Mazingira magumu ya kuanzisha Biashara Tanzania, nani ananufaika nayo?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,704
6,499
Ni kama kuna Watu wana nufaika na huu ugumu.

Mazingira au urahisi wa kufanya Biashara Tanzania bado changamoto ni nyingi sana, na nashindwa kuelewa je bado tunahitaj kwa hisani ya Watu wa Marekani ndo watusaidie?

Fikiria u aenda TRA unaambiwa anaye saini Docoments hayupo njoo wiki ijayo, ukienda Halishauri kwa ajili ya Leseni mambo ni yale yale utaamvia mara afisa wa Biashara yuko kwenye Ziara, mara ametoka mara ana udhuru njoo baada ya siku kadhaa utamkukuta.

Watendaji wanatembea na Offisi na kama hayupo hakuna kinacho fanyika sasa mbaya ukute anaumwa.

Hizi ni kero sana na usumbufu mkubwa hapo bado hujaongelea watendaji kukwepa kusaini Document na kutengeneza ubize ili tu uwatoe pesa.

Haya mambo yanapigiwa kelele miaka nenda rudi na hakuna anaye jali na nazani Serikali inanufaika na haya mazingira magumu ya kufanya Biashara Tanzania.
 
Sijui nan aliwaloga waTZ, yaani tunasafari kubwa sana ya kutafuta maendeleo.

Imagine uko chuo kikuu, umefanikiwa kumaliza step zoote za kupata PhD anatokea mtu anakwmbia dissertation yako ikiwekwa ruler inaonekana font hazijakaa sawa na so utagraduate mwakani.

Hivi ukiwa na bunduki si unamaliza ofisi nzima. yaani after 5yrs ya kuisotea PhD halafu mjinga anakwambia utagraduate mwakani. WTF.

sasa hapa ni kwenye elimu tena ya PhD, vp mtaani.
 
Unalipa kodi kabla ya kujua unaingiza kiasi gani kwa mwezi/mwaka, kodi ya maduka/makaazi/usafiri kila kitu kodi ipo juu. Kuwekeza Tanzania na kufanikiwa inataka njia ya ufisadi/unyonyaji kwa sana.


Lunatic
 
Wasomi tunachelewa kwenye biashara kwa kutaka kufuata taratibu zote za kisheria. Hapo angekuwa darasa la saba, angesheaanza biashara mapemaaa. Hao TRA, sijui halmashauri wanafuata wenyewe anawapoza maisha yanaendelea. Ushauri wangu ni huo huo. Wewe piga chapa kazi, kazi yako ikionekana watakutafuta wenyewe kukudai kodi.
 
Wasomi tunachelewa kwenye biashara kwa kutaka kufuata taratibu zote za kisheria. Hapo angekuwa darasa la saba, angesheaanza biashara mapemaaa. Hao TRA, sijui halmashauri wanafuata wenyewe anawapoza maisha yanaendelea. Ushauri wangu ni huo huo. Wewe piga chapa kazi, kazi yako ikionekana watakutafuta wenyewe kukudai kodi.
Mkuu kwa baadhi ya Biashara unatakiwa kufuata tu utaratibu, sio biashara zote no kufanya tu kimagumashi,
 
"....nani ananufaika nayo"m hili ni swali zuri sana la kuanzia kufikiri.
Taasisi nyingi zimeshikiliwa na wakuu wanaoteuliwa na wanasiasa kwa hiyo ni wazi wanasiasa wanateua watu wanaofanana nao.
Kwa vile upeo wa wanasiasa wengi hawawazi zaidi ya familia na koo zao na hawa wakuu ni hayo hayo, wanajiangalia na kudhani kuwa 'engine watajijua" huku wakisahau ustawi mpana wa jamii hii fura ya wote
 
Back
Top Bottom