Maxence Melo: Rais Magufuli anafanya vyema katika Mapambano dhidi ya Ufisadi lakini tunahitaji Taasisi imara

Status
Not open for further replies.
Taasisi zote sasa zinafanya kazi vile atakavyo uchwara. Kwa maneno mengine hakuna kazi yoyote inayofanywa wakati uchwara mwenyewe ndiye mlezi na mtoa rushwa mkubwa hadi ndani ya Bunge.

Tunatengeneza taasisi nyingi sana imara kuzuia rushwa lakini kama watu hawabadiliki ni kazi bure.

Tatizo la rushwa nchi hii sio taasisi wala sheria, tatizo ni uadilifu wa mtu mmoja mmoja na kulindana.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo akihojiwa na vyombo vya Reuters na Sauti ya Amerika(VoA) amesema ...
“Hadi sasa tunapambana na ufisadi wa awamu zilizopita, uhuru wa kuongea na Bunge huru vimesaidia haya kuibuliwa awamu zilizopita, awamu hii ikitoa uhuru wa kutosha basi Rais hata kabla hajarudi bandarini Dar es Salaam vyombo vya habari vitakuwa vimeshaibua mengine makubwa ambayo yatachangia juhudi za kupambana na ufisadi.”...
Katika yote aliyoyasema, hilo hapo ndilo la msingi lifanyiwe kazi ya dharura, kama siyo ziada, na Rais Magufuli na serikali ya CCM.
 
Bado sijaona akipambana na ufisadi wowote zaidi ya kufuatilia BAADHI ya wanaoitwa mafisadi ila wale Mafisadi haswaa hawaguswi.
 
Hebu acha kukurupuka Mkuu! Dah!
Hebu tuambie huu uchunguzi ni mwaka sasa ripoti ya Takukuru inatolewa lini!?

Au kwa kuwa mtoa rushwa ni uchwara mwenyewe kwa Wabunge wa MACCM. Takukuru wamepigwa marufuku kuchunguza hili!?

Takukuru yachunguza Sh10 milioni za wabunge CCM
Hiyo siyo rushwa ni motisha kutoka kwenye ruzuku ya CCM. Mkuu muulize mwenyekiti wa Chadema fedha za ruzuku za Chadema zinafanya nini
 
Acha kujitoa ufahamu weye!!! Kwenye bajeti inayotokana na pesa za walipa kodi hakuna fungu la motisha. Upuuzi peleka lumumba si humu. Kama huna la maana la kuandika kaa kimya.

Hiyo siyo rushwa ni motisha kutoka kwenye ruzuku ya CCM. Mkuu muulize mwenyekiti wa Chadema fedha za ruzuku za Chadema zinafanya nini
 
Acha kujitoa ufahamu weye!!! Kwenye bajeti inayotokana na pesa za walipa kodi hakuna fungu la motisha. Upuuzi peleka lumumba si humu. Kama huna la maana la kuandika kaa kimya.
Sawa mkuu nakusubiri utoke kwenye mazishi ya mbwa halafu tuendelee na mjadala
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom