SPINE
JF-Expert Member
- Dec 11, 2017
- 1,062
- 1,136
Habari wakuu, kama kichwa cha habari kilivyo, naomba kujua yale mayai ambayo yanafaa kutumika kutotolesha vifaranga vya kuku wa nyama yanapatikana wapi kwa mkoa wa Arusha. Vifaranga vimekuwa adimu sana hapa Arusha, nina mpango wa kuvuta incubator wiki chache zijazo ila nimeona ni vyema kujua haya mayai yanapatikana wapi maana najua yana muda maalum wa kutumika baada ya kutagwa na pia yawe ni yale yaliyorutubishwa na jogoo. Naomba kwa anaefahamu anijuze, idadi ni mayai 1000 kwa kila awamu......asanteni.