Mazingaombwe ya Magufuli: Jana Sheria Msumeno. Leo: Hekima itumike

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Kasi ya Rais Magufuli ya kufyatua vimbwanga inaendelea, Na inafika mahali mtu unajiuliza maswali ya msingi. Wakati anaendesha zoezi la Bomoa Bomoa bila fidia katika maeneo ya Kimara na kuendelea, Rais Magufuli alikuwa mkali kama pilipili, akinukuu sheria ya miaka karibu mia iliyopita. Sheria msumeno. Kabla ya hapo aliendesha bomoa bomoa katika maeneo ya mabondeni, pia akinukuu sheria. vilio vilitawala. Leo anasema amesimamisha bomoa bomoa, siyo makosa ya wananchi. busara itumike.

Hapo nyuma tumeshuhudia watu wakibomolewa nyumba zao kwa sheria ya mita 60 toka mtoni. Kilimo katika maeneo yaliyokatazwa, vyanzo vya maji, ilipelekea kuharibiwa kwa shamba la Mh. Mbowe. Leo tunaambiwa busara itumike.

Inawezekana pia kuna watu walilengwa, na sasa wameshashughulikiwa, "busara ndiyo inatumika"? maana kulilkuwa na operesheni ya kukusanya madeni ya nyumba za NHC. Tulishuhudia jengo ilipokuwepo Bilicanas, iliyomilikiwa na Mh. Mbowe, ndilo pekee lililoshughulikiwa. Mbowe akatimuliwa na baada ya hapo kimya.

Hapo nyuma, Rais Magufuli alitumia sheria zilizotungwa "na wakoloni" kuhusu upana wa barabara ya Morogoro, akabomoa maelfu ya nyumba bila huruma na bila fidia, leo anasema kwamba "hizi sheria tulirithi kutoka kwa wakoloni, zimepitwa na wakati, tuangalie rialite ya watanzania".

Inaeonekana wazi Magufuli ameshatosheka na kisasi chake kwa watu au makundi ya watu, na sasa anaangalia 2020. Amesababisha maumivu makubwa yasiyosemekana kwa watu wengi, amewatia wengi sana umasikini, wengi wamefariki, leo anasema "busara itumike".

Lakini pia kuna baadhi ya maamuzi ambayo anayatoa, mfano kuruhusu wamachinga, halafu baadaye atakauja rais mwingine katili kama yeye au hata kumzidi yeye, naye atasema "sheria msumeno", na kuwafurusha. magufuli atakuwa ametimiza mahitaji yake ya kisiasa kwa sasa lakini hatakuwa ametoa ufumbuzi wa matatizo ya watanzania.

Na hii ndiyo athari ya kuwa na Rais ambaye hatumii wala kufuata "sera" inayoeleweka. leo atasema hivi, kesho atasema vile. Ila burudani kubwa zaidi ni kwamba daima watu watampongeza. akivunja nyumba leo watampongeza kwa kuwa "imara" na mwenye msimamo katika "kuwaletea watanzania maendeleo". kesho akisema "busara itumike" watampongeza kwamba ni Rais "msikivu" na "anayejali maisha ya watanzania".
 
Labda hujaelewa busara anazosema yeye. Kama ni maumivu tumeyapata sana tumelia mbaka tumecheka kwa mateso.
 
Itakuwa amejiuliza, muache afanye atakalo, au nyie mlitaka aendelee kuboa magheto ya watu...kweli binadamu hana pema.
 
Sheria ilifuatwa kuwaumiza watu fulani fulani tu. Malengo yao yametimia wanaona hamna haja tena ya kufuata hizo sheria. Nchi inanuka uonevu na manung'uniko yamejaa kwenye vifua vya wananchi.
 
Hakuna cha chadema watu kama nyie ndio wakuwashangaa sana......waache wahanga tufarijiane sababu ujakutwa......nyumba umeanza jenga tangia 1990 ukahamia 1999 haijakamilika leo umekamilisha kila kitu unaishi takribani baada ya ujenzi wa miaka 29 halafu mtu anakuja kubomoa kwa siku 1 tena kwa ubabe kwa sheria za kikoloni 1929......unajua uchaguzi unakaribia anasema busara zitumike wakati watu wamefariki kwa presha wengine ni masikini tayari
Chadema mnapata sana shida walahi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom