Maxence Melo, tutapambanaje na sheria kandamizi bila kupambana na wakandamizi?

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
3,948
2,000
Kwanza nikupe hongera wewe binafsi kwa kitendo cha kishujaa sana cha kusimamia kile unachoamini ni haki bila kujali nguvu za unayepambana nae.

Naomba nimquote R. F. K akisema
“ Few will have the greatness to bend history itself, but each of us can work to change a small portion of events. It is from numberless diverse acts of courage and belief that human history is shaped. Each time a man stands up for an ideal, or acts to improve the lot of others, or strikes out against injustice, he sends forth a tiny ripple of hope, and crossing each other from a million different centers of energy and daring those ripples build a current which can sweep down the mightiest walls of oppression and resistance.
Robert F. Kennedy

Pili niwapongeze wote, kasoro CCM, waliokupigania kwa njia
mbalimbali kuhakikisha kuwa kwa wewe na kile unachokisimamia, haki inatendeka.

Binafsi nimesoma na kutizama na kusikia kutoka vyombo mbalimbali vilio, hoja, mitazamo mbalimbali kuhusu kile unachokisimamia, uhuru wa mtu kutoa maoni yake.

Nimeona clip moja YouTube unaposikika ukisema wewe huna tatizo na mtu yoyote katika sakata hili kwa kuwa walikuwa wakitimiza wajibu wao.
Na hapa haswa ndio linapotokea swali langu; tutapambanaje na sheria kandamizi juu ya uhuru wa kutoa maoni, juu ya uonevu, bila ya kupambana na wakandamizi /waonevu?

Nitajitahidi kukuonyesha wakandamizi /waonevu hao.
Serikali iliyoko madarakani ni serikali ya CCM. Inatekeleza ilani ya CCM. Ilani ya CCM ni kandamizi kwakuwa imeandikwa na wakandamizi.
Katika mambo mengi ya kikandamizi, imewaelekeza wakandamizi ndani ya serikali kutunga, kupitisha na kusign sheria kandamizi juu ya utoaji wa maoni.
Hapa naongelea wizara ya habari na michezo chini ya Nape Nauye, wabunge wa CCM na rais Magufuli.

Sasa ndugu Melo na wadau humu ndani mnisaidie ; tutapambanaje na panga bila ya kupambana na mwenye panga?

Kwa maoni yangu, CCM ndio chama kandamizi, chenye ilani kandamizi, wabunge kandamizi, rais kandamizi na wote kwa pamoja ndio wanaozaa sheria kandamizi. Tukiwaondoa hawa kwenye nafasi ya kutukandamiza nakuhakikishia hawata acha kitu nyuma.
WATAONDOKA NA SHERIA ZAO KANDAMIZI.
 

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
2,968
2,000
Waliounga Mkono Vipengere vya kwenye Sheria za Mitandao na Vyombo vya habari ambavyo ni vya kikoloni huku wakiwatukana wale wote waliokuwa wanapinga kwa hoja eti leo wanajidai nao wanamuhurumia Max.
 

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
3,948
2,000
[HASHTAG]#usirudiekosa2020[/HASHTAG]

“ The oppressed are allowed once every few years to decide which particular representatives of the oppressing class are to represent and repress them.
Karl Marx
 

kahupwe

JF-Expert Member
Sep 9, 2016
290
250
Ni ukweli ulio wazi ni wabunge wa CCM,waliohongwa miliono kumi ni wabunge haohao waliopitisha sheria kandamizi ya habari.Halafu wanajidai kupambana na rushwa utambanaje nayo wakati wewe unaishi kwa rushwa? CCM na rushwa ni koromeo na mdomo bila rushwa hakuna CCM.Nawasilisha.
 

martin kabaya

Member
Nov 20, 2016
41
95
Waliounga Mkono Vipengere vya kwenye Sheria za Mitandao na Vyombo vya habari ambavyo ni vya kikoloni huku wakiwatukana wale wote waliokuwa wanapinga kwa hoja eti leo wanajidai nao wanamuhurumia Max.
Swala ni kwamba walisha pndua nchi bac wawaachie na wengine waongoze
 

georgemwaipungu

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
2,780
1,500
Mkuu, ni kifungu gani cha Ilani ya chama CCM wanaelekeza sheria kandamizi zitungwe? Nitashukuru sana kuona hicho kifungu.
Wewe kweli dudus una macho huoni?
Ndiyo maana wanapendekezwa akina jecha kwenye ccm maana sifa si Elimu bali kujua kusoma kiswahili ama kiingereza.
Hata wewe yawezekana una sifa hizo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom