Maxence Melo na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, wapo Clouds TV kipindi cha 'Tathmini ya Uchaguzi'

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Wakuu,

Hapa naangalie Clouds TV namuona Mwenyekiti wa ACT - Wazalendo, Anna Mghwira akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media wamiliki wa mitandao ya FikraPevu.com pamoja na JamiiForums Maxence Melo, kwenye kipindi cha 'Uchaguzi Tathmini' wanaelezea jinsi uchaguzi ulivyoenda na nafasi ya mitandao ya kijamii.

Mama Mghwira, anaelezea kuwa kipindi cha kampeni za urais ilifikia hatua walikosa coverage kwenye media, na kwamba Watanzania tumeiga vitu vingi kizungu, ukoloni ni mwingi sana.

Amesema pia kwamba kama tunahitaji mabadiliko tunatakiwa tuweze kushughulikia suala la Katiba Mpya itokanayo ili miaka mingine ijayo, tuwe na mabadiliko mazuri ya kisiasa, kwani siasa zilizopo sasa ni siasa za watu wengine.

-Anasema maisha yetu hatutakiwi kuishi kwa ahadi tu, lazima mambo yanayoahidiwa yatekelezwe, hivyo Katiba Mpya ituweke sawa na kutazama kama ndugu. Nilipata nafasi ya kuwatembelea watanzania kama Mwanasiasa, kama mtafiti lakini hili ninataka tuzunguke tena tudai katiba mpya.

-Aidha, ameelezea kuwa Waafrika ni wanyenyekevu, hivyo tunatakiwa tutumie unyenyekevu wetu kunufaika na mali zilizopo nchini kwamaana kama sasa hatutakuwa tayari kipo kizazi kitakazokuja kitakachohitaji kutumia mali zilizopo ikiwemo gesi, mafuta na uchimbaji wa madini.

-Anasema walifanya kampeni za Kitanzania kwasababu walipoishiwa fedha za kufanya kampeni walitulia kimya na wanapopata hela waliendelea na zoezi.

-Pia alikuwa amejiandaa kisaikolojia kugombea Ubunge, kwa muda mrefu walikuwa wakitafakari namna ya kuwa na mgombea urais hivyo kwa muda huo ilimwia vigumu kujua kuwa angesimama kuwa mgombea urais.

Maxence Melo, anasema kuna haja ya vyama vichanga kupewa ruzuku ili waweze kufanya kampeni sawa na vyama vikongwe kama kuna uwezekano.

-Anasema JamiiForums walitoa nafasi kwa UKAWA, CCM na vyama vingine vya siasa kutangaza na mtandao wao lakini waliojitokeza ni wachache na wengi wao walikuwa wanalalamika kuwa kuna upande unapendelewa kutokana na baadhi ya watumiaji wa mtandao kushindwa kujua platfom ya JF.

Maxence, amemuuliza mama Anna kuwa wamefanikiwa kuwa na Mbunge mteule mmoja kwa Tanzania nzima, je, viti vya udiwani nchi nzima viko wangapi?

Mama Anna amesema wana jumla ya Viti 30 vya udiwani nchi nzima na pia walikuwa na wagombea ubunge 150 nchi nzima lakini hadi mwisho wa kampeni walikuwa na watu waliotangaza nia 216, amesema uwezo wa kuendesha kampeni za sera kwa wagombea wao ilikuwa ni changamoto.

-Maxence, anasema kuna majeraha yamebaki kwenye vyama vya siasa kutokana na michakato ya kuwania uongozi wa nafasi za juu, je ACT hawakupata majeraha yeyote?

-Mama Anna anasema wakati wa kuandaa wagombea urais walipitia changamoto nyingi kuanzia kwa Prof. Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba hadi kwake yeye mwenyewe ilikuwa shughuli nzito.

-Maxence, amesema Rais anayekuja ajitahidi kutuunganisha Wanzania ili wawe kitu kimoja na pia amesisitiza kuwa rasimilimali zilizopo nchini ni kwa ajili ya Watanzania wote na sio kwa ajili ya wanasiasa.

Amesema taunze ukurasa mpya chini ya Rais Mteule, Dk. Joseph Magufuli.
 
Evident : Act-Wazdo lack of clear strategy and overstretching of meagre financial and human resources
 
Aisee nasikitika kukosa hicho kipindi......Mghwira ana madini kichwani.
 
Zitto alinidanganya akina Habibu mchange wakawa wanapayuka payuka ovyo. Wamekosa sasa sijui itakuwaje ?
 
Eti mama kichwa ....... watu wanajisahaulisha kanuni za siasa MDOMONI UWE VIZURI.
 
Usihangaike. Ninamfahamu vizuri sana sana Anna Mughwira. To be brief, anatafuta cheo tu. Not more.
 
Back
Top Bottom