Mazao gani unayoweza kulima pamoja na mihogo na yakaongeza rotuba ya udongo?

Idrissou02

JF-Expert Member
Jul 31, 2018
354
643
Naam mm ni mkulima ambae nimekua nikilima mihogo sana, sasa naona ardhi yangu inaanza kupunguza uzalishaji. Nimewahi kuskia nikilima mihogo pamoja na mazao mengine yanayoendana yataongeza rotuba ya udongo.

Msaada, ni mazao gani hayo?
 
Lima mihogo yako panda pamoja na mazao jamii ya mikunde(kunde, choroko, Maharage)
Pia kua na utamaduni wa kuacha masalia ma mazao shambani yaoze yachanganyike na udogo ili kuongeza(Organic matter)
 
Pia fanya fallowing(Pumuzisha shamba hata miaka 2-3), fanya crop rotation(yaani ukilima mwaka huu mihogo mwaka unaofuaata lima mahidi+kunde, mwaka mwingine lima zao lingine, Weka mbolea ya samadi, zuia mmomonyoko wa udogo, epuka kulima kwa kutumia heavy equipment(viafaa vinatifua sana ardhi kama jembe la tractor, lima kwa kutumia conservation tillage, fanya conservation farming(panda bila kulima)
Yapo mambo mengi ukitaka kuhifadhi rutuba ya udogo/aridhi yako naomba niishie hapo
 
Kitambo kulikuwa na mmea unaitwa marejea, shamba likichoka unapanda huo
 
Back
Top Bottom