Mazingaombwe (Jugglery) ni Sayansi au Uchawi?

Tusiwe wavivu wakutafuta mambo tokea mada imetolewa mpaka leo bado amjajua tu kama si uchawi NICOLAX aligusia kuhusu muvi ya illusionist niliitafuta youtube nikakutana na jamaa mmoja ana vaa mask.Uule jamaa kaonesha mambo mengi sana mangine nilikua nayajua kitambo ila kuna mengine nimeyajua juzi tu kupitia huu uzi baada ya kutafuta youtube ni ujanja tu akuna uchawi.
Kwa hiyo baada ya kugundua hayo maujanja, sasa unaweza kupafom kama wanamazingaombwe? Mfano, unaweza kuingiza simu janja kwenye chupa ya soda?
 
Nilishawahi kuangalia show moja inaitwa "The secrets of the magicians!" inaonesha how magicians perform their tricks and at times fool u! Inshort mazingaombwe ni maujanja flani huwa yanafanyika without the audience having a slightest idea o clue of what is taking place behind the scene!
Hapo hapo kwenye audience kukosa uwezo wa kujua kinachofanyika ndio swali lilipo? Is that a science?
 
Wakuu kipindi nipo primary nimeshuhudia sana hiki kinachoitwa mazingaombwe. Toka kipindi hicho nimekuwa nikijiuliza maswali ambayo mpaka sasa sijapata majibu yake. Baadhi ya maswali ni haya.
1. Je kuna uhusiano wowote kati ya uchawi na mazingaombwe?
2. Kama hakuna uhusiano, je ni nguvu gani wanazotumia?(maana kuna wasioamini uwepo wa Mungu wala uchawi).
3. Je kuna mahali wanasomea haya mambo?
4. Vipi kuhusu historia yake, na yana nafasi gani katika hii dunia ya utandawazi?

Natanguliza shukrani...karibuni.
Mi nadhani ni uchwawi. Kuna dada alitobolewa tumbo zikatika ndizi mbivu na watu wakala. Baadae tumbo likafunga bila kidonda wala kovu.

Uke utalaam uko wapi leo mbona hatuuoni?

Uchumi wa kati umeua burudani nyingi sana.
 
Mpaka sasa hakuna jibu la huu uzi hakika likmekuwa ni swali gumu kweli kweli .Wanaonekana wataalam wa giza nao wamekula mbio kama wamesikia mlio wa risasi karibu na benki..

Sitaki kuamini Mshana Jr hujaona huu uzi .karibu utoe Neno lolote tuzidi kuunga doti.ila nimejifunza inawezekana mazingaumbwe yana kiapo cha siri ndio maana mpaka sasa kimya hakuna anayekubali kuvunja kiapo cha siri .sio kweli wote waliopitia hapa Hawajui trick .Ni mtazamo tuu
 
Mazingaombwe yako aina nyingi inategemea yako vipi ya kumbi maalumu zilizoandaliwa kabisa kwa ajili ya mchezo huo,au ni yale ya tukusanyike kokote kule na tushuhudie mfano,barabarani,mashuleni n.k, neno mazinga likiwa na maana kadhaa za kibantu kama kizuizi,mafumbo,mipaka,maficho na n.k hutumika kama utambulisho wa mchezo huo ama sanaa hiyo lakini neno ombwe likiwa na maana ya wana kadamnasi,wapokeaji,maafikiano n.k hufanya maneno hayo mawili kuwa na ukamilifu katika uwasilishwaji wake.

Kwanini nimesema inategemea na maeneo ya mchezo huo unatendeka wap na utakuwa ni wa aina ipi kwa wakati huo,sababu hii michezo tukianza kwa miaka ya zamani huko kutizama michezo hio ilikuwaga ikifanyika katika sherehe za machifu,watemi lakini baadae ikaja katika sherehe za mavuno na baadae maeneo ya biashara kama magurio na mwisho zilipoanza shule sasa maonyesho hayo ya mazingaombwe yakafikia mashuleni..

Ukweli halisi wa uo mchezo ni wa dawa za viini macho zina tafutwa zinatengenezwa sehemu na fayari kwa kwenda kufanyiwa mchezo huo kwa mitindo tofauti tofauti,kwa namna nyingine unaweza kuita uganga maana mtu wa mazingaombwe yeye pale anapokuwa mchezoni anacheza na dawa lakini pia anakuwa na watumwa ambao watumwa hawa wanakuwa na bidhaa kede kede mahusi kwa mtindo wa michezo wanaouhitaji watumwa hawa wanakuwa misukule ambao nao wanakuwa katika formula ya dawa huwezi kuwaona kwa macho ya kawaida...

Labda kuwaona kwako ww uende na hiyo dawa na wakikubaini wanakutoa sababu wale misukule wanapokuwa mizungukoni kushughulika ww utawabaini na kuharibu mchezo mfano labda nitolee umemkabidhi mcheza mazingaombwe simu simu yako ww ataipokea atampatia msukule kuipeleka mahali fulani ambapo kwa baadae ndipo atadai iko kule huku atachobaki nacho mkononi ni mzizi tu wa dawa wakat huo ww utabakia kuiona kama simu yeye ataifanyia chochote kwa uharibifu eidha kuipasua au kivyovyote vile na utahakiki imeharibiwa lakin baadae ifafuatwa ile simu sasa asili iliyopelekwa kule na msukule kisha kuletwa...

