Maziko ya Bi. Safia bint Juma Makasara - Mama yake Balozi Dr. Dau

Mzee hajielewi huyu ana udini sana...sasa hapo kuna watu wengi kuzidi misiba ya Mzee Nyerere, Kanumba na Rais John Pombe Magufuli??Muda mwingine tuweni wa kweli na wawazi hii mitandao isitudanganye kwa faida yako au dini yako
Na habari zake n za waislamu tuu

Mzee kifupi n mdini japo anamambo mengi ya manufaa kwa umma ila sipendi anapoingiza Sana udini

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Na habari zake n za waislamu tuu

Mzee kifupi n mdini japo anamambo mengi ya manufaa kwa umma ila sipendi anapoingiza Sana udini

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Peramiho...
Jina lako ni Peramiho na mimi naijua historia ya Peramiho lakini sikuiti mdini.

Bahati mbaya tumekuwa leo na hofu ya kitu chochote kinachohusu Uislam na Waislam.

Unataabika kusoma historia ambayo utawakuta Waislam wametawala.

Kama nisingenyanyua kalamu kuandika kitabu cha Abdul Sykes historia ya uhuru ingepotea na sababu ni kuwa walioshika madaraka ya uongozi walikuwa na hofu
na Uislam na Waislam na historia ya uhuru ilijaza Waislam katika mstari wa mbele.
 
No hard feelings kabisa nimependa unachofanya watu wengi tulikuwa hatujui kuhusu ukweli wa uhuru wa Tanganyika…kuhusu historia ya jiji la Dsm…na mambo mengi kuhusu watu wake wazawa….hongera sana na Mungu akubariki.
 
Paris...
Ahsante.
 
Mzee ni kweli Tanzania all Muslim party ilikwamisha kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika mapema?
 
Mzee ni kweli Tanzania all Muslim party ilikwamisha kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika mapema?
Impipi,
Walikuwa na fikra hiyo kwa hofu kuwa Waislam hawatatendewa haki uhuru ukipatikana.

Ikawa wao wanataka kwanza Waislam wanyanyuliwe katika elimu kufikia kiwango cha wao kushika madaraka sawa na Wakristo.

Walikuwa na uwezo wa kutaka haya kwa kuwa Waislam ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Waislam hawakuwaunga mkono AMNUT.
Historia ya AMNUT nimeieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Soma barua ya AMNUT kwenda UNO 1960:

1638328932491.png
 
Wote hawa nimeshuhudia tu maziko ya shekh ilunga kapungu ama kweli ulikuwa ni ummat uliojaa, allah awarehemu
 
nashindwa kuelewa watu wenye makasiriko..huyu mwandishi ana andika juu ya kile anachokifahamu kwa hadhira fulani anayoifahamu, anatoka mtu huko kavimbiwa viazi anamuamulia juu ya andiko lake.., ukiangalia mtiririko wa hao waliotangulia ni jamii fulani hivyo hiyo rekodi inahusu jamii fulani, sio nchi nzima jamani..mwacheni mzee wa watu atiririke, ndio humo humo kuna vitu na wengine tunajifunza.
 
Kimo...
Uchaguzi wa Kura Tatu mwaka wa 1958 ulisababisha farka ndani ya TANU na wa kwanza kujitoa katika chama alikuwa Zuberi Mtemvu akaunda African National Congress (ANC) chama hiki kikajulikana kama Congress katika umaarufu wake.

Wanachama wake wakaweka kibwagizo cha maneno haya katika kukisifu chama chao, ''Congress Jiwe Lisilovunjika.''

Baada ya Mtemvu kutoka TANU, Mashado Ramadhani Plantan na yeye akajitoa TANU akaunda All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT).

Hiki chama kilisababisha hofu kubwa sana na si tabu kuelewa kwa nini.

Zuberi Mtemvu chama chake kilikuwa kimesimama kwenye sera ya Afrika kwa Waafrika lakini chama cha Mashado Plantan kiliangalia maslahi ya Waislam baada ya uhuru hofu ikiwa Waislam kutotendewa haki na wale watakaoshika madaraka.

Kitu gani killisababisha hii shaka?

Ukoloni uliwanyima Waislam elimu, elimu ikawa katika mikono ya serikali na Wamishionari.
Ikawa wazi kuwa uhuru utakapopatikana watakaoshika madaraka ya kuendesha nchi watakuwa Wakristo.

Swali likawa, je hawa Wakristo wakiongozwa na Julius Nyerere watafanya uadilifu kuona kuwa Waislam wanatendewa haki na watapata fursa za elimu kama wengine?

AMNUT ikadai kuwa uhuru ucheleweshwe hadi pale Waislam watakapo kuwa na elimu ya kushiriki katika uendeshaji wa serikali.

Dai hili lilipingwa na TANU kwa mantiki kuwa hali ya baadae ya Waislam si suala la kujadiliwa na Waingereza waliokuwa wanaitawala Tanganyika.

