Mazingaombwe: Imeishia wapi ile michezo? Wewe unakumbuka nini enzi zako?

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,540
12,398
Habari za mchana wanajamvi?

Bila shaka shughuli zimekwenda vizuri katika muda huo wote tangu tumeanza pale asubuhi na mapema!

Jamani kuna wakati Miaka ya 1980 hadi mwisho wa miaka ya 1990 kulikuwa na watu waliotambulika kuwa wana mazingaombwe walikuwa wakija mashuleni wakati ule tupo shule za msingi.

Hawa jamaa alikuwa wakionesha mambo (michezo) mbalimbali ya kimazingaombwe; mfano kijiti kugeuzwa Penseli, kishikizo kugeuka Pelemende na kadhalika, swali linakuja hivi ni kwa namna gani yale mambo yalikuwa yakitokea je kuna uhusiano na ushirikina?

Wakati mwingine walikuwa wanajiita Pawa (Power) kwa maana ya mtu mwenye nguvu za ajabu waliweza kuzuia magari na pikipiki (sikuwahi kusikia kuhusu Treni)!

Na mbona imetoweka kabisa au ni kwa sababu ya kukuwa kwa sanyansi na Teknolojia ikihusisha kuwapo kwa michezo mingi ya kiteknolojia zaidi au kuna sababu nyingine ya kutowesha hiyo michezo?
 
Haijatoweka mzee kwani hukuiona uwanjani kwenye sherehe za miaka 50 ya uhuru wa iliyokuwa tanganyika
 
Wanafanya sana Misikitini mkuu...jitahidi kutembelea misikiti utakutana nayo tu maana mitambo ya kufanya mazingaombwe ni MAJINI
 
Kuja kwa television kumebadili sana mambo mengi, watoto wetu kidogo tu wako kwenye kuangalia muvi za kina Kanumba.
 
Kuja kwa television kumebadili sana mambo mengi, watoto wetu kidogo tu wako kwenye kuangalia muvi za kina Kanumba.

Lakini hii michezo mostly si ilikuwa inapelekwa mashuleni au kuna wakati serikali ilipiga marufuku?
 
duh,namkumbuka power mabula enzi hizo pale makurumla shule ya msingi(mwembechai)siku hizi kuna shule mbili sijui,yani mpaka ladha imepotea,..ndugumbi,nyerere primary school..crap..mnatuharibia historia
 
Wanafanya sana Misikitini mkuu...jitahidi kutembelea misikiti utakutana nayo tu maana mitambo ya kufanya mazingaombwe ni MAJINI

Serious? Wewe una kizibo lazima! mazingaombwe si wanafanya kila siku wakina mzee wa upako, mwingira, kakobe..na wewe kwa ujinga wako unaamini ni kazi ya mungu!
 
Ipo, sema wanamazingaombwe wetu hawa-advance, angalia wakina Brain, Wakina Angels; wanafanya mazingaombwe na viinimacho na wanatengeneza pesa za kutosha kabisaaaa huku watu wakitoka intertained!
 
Wanafanya sana Misikitini mkuu...jitahidi kutembelea misikiti utakutana nayo tu maana mitambo ya kufanya mazingaombwe ni MAJINI

Duh naona umeongea kinyume: Mazingaombwa ni technik inayotumiwa na makanisa mengi ya maombezi; mifano yake ni kuponya vilema feki, kuponya magojwa, kikombe cha mchungaji loliondo, misukule feki. TANZANIA YA SASA NI SAWA NA NIGERIA kwa utapeli makanisani
 
Ipo, sema wanamazingaombwe wetu hawa-advance, angalia wakina Brain, Wakina Angels; wanafanya mazingaombwe na viinimacho na wanatengeneza pesa za kutosha kabisaaaa huku watu wakitoka intertained!

Hao uliowataja kwa majina wana-movie zao au ni novel?
Nawezaje kupata nijikumbushe walau maisha ya zamani wakti ule double cola ilikuwa sh. 5 pekee!
 
...zamani mazingaombwe ulikuwa mchezo tu. Siku hizi wachezaji walewale wanawaibia watu kwa kutumia mchezo uleule kwa kujifanya waganga eti. Amakweli WAJINGA NDIO WALIWAO!!
 
Back
Top Bottom