Kwenye upasuaji na uchinjaji hutumia wanyama na dawa za viini macho anaweza pasuliwa mbwa mtu akawekwa pembeni nyie mkaona kama mtu anaweza chinjwa kuku mtu akawekwa pembeni nyie mkaona kama mtu akichinjwa,

Ni marufuku na ni hatari kwenda katika mazingaombwe ukiwa na kipande kuni kilichoingia jikoni na kubaki kipisi kwa mbele kule kama mkaa,ni marufuku kuigiza maneno ya mwana mazingaombwe anayotamka kwa kumfatilisha nyuma kila atoapa hatua ya neno,ni marufuku kugeuzia nguo ya ndani katika mkusanyiko wa mazingaombwe,pia ni marufuku kuingia kinyumenyume katika ukumbi wa mazingaombwe au mkusanyiko...

Sijajua kwa sasa kama bado mazingaombwe yanafanywa maana ile michezo ilikuwa inafanywa sana na vijana waliokuwa wanajifua katika kuzinoa na majaribu ya dawa kwenye makundi tofauti ya uganga na uchawi wengi wao ndio maana hutawakuta wakiwa na mabadiliko ya kimaisha japo walikuwa wanafanya maonyesho sana maana zilikuwa ni majaribio sana sanaa ya dawa na wengi tuu walikuwa wanafeli na kuwaletea madhara watu..

Nihitimishe kwa kusema mazingaombwe ni majaribio ya dawa za kiganguzi(uchawi) japo yapo mazingaombwe ya ujanja ujanja ila kiasili ni uchawi...asanteni sana.
 
Kuna siku nilienda kufanya mazingaombwe kule Sumbawanga. Nilikuwa na uwezo wa kumgeuza binadamu kuwa panya kisha nikamrudisha tena na kuwa binadamu.
Basi nikaenda sokoni nikawakusanya watu, nikamgeuza jamaa kuwa panya.
Kulikuwa na mama mmoja pembeni akajigeuza na kuwa paka, kisha akammeza yule panya, na baada ya hapo akarudi kwenye umbo lake la ubinadamu.
Nilijuta kuzaliwa, sitaki kukuelezea kilichotokea baada ya hapo.
...Mkuu Bujibuji, hii nahisi inafaa zaidi Kyle jukwaa LA Vichekeko!!!
 
Kuna siku nilienda kufanya mazingaombwe kule Sumbawanga. Nilikuwa na uwezo wa kumgeuza binadamu kuwa panya kisha nikamrudisha tena na kuwa binadamu.
Basi nikaenda sokoni nikawakusanya watu, nikamgeuza jamaa kuwa panya.
Kulikuwa na mama mmoja pembeni akajigeuza na kuwa paka, kisha akammeza yule panya, na baada ya hapo akarudi kwenye umbo lake la ubinadamu.
Nilijuta kuzaliwa, sitaki kukuelezea kilichotokea baada ya hapo.

Liongo wewe
 
Nilishawahi kuangalia show moja inaitwa "The secrets of the magicians!" inaonesha how magicians perform their tricks and at times fool u! Inshort mazingaombwe ni maujanja flani huwa yanafanyika without the audience having a slightest idea o clue of what is taking place behind the scene!
Lakini ile ni ana kwa ana, behind the scene hazina nafasi
 
Kuna siku nilienda kufanya mazingaombwe kule Sumbawanga. Nilikuwa na uwezo wa kumgeuza binadamu kuwa panya kisha nikamrudisha tena na kuwa binadamu.
Basi nikaenda sokoni nikawakusanya watu, nikamgeuza jamaa kuwa panya.
Kulikuwa na mama mmoja pembeni akajigeuza na kuwa paka, kisha akammeza yule panya, na baada ya hapo akarudi kwenye umbo lake la ubinadamu.
Nilijuta kuzaliwa, sitaki kukuelezea kilichotokea baada ya hapo.
Member wa zamani mmepata umaarufu kwa uongo uongo kama hivi

Ndio maana siku zote nasema Mshana Jr ni mjanja mjanja tu wala hakuna anachofahamu, nakumbuka alikamata hadhira kwa vistori vya uchawi mpaka leo ndio umaarufu wake lakini nachojua si mchawi, mganga wala hajui mambo hayo
 
Salaam wakuu

Nimeangalia video nyingi Sana za hawa magicians Wazungu kwa Waafrika na nimejikuta najiuliza maswali mengi Sana kuwahusu wao na pia kila kukicha wanaibuka wapya

Unakuta mtu anatafuna viwembe vya kutosha tu alafu anatafuna na uzi alafu anashushia na maji baada ya hapo anavitoa vile viwembe vikiwa vimejipanga kwenye ule uzi na maajabu mengine mengi tu

Hivi wakuu hawa magicians nguvu zao zinazowawezesha kufanya magics wanazitoa wapi/wanazipataje?

Je,Kuna vyuo wanavyofundisha magics?

Au niwaongo tuu hawafanyi ukwelii kwamba wanafanya tricks?
images%20(5).jpg
images%20(4).jpg
images%20(3).jpg
 
Nyingine ni tricks nyingine ni uchawi...mfano ukiona MTU anaetafuna viwembe na chupa ujue hiyo kala dawa....na inakua pia kinga ya sumu...MTU anaekula viwembe..chupa ..sindano na pin...hafi kwa sumu iwe ya kulishwa..au kunyweshwa
 
Mkuu mtu ale dawa gani ili akitafuna hizo chupa na viwembe visimdhuru?

Unamaanisha dawa gani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom