MAZINGARA Vs MAZINGIRA, SARE Vs SURUHU na PASWA vs PASHWA!!!

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,194
1,434
Ninaisikia huu mkorogo mara nyingi sana (almost mara moja kila wiki) kupitia vyombo vote vya habari kasoro magazeti.
Mfano; Timu A imegawana pointi na timu B baada ya kutoka suruhu ya bao 2 kwa 2. Ninavyojua mimi suruhu ni goalless draw-wataalam nikosoeni

Mfano; Jamii inapashwa kufanya kazi kwa bidii ili uindokane na umaskini unaoukabili. Ninavyjua mimi, kupashwa ni 'be informed' ilhali hapa ilibidi iwe inapaswa yaani urged

Mazingara ninavyojua mimi ni kaka mauzauza au mazingaombwe fulani lakini watu wengi wanachanganya na neno mazingira (environment/circumstance)
 
sio suruhu ni suluhu, sare inamaana kufanana, suluhu maana ni kupatana. Kwa lugha za spoti ambazo mara nyingi si lugha rasmi, ni sahihi kutumia sare, suluhu, kutoshana, nguvu sawa pale ambapo mshindi hajapatika.

Kwenye mazingara vs mazingira, paswa vs pashwa; upo sahihi.
 
Kupaswa ni kutakiwa uwajibike na jukumu fulani...mfano wanafunzi wanapaswa kusoma ili wafaulu mitihani yao. Au akina baba na akina mama wanapaswa kuwatunza watoto wao.

Kupashwa: kuna maana mbili, 1. kusutwa, au kupewa vipande vyako na watu wengine hususan wa rika lako au wenzako.
2. Ni kupewa joto..mfano chakula kinapashwa moto nk,

Mazingara ni kama mazingaombwe ya kishirikina...uchawi uchawi nk
Mazingira: Mandhari inayokuzunguka.

Suluhu (siyo Suruhu) sawa au sambamba- kimpira timu zinakuwa zimetoka bila bila(0-0), kwa mabondia pale wanapopata nukta (points) sawa, au wapiganaji wanapolingana kiupiganaji.
Sare ni sawa na sambamba ila kimpira ni timu ambazo zimefungno magoli yanayolingana.

Waandishi wetu wengi wao ni vihiyo, na wanachangia sana katka upotoshaji wa kiswahili!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom