ndiyo maana ya maskini jeuri.

  Watu wa Pwani hupenda sana starehe hata kama hana kipato. Wanathamini sana sherehe, ngoma, kazi za kuongea kuliko zile za kutumia misuli. Huamini kuwa wao ni maskini, na hivyo wao wanastahili kusaidiwa, hawawezi kubadili hali hiyo. Ukimtazama Rais wetu, anapenda sana kuomba (aliwahi pia kutamka kuwa sisi ni maskini na huko nje kuna pesa nyingi, tunachotakiwa ni kueleza ili watuelewe; huwa anaenda nje kuhemea, n.k), anapenda sana kuongea (matendo hakuna), hasumbuliwi na maneno wala kejeli wanazozitoa wananchi wengi dhidi yake, anapenda sana michezo (yeye mwenyewe alisema anapenda sana mpira na dansi), na kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa bunge safari hii ameelezea kuwa ameridhishwa sana na maendele ya sanaa (muziki, tamthilia, na akawataja wanamuziki wa taarabu kama mfano wa mafanikio).

  Ninachojiuliza, utendaji usioridhisha wa Rais wetu ni upungufu wake binafsi au matokeo ya mazingira aliyokulia? Na ikiwa ndiyo hivyo, kuna umuhimu wowote wa kuangalia mazingira ya mtu aliyokulia kabla ya kumchagua kuwa kiongozi mkuu wa nchi? Na je, ikifanyika hivyo itakuwa ni ubaguzi wa kikabila au kimaeneo? Kama tunataka viongozi wazuri na watakaofanya mambo ya kusaidia nchi yetu, tunafanya nini katika kuwaandalia mazingira watoto wetu yasiyo hasi kwa maendeleo ili waje kuwa viongozi wazuri na raia wenye mchango mkubwa kwa Taifa letu?

   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Hilo nalo neno
   
 3. z

  zainzion New Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana unayosema yakawa na ukweli ndani yake. hatahivyo yanahitaji uchunguzi wa kina kutoka kwa wanasaikolojia. kumbuka binadamu wote huzaliwa sawa ila malezi na makuzi ndiyo hutufanya tuwe hivi tunavyooonekana. soma historia ya Hitler, utajua kwa nini alikuwa katili.
   
 4. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maneno yako yana ukweli ndani. Mkurya na mtu wa pwani wanatofauti inapokuja swali la kuangalia mambo. sababu kubwa ni mazingira wataalam wa sociology wanaita "social construction". Msichana aliyelelewa akiambiwa awe na adabu ndipo atapata mume atakuwa tofauti na yule aliyefundishwa kujitegemea na kutowaamini wanaume kabisa. Msichana aliyezaliwa kwenye familia ya wazazi wanaopendana atatamani kupata mme lakini yule ambaye kila siku anashuhudia kipigo kwa mama yake atawaona wanaume kama terrorists. Kwa ufupi mazingira yana athari kubwa katika maisha ya mwanadamu. Alikadhalika mtu aliyelelewa katika mazingira ya "saidia baba" atamua kuomba ili mradi watu wake wasile mihogo! Wakati wa kampaini kituko ilikuwa ni kusema kile ambacho marekani imeahidi. Ukitaka soma kitabu kinaitwa SOCIAL CONSTRUCTION A READER by Gergen and Gergen (ni google book)
   
 5. M

  Msenshe Member

  #5
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata aliyeiweka thread hii hajasema tumezaliwa tofauti anajaribu kuonyesha malezi yanavyoathiri. Tanzania ya sasa inamuhitaji Rais anayeweza kuchangia kwa ufasaha na kuonyesha upande anaoupa sapoti ktk kila hoja nzito ya kitaifa mfano,katiba. Sio JK kila ishu anakaa kimya mpaka taifa linaparanganyika. Nahisi hawezi kusimamia hoja anazoamini.
   
 6. m

  mbezibeach Senior Member

  #6
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaah ni kweli kabisa mkuu.....mazingira na makuzi kwa kiasi kikubwa sana kinachangia Tabia na hulka za binadamu ingawa wakati mwingine hulka hizo na Tabia zinaweza pia kuathirika na vitu vichache kama New Exposure...sasa kinachotian wazimu ni jinsi gani binadamu wengine wanavyoweza ku-change na wengine wanavyobaki static...Tkirejea ktk viongozi wetu je Pinda anazo tabia za bara au Andrew Chenge anaathirika na tabia za pwani au bara?
   
 7. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Bams,

  Sina cha kuongezea kwa kile ulichoeleza kwa sababu kila kitu kiko wazi.

  Uchumi wetu kwa jinsi unavyocheza kila anapoingia kiongozi mpya unanikumbusha Graph maarufu AC (Sinusoidal)

  Kifupi naona kuna umakini mkubwa na maendeleo huwa yanaonekana pindi mtu wa bara anashika madaraka, lakini kwa kweli si kwa ubaya ila pwani kazi kiswahiba zaidi, uchumi wetu huwa unadorora.