Suala la Waislam hili litatatuliwa na serikali huru ya Tanganyika.
Huu ndiyo ulikuwa msimamo wa TANU na ahadi ya TANU kwa Waislam.

Katika hotuba yake maarufu ya kuaga alipostaafu aliyoitoa Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985 Mwalimu Nyerere aliwaeleza Wazee wa Dar es Salaam aliokuwa anawahutubia kuwa ametimiza ahadi yake ya kuleta usawa baina Waislam na Wakristo kiasi kuwa hawezi kujua waziri anayemteua ni Muislam au Mkristo.
 
Mzee hajielewi huyu ana udini sana...sasa hapo kuna watu wengi kuzidi misiba ya Mzee Nyerere, Kanumba na Rais John Pombe Magufuli??Muda mwingine tuweni wa kweli na wawazi hii mitandao isitudanganye kwa faida yako au dini yako
We ndio mdini Sasa nyang'au we! Idiot
 
Kizeze,
Kila mwandishi anakuwa na watu wake anaowaandikia.

Mimi nimetokana na jamii ya mjini Dar es Salaam na ninaponyanyua kalamu hawa ndiyo ninaowaandikia.

Hii sikuanza leo.

Wengi hapa JF wamenifahamu kwa kuandika historia ya watu wa pwani na mfano wa hao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia hii iligueza historia iliyokuwapo na kufunzwa shule za msingi hadi vyuo vikuu.

Niliamua kuandika historia hii kwa kuwa hakuna mtafiti aliyeiandika labda kwa kuwa si historia yao hivyo hawaijui au waliona haina umuhimu.

Wala mimi sikusema hawakuiandika kwa sababu ya udini.

Sikuona haja ya kukejeli wala kuandika maneno makali kwa sababu historia ya wazee wangu na jamii yangu haikuandikwa.

Wala sikughadhibika kuwa historia inayosomeshwa imetutupa nje.

Nilichofanya niliamua kufanya utafiti na kuandika.

Kilichonishangaza ni kuwa wako waliokujakunilaumu kuwa nimesukumwa kuandika kwa sababu za udini.

Hawa wote ni watu wa hapa nyumbani.

Nje ya mipaka ya Tanzania historia hii ilipokelewa vyema sana na nikaalikwa vyuo vingi kuzungumza.

Sasa ninapoandika historia ya maziko makubwa ninakusudia kueleza historia ya jamii yangu ifahamike ilikuwaje.

Hakuna anaekataa kuwa maziko ya Mwalimu Nyerere yalikuwa makubwa.

Lakini nitakuambia kitu.

Nyerere alipofika kwenye maziko ya Abdul Sykes hakuamini macho yake.

Alikuwa hajapata kushuhudia mazishi kama yale.

Sasa kama nisingeandika historia hii wewe ungeyajuaje haya?

Kuna mengi tungeweza kujadili kwa taratibu bahati mbaya historia hii inawapandisha hasira.

Ningeweza kuhadithia jinsi Mwalimu Nyerere na Mama Maria walivyopokelewa Dar es Salaam katika mitaa ya Kariakoo na wazee wetu na mapenzi yaliyokuwa baina yao.

Ningeweza kueleza maisha yalivyokuwa na mapenzi yaliyojengeka baina yao na kisa kilichomshtua Abdul Sykes siku ilipodhaniwa Nyerere kalishwa sumu katika chakula nyumbani kwake.

Mengi ninayo kwa kuwa ingawa mimi nilikuwa mtoto lakini ni sehemu ya historia hii na waliofanya haya ni wazazi wangu.
Mzee mohamed said achana na hao vitoto vipuuzi ambao hawajielewi hao
 
Ukubwa wa Mazishi una vigezo vipi ? Labda tukianzia hapo ndio tutakwenda sambamba ya yapi ni makubwa na madogo ni yapi...., Ingawa sidhani kama kulinganisha ukubwa huu una tija sana.... Anyway asante kwa Taarifa
 
Key...
Sikiliza hii video naeleza maziko makubwa mwaka 1968 na yale yaliyokuwapo:

Thread 'Zumari: Maziko ya Abdul Sykes 13 oktoba 1968' Zumari: Maziko ya Abdul Sykes 13 oktoba 1968
 
Key...
Sikiliza hii video naeleza maziko makubwa mwaka 1968 na yale yaliyokuwapo:

Thread 'Zumari: Maziko ya Abdul Sykes 13 oktoba 1968' Zumari: Maziko ya Abdul Sykes 13 oktoba 1968
Sasa mkuu wewe Tozo hazijakukumba huko ulipo ? Nimekuomba tu vigezo vya ukubwa na udogo kama hautojali kwa sentensi chache wewe unaniambia nikatumie MB zangu chache za kudunduliza nikaangalie video..., Kweli tunatakiana Heri sisi kama Watanzania ?
 
Back
Top Bottom