Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze?

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,068
184
:israel:Wana JF;

Mimi na wenzangu tumeamua kutafuta eneo la kilimo maeneo ya Chalinze, kama kilometa 10 - 15 kutoka pale Chalinze mjini. Mipango yetu y amuda mrefu ni kufanya kilimo cha mazao ya kudumu na cha kitaalamu. Kwa wenye uzoefu na maswala ya kilimo, hali ya udongo (Ardhi) n.k naomba mnisaidie mawazo ya nini kinafaa kulimwa pale (Mazao gain yanayostawi vema na yanayofaa kulimwa kule)
Natanguliza shukrani zangu za dhati:israel:
 
Chukua sample ya udongo peleka SUA watakufanyia analysis na kukushauri cha kulima.
Ila vinanasi na machungwa yanastawai sana pale
 
Ni kweli Njowepo... Lakini eneo lote kuanzia unapovuka mto Ruvu kuelekea Morogoro ukitokea Dar hadi Mdaula kunapata Mvua kidogo saaana... Labda afanye kilimo cha umwagiliaji... Lakini chanzo cha maji kipo mbali sana...
 
Kama ni lazima ulime Chalinze,basi fuata maelekezo haya, ukitoka Dsm kwenda Chalinze, kabla hujaingia Chalinze mjini mkono wako wa kulia kuna misufi mingi na petro station fulani hivi. Kuna kiukuta na njia/barabara ndogo inaingia ndani. Pembeni yake huwa wanapaki basikeli za kukodi. Ukifika pale uliza njia ya kwenda Talawanda/magurumatali. Ni km 20 toka Chalinze mpaka Talawanda. Eneo lote kuanzia pale chalinze mpaka Talawanda linafaa sana kwa kilimo cha ufuta,mahindi,alizeti,karanga, korosho,mtama na ufugaji wa mbuzi, na udongo wake ni mzuri sana. Mvua za pwani unazijua vizuri. Ardhi bado kubwa sana na haijatumika vilivyo. Moja ya ahadi ya rais ni kupeleka maji toka wami.

Tahadhari ukifika Maguru matari,kuna pori la watu pale la eka 500. Kama ni kilimo cha mvua za Mungu huko kunafaa.
 
bei kwa ekari au kukodi nisaidie .
 
Back
Top Bottom