  Nimeshuhudia maeneo mengi hata ya pwani yaliyo na Rutuba wenyeji wakinunuliwa na baadaye kwenda kuomba vibarua kwa wageni. Wamelelewa mazingira ya kivivu. Angalia japo Jembe wanalotumia kulimia litakupa jibu kama lengo ni kulima au kupoteza muda.

  Ukifika kanda Kaskazini,Kanda ya Kusini, kanda ya Ziwa na Magharibu shughuri nyingi zinafanywa na wenyeji wa kule ikiwa ni ktk viwanda,mashamba, biashara nk. Lakini kinachonipa kuamini maneno yako, Tazama hata hapa Dar Es Salaam watu wa pwani wangapi wako ktk mashirika ya umma,Viwanda na hata kule shambani Kimbiji. Utakuta kazi nyingi wameshika wageni nao kufanywa vibarua tena wa kazi laini zaidi.

  Huu ndiyo Ukweli wenyewe. Tunapochagua kiongozi tuangalie amekulia mazingira gani:ranger:
   
 8. c

  chach JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 434
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  :whoo:Raisi wetu ni sawa na mzazi ambaye hata mtoto akimpiga mama yake yeye kimya tu.Watu wanaongea Dowans,Katiba,nk utafikiri hayupo au au hasikii.Haya watendaji wake kila mtu anaibuka na lake .No common vision,no common goals on matters.Kiongozi ni muonyesha njia sijui hakai na watendaji wake ili wawe na common vision on serious national issues.KATIBA NI LAZIMA
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  NI kweli kabisa mazingira yanajenga tabia ya mwanadamu,kwa mfano katika nyumba ukiwaaminisha watoto kwamba hakuna mahala patafungwa kwa kuzuia wizi basi watoto watakuwa katika uaminifu na kutokuwa wadokozi kwa sababu kila mahala ndani ya nyumba wataweza kupafika na kuheshimu,wale waliolelewa katika misimamo na kujiamini mara zote wameweza kujitegemea na kuamini katika ndoto zao na kufanya mambo makubwa sana katika maisha yao ya kijamii na kimaendeleo na ni mara chache wanaweza wakadhoofu kwa mitikisiko ya kimaisha,hata pale inapotokea kwamba mambo yanawaeendea kombo huwa wanajikung"uta na kuanza upya wakiwa imara kisaikolojia,mazingira aliyokulia mtu yanaweza yakaonyesha hali halisi ya mwanadamu japo sio mara zote yanakuwa sawa ukubwani wachache hubadilirika
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nimeambiwa mwaka ujao 2011 hapa JF kuna watu wamenunua visu, mapanga na bunduki kutudhuru wengine, damu za watu zitamwangika. Awali nilikuwa siamini kwamba watu wanaweza kutumia silaha hizi kwenye kompyuta (jamvini/blog) kumbe maneno makali yenye kuleta majeraha moyoni hayana tofauti na matumizi ya silaha halisi. Miaka inasonga mbele matumizi ya silaha za kuchoma mioyo zinaongezeka.

  Neno moja kali linapokimbilia kuleta madhara moyoni ni sawa sawa na risasi inapoingia mwilini. Risasi inaweza kukuua hapohapo kutegemeana na mahali itakapotua mwilini na maneno makali yanaweza kumuua binadamu hapohapo kutegemeana na shinikizo la juu au mshituko wa moyo utakavyo himili maneno hayo.

  Wewe unawachokoza Malaria sugu, Dar es salaam na Yaya. kutoka huko waliko wataripuka sasa hivi na kuwasha moto hapa. mods tafadhali kaa macho ili uweze kuthibiti vita vya maneno.
   
 11. v

  vassil Senior Member

  #11
  Dec 31, 2010
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  analysis nzuri.Watu walio karibu na Mkapa au wanaomjua wanasema kwamba huyu bwana anaamini sana Wazungu kwa sababu ya kukua karibu na wazungu utotoni mwake wamemuathiri ana tabia ya kufikiria watu weusi ni wapuuzi hawana uwezo.Mfano wa kwanza alipoingia madarakani alileta wazungu wa South Africa kuja kufanya kazi ya collection ya madeni ya Tanesco,ni kweli walifanya kazi nzuri lakini ukiangalia kwa karibu ni kujidhalilisha kukusanya madeni hauhitaji kutafuta watu wa nje.Mfano mwingine ni ubinafsishaji wa Mabenki,alidiriki hata kuignore amri ya bunge kupinga kuuzwa NBC ili alete wazungu wake.
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa maana hiyo wachagga hawafai kuwa Rais kwani ni watu ambao wana hulka ya kutafuta pesa hata kwa njia ya wizi ili mradi awe tajiri
   
