Mazingatio juu ya uandishi wa CV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazingatio juu ya uandishi wa CV

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Kilongwe, Oct 5, 2010.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  MazingatiojuuyauandishiwaCV

  [​IMG]

  Moja ya kati ya vitu vigumu pindi uandikapo Cv ama Resume ni jinsi ya kuchunga idadi ya kurasa.Nakumbuka nilipoandaa CV yangu ya kwanza ilikuwa na kurasa kama nne,nikampelekea mmoja wa watu wangu wa karibu kuichambua na kutolea maoni,akanirudishia ikiwa na kurasa moja na nusu.Binafsi kipindi kile moyoni sikuridhika kwa sana ila kwakuwa mtu aliyenirekebishia ni mtaalamu kwenye masuala hayo hivyo sikuwa na budi kukubaliana na marekebisho kwa moyo upande.
  Niliwahi kufanya mahojianao na baadhi ya waajiri ambao wanatoka nchi mbalimbali tena nyanja mbalimbali,wengi wao walisema ni nadra sana kwake kuangalia kurasa zaidi ya pili ya CV,waajiri hupendela na kutamani CV fupi,najua kuna baadhi yetu wanaweza kuwa na mtazamo tofauti juu ya hili,hivyo leo nitatoa muono wangu halafu mlango umefunguliwa kwa wenye maoni wachangie.

  Je unaijua CV?:
  Kiufupi ni kuwa CV haitakiwi iwe na kurasa nyingi,hii ni kwa sababu hii ni CV na sio utambulisho binafsi (autobiography).Wengi wamesahau kuwa hautapata kazi kupitia CV yako bali utapata nasafi ya kufanyiwa usaili(interview) kutegemeana na CV yako, matokeo yake ni kupata ajira kulingana na nini ulichokifafanua kwenye usaili.Kumbuka kwenye usaili ndio uwanja wako wa kujidai ambapo utwaweza kufafanua kwa mapana na marefu huku ukijidai kwenye fani yako.


  Uzoefu wa kazi:
  Kuna wengi wanaamini kuwa jinsi anavyoorodhesha uzoefu wake ndivyo anavyowavutia waajiri,hili halina ukweli isipokuwa kama huo uzoefu wako una uhusiano na kazi iliyopo mkononi.Ndio maana watu husema andika CV inayoendana na kazi husika.Maharage yanaweza kuwa ni mboga kwa mtanzania ila sio kwa mchina.Hapa nina maana uzoefu wako kama daktari hauna msaada kwenye kazi ya kunyanyua mizigo bandarini.Wengi wetu tumekuwa tukichanganya juu ya nini ni muhimu kwako na nini ni muhimu kwa waajiri na ni jinsi gani utaunganisha mawazo uako na ya muajiri.


  Majukumu:
  Cha msingi kukumbuka pindi uandikapo CV yako ni kuweka bayana nini umefanya(accomplishments) na sio kazi zako(duties).Vilevile weka akilini kuwa lazima uhakikishe unazifikisha kwa undani wake.Kwani waajiri hupenda sana kuuliza nini utafanya na sio nini umesoma au unacho kwenye cv.Kwa mfano labda wewe ni mtoa msaada(tech supporter) wa kampuni A,unatakiwa kufafanua pindi ulipokuwa kampuni A uliweza vipi kupunguza mlundikano wa matatizo,uliweza vipi kuongeza ubora wa huduma kwa wateja,je wateja walinufaika vipi na nini maoni yao siku ya mwisho? Mambo kama haya na mengine mengi yanaweza kuwa na msaada mkubwa kwako pindi uandikapo CV yako.
  Labda nikupe ujanja ambao unaweza kuwa na msaada kwako,baada ya kumaliza kuandika CV yako na kuelezea nini ulifanya kwemnye kampouni fulani,jiulize mwenyewe,"SASA"??? Hii itakusaidia kujiweka kwenye nafasi ya muajiri na kufikiria kama muajiri? Ingawa ni ngumu kupata mchanganuo wote ila utaweza kupata picha ya mchezo kamili.


  Suluhisho:
  Kitu cha msingi ambacho leo nimegawana nanyi wana AfroIT ni kuwa,jaribu kufupisha CV yako,andika CV inayojiuza na kujiongoza,usiwachoshe waajiri na kufanya waanze kukuchukia au kukushusha kiwango.Baada ya kuandika CV yako,jaribu kuomba ushauri toka kwa watu mbalimbali walio kwenye hiyo idara.

  Maoni:

  Je nini maoni yako? Ni kitu gani cha kuzingatia kwenye CV nenda hapa
   
 2. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
 3. R

  Rwey Senior Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ahsante mkuu kwa msaada zaidi
   
 4. AG.6851

  AG.6851 Member

  #4
  Aug 25, 2017
  Joined: Jul 31, 2013
  Messages: 88
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 25
  Habari wana JF

  Miongoni mwa mambo yanayotukosesha ajira baadhi yetu ni kushindwa kuandika CV. Sasa basi hebu mwenye uwezo huo wa kuiandika ikiwa na vitu vyote muhimu aweke humu tufaidike sote.

  Itakuwa faraja Sana kama utatoa msaada wako ili kuwakwamua walioshindwa au kuwaongezea ujuzi wengine

  Aidha kama unayo Unaweza pia kunitumia kwa WhatsApp Namba 0763769886.

  Ahsante Sana!!!

  Nakupenda Sana Mama Yangu
   
 5. silasc

  silasc JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2017
  Joined: Feb 10, 2013
  Messages: 3,391
  Likes Received: 1,859
  Trophy Points: 280
  Google mkuu.
   
 6. Eng Nyahucho

  Eng Nyahucho JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2017
  Joined: Dec 18, 2016
  Messages: 592
  Likes Received: 824
  Trophy Points: 180
  Uki Google makosa ni yale yale, bora hata ungetoa sample hapa ili kuonesha mtiririko sahihi

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 7. u

  uniquelady JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2017
  Joined: Apr 3, 2015
  Messages: 425
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
 8. GIPAMA

  GIPAMA JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2017
  Joined: May 21, 2016
  Messages: 903
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 80
  Mkuu, ukiipata nami nitumie kwa whatsApp namba 0757062351
   
 9. w

  wisdom empire JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2017
  Joined: May 5, 2017
  Messages: 348
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  ivi katika ajira portal kuna sehemu ya kuattach CV?

   
 10. AG.6851

  AG.6851 Member

  #10
  Aug 25, 2017
  Joined: Jul 31, 2013
  Messages: 88
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 25
  Ukifungua profile kuna sehemu ya kujaza hizo information

  Nakupenda Sana Mama Yangu
   
Loading...