Mazingira ya Chuo Kikuu Iringa yapoje?

Me nasoma apo mkuu nimejitolea kuwa mwenyeji wako....mazingira ni mazuri sana na ni rafiki kwa kila mwanafunzi
 
Ukithubutu kula nyama, umekula mbwa.. mzee.

Kuna mwaka nililishwa mbwa, nyama ilikauka vizuri.. mwisho wa picha kumbe mbwa.
 
Vyumba vizurii kuanzia elfu70-100,000 self kikubwa kuanzia semtema kushuka chuoni,ambavyo sio self ni elfu 50,mitaa ile ile ya chuoni mpaka juu juu semtema,na kule bwawani..kama unajiweza kwa nauli unaweza kusogea mpaka ngome,changalawe,kihesa,kwa beda,mwang'ingo...

Vimbweta vipo vya kutosha

Kitabu inategemea na course unayosoma ila upande wa law wapo vizuri..

Itunze boom yako nunua kiwanja kigonzile,zungushia uzio/miti ama ukuta.utakuja kunishukuru badae

ONYO: Mwezi wa 11 ikishanyesha tu mvua unaanza msimu ulanzi mpaka mweziwa 4 kaa nao mbali huu ndio unafanya wanafunzi wanafeli wanaanza kusingizia walimu..ulanzi litre 1=500 wa baridi kama umetoka kwenye fridge unashuka kooni kama bia laini..ukikaa kwenye kijumba hukumbuki kipindi kinacho endelea darasani mama muuza anaweza kuwapikia ugali hukohuko...iringa kumenoga na uhakika wa kupata DISCO upo ukiendekeza ulanzi
Hahaha dah ulanzi
 
Aiseee 2 years ago...maskani yangu yalikuwa hapo Semtema karibu na kituo cha polisi. Uwepo wa hivyo vyuo hapo town umefanya maisha yawe ghali sana.

Yaani ukienda gengeni kama ww si mwenyeji utauziwa vitu bei ndefu ila mwenyeji bei chee..

Mazingira ya iringa ni mazuri sana na kuna fursa kibao.
 
Back
Top Bottom