 13. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nakuunga mkono kwa hoja zako na kwa kiasi kikubwa katika maisha ya kila mtu mazingira aliyokulia yana sehemu. Rais tulie nae sasa ni mtu wa Pwani na kwa watu hawa usitarajie lolote la maana hasa katika suala la maendeleo. Ni watu wanaoendekeza starehe na maneno mengi bila matendo. Mfano unaweza ukajiuliza hivi ni kwa nini karibu kila siku Jk anaenda kwao bagamoyo na misafara ya magari ya wapambe wake? Cha ajabu ni kwamba hakuna la maana zaidi ya kuwajulisha wanakijiji wa kwao kwamba yeye ni mtu mkubwa na hakuna wachofaidi zaidi kutoka kwake. Yeye huwaringishia mafakiri na pia huwa duni sana kwa wale anaofikiri ni zaidi yake kama wazungu na yupo tayari kulamba miguu yao. Ndio maana tumemsikia akisifu kuomba omba kwake anakofanya kwa wazungu zaidi ya zaidi ya jitihada zinazoweza kufanywa na sisi wenyewe kujikwamua kimaendeleo. Tabia yake yakukwepa kuyashughulikia masuala mazito nayo ni kikwazo kikubwa, hili nalo husababishwa na tabia yake ya kutokuwa na falsafa ya dira ya taifa na badala yake anaendekeza unafiki wa kumfurahisha kila mtu yaani waovu na wenye haki kwake yeye ni mamoja.
  Mi nasisitiza kumchagua kiongozi ni lazima historia ya mazingira aliyokulia ichunguzwe kwanza nakufanywa kigezo mojawapo ya sifa za kupewa uongozi.
  .

  .
   
 14. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #14
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa mawazo yako inaonekana anaeweza kuiongoza Tanzania ni lazima atoke bara tu. Umekataa kabisa sifa zote za uongozi bora na umechukua sifa moja tu kua lazima mtu awe mbara. Kwa mfano umemtaja Mwalimu nyerere kua kisu kwa kua ametoka bara lakin kama mtu atakuambie utaje kwanini akijiunzulu sijui utaelezea vipi.

  Umetaja watu wapwani kua wanapenda utani yet, umeshindwa kueleza kua hilo linauhusiano gani na uongozi. Hiyo ni culture ya mtu ambayo ni muhimu kwake kama ingefanywa na rais wa America ungeiona ina maana sana. Kuna maana gani mtu kutembea na mbwa mpaka kupanda nae ndege, lakin kwa kua ni culture yake basi watu wanaeheshimu.

  Unasema kua Mwinyi aktoa mifano ni lazima ataje pilau. Kwa kukufahamisha mara nyingi inatolewa kwa wale walengwa ili wafahamu, ndio maana ukizungumza na mzungu kitu muhimu atakuuliza do you drink au akikuelekeza kitu lazima atataja pub. Sasa kuna maana gani mtu kua mlevi?.

  Umekubali kua wakati wa Mwinyi demokrasia ya maneno iliongezeka lakini wakati wa Mwalimu huwezi kusema sana, sijui kama unajua kua kwa kusema hivyo unamfanya Mwalimu aonekane kua alikua Dikteta. Unasema Mkapa alikua anapenda anachotaka yeye lazima kifanyike, kama ni kweli unajua huo nao ni udikteta mwingine. Jaribu kufikiria unachosema kwani unaweza ukachekesha hasa ktk karne hii ya 21. Jaribu kufuatilia ombaomba wengi wanatoka mkoa gani Tanzania.
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Watu kama hawa tulishaacha kuwajibu? wenyewe wana elements za ubaguzi

  Vipimo (measurement of good leader) kwao ni mabavu, kuonea, kugombeza, etc

  Personally ninatoka bara, lakini ukweli ni kwamba wabara ni walafi na wabinafsi sana!

  Imagine kama Dar es Salaam ingekuwa ni nchi ya wachagga, wamasai etc..

  Watu wasinge nunua ardhi (ulafi na umimi) wala bahari ingekuwa shamba la ukoo

  I admire watu wa pwani hawana tamaa za kijinga wamerizika na wanajua huwezi kumaliza dunia kabla haijakumaliza kiaina..

  Tujifunze uungwana wa watu pwani na si kuwadharau na kuwakejeli...ni malezi ya kurizika
   
 16. K

  KALAMAZOO JF-Expert Member

  #16
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora tu ungekuwa muwazi zaidi ukasema kuwa kuzaliwa kwake na kulelewa katika uislam ndilo tataizo badala ya kuzunguka.
  Wanaosema nchi imemshinda wao hasa walitaka nchi iweje? Labda watoe mfano wa nchi yoyote ya kiafrika ambayo ina kiongozi shupavu amabe ameivusha nchi yake kutoka ktk dimbwi la umaskini? Hakuna.Nchi zote za jirani zina matatizo
   
 17. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #17
  Dec 31, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mkuu, kwanza nikupongeze kwa uchambuzi unaoleta hamu ya kuendelea kusoma. Kwa ujumla, nakubaliana na wewe kuhusu tofauti ya tabia ambayo msingi wake ni malezi yanayochangiwa kwa kiasi kikubwa na jamii inayozunguka. Lakini siyo rahisi kwa nchi kubwa namna hii kuwa na viongozi wenye tabia zinazofanana siyo rahisi na kwa kweli hii ndiyo raha yake. Mimi binafsi ni mtu wa bara. Nilipomsikia jk anamtaja msanii wa taarabu Mzee nilipigwa na butwaa lakini kwa watu wa pwani jk aliwakuna sana.

  Sasa kwangu mimi pamoja na tofauti hizo za tabia ambazo hatuwezi kuzikwepa, ni muhimu viongozi wetu watuongoze kwa kutumia katiba, sheria na maadili. Kila kiongozi akijitahidi kuzingatia hayo, basi tofauti za kitabia zitamezwa kirahisi.
   
 18. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #18
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,632
  Trophy Points: 280
  nimekuelewa sana mkuu kweli unajua kasoro na mipango mzima ya watu, umeonea sahihi mana sio Mkabila wala ndini , ukuficha ukweli umechambua sawa sawa, lakini kwa hulka ya Mchagga kama angepewa nchi hii angetumaliza kabisa, chukulia Mramba na Barabara za Rombo, na ahadi zake za kula nyasi, chukulia Mzee Ruasa aliyecopy mambo ya kabila hii, si unaona kuwa na karibu na mbuzi mwizi nilazima nawe uibe, kwa mana hiyo EL kwa kukaa na kukaribiana nao ndio anakuwa na tendecy za wizi kama wao,
   
 19. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #19
  Dec 31, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Aloleta thread hii nae angetuambia ni mtu wa wapi ili tutathmini uelewa wake kwani analidanganya Taifa Hadharani eti JK anaendeleza ombaomba WB statistics shows Budget yetu ina depend Donors by 28 % while Mkapa aliacha 48% je kitu gan kinamfanya asitambue kupungua kwa Uombaomba ni Chuki au tatizo la Eneo alilotoka? anajaribu kumhusisha Mkapa na Malezi ya Ndanda, atueleze Contribution ya malezi hayo kwenye Wizi wa Rasilimali za Taifa kama Nyumba za Serikali, Migodi ya kiwira, kuanzisha biashara Ikulu,Meremeta, Epa, n.k ,By now anapaswa kutambua kuwa JK AMEINGIA KWENYE hISTORIA YA KUWABURUZA vigogo wengi zaidi Mahakamani, mawaziri 2, makatibu na watumishi wengine wakubwa na mabalozi anaebisha atoe data za kupinga hili, akina Mahalu, mgonja, mramba,liyumba, patel tumewashuhudia cortin, kama Nyerere alifia Record hii mtu ajitokeze alete ushahidi,Demokrasia imeshehena zaidi kuliko kipindi chochote anaebisha aje na ushahidi, kabla ya kumuona mzee Mwinyi kuwa ni mzembe atu alete ushahidi wa hali ya uchumi 1985 wakati anaingia tufanye tathmini na wakati anaondoka tuone kama alivurunda au ni kitchen words,
  Mmesahau kuwa Ubishi wa Nyrere wa kupinga :Mawzo ya Hayati Kambona kwenye Azimio la Arusha, Edwin Mtei kwenye sera za kiuchumi, Mzee Christopher Kasanga Tumbo kwenye Operation vijiji ndo matokeo ya haya tunayoyaona,

  Tafadhali usifiche ajenda yako ya siri kwenye kichaka cha umaeneo, tushafyeka kichaka hicho weka ajenda yako hadharani bila woga,
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sawa kabisa mkuu,

  Nyerere aliondoka watu hatuwezi kununua hata nguo achana na TV? kuna watu wanaweza/thubutu kumuita st. aibu hawana?

  Nimeenda wizara ya ujenzi ntaleta data za barabara mpya zilizojengwa wakati wa JK mikoani I was surprised?

  Mkuu JK amepeleka pesa wilayani nyingi kupita rais yeyote yule Tanzania of course wilaya zenye walafi na usimamizi mbovu zimelewa

  Lakini ile guts za kutoa pesa serikali kupeleka kwa wananchi ..is a measurable leadership skill

  Ameruhusu CAG ku expose goverment audits...hallo Mkapa hajawahi kujaribu...hii inaitwaje -good governance

  Pamoja na kucheka lakini ni kiongozi mzuri mtu..ila yuko a bit slow..
   
Loading...