Maxence Melo na JF ni underrated. Wapewe heshima wanayostahili, wao ni zaidi ya akina tiGO, Voda na wengine

CCM Music

JF-Expert Member
Dec 5, 2018
1,036
1,782
Ki ukweli Melo na JF kwa ujumla ni wadogo sana ukilinganisha na akina Tigo, Voda na wengine.

Lakini hawa Jamaa pamoja na udogo wao wamepambana waziwazi mahakamani kulinda faragha ya watumiaji wa mtandao wao.

Hawa Jamaa wamepambana uso kwa uso na Polisi.

Wamepambana uso kwa uso mahakamani.

Wamepambana uso kwa uso na Serikali ya awamu zote.

Na zaidi ya yote bado Jamaa hawaja surrender. Yaani bado msimamo wao nni ule ule wa kulinda faragha ya watumiaji wa mtandao wao.

Haijawahi kutokea hata kwa mara moja mtu kwa kutumia ID ya JF akapelekwa mahakamani kwa sababu ya andiko lake humu.

Haijawahi kutokea hata mara moja user wa JF akapelekwa Polisi kwa sababu ya andiko lake humu.

Yote hayo ni kwa sababu Melo kama Mkurugenzi Mtendaji wa JF kwa ujumla husimama imara kulinda faragha ya wateja wao.

Kuna mtu anaweza kudhani hii kazi ni ndogo sana. Ukitaka kujua uzito wa hii kazi kumbuke yale ya akina Voda na haya ya sasa ya akina Tigo.

Ki ukweli Melo na JF kwa ujumla wapo under rated mno !

Swali dogo:

Najua na inajulikana kuna watu kwenye mamlaka ambao mara kadhaa wametaka kufahamu privacy kadhaa za watumiaji wa mitandao yao.

Je, ni lini walau kumewahi kuwepo hata kesi moja ya uchawara mitandao hio ikijaribu kulinda faragha ya wateja wake?
 
Tigo na Voda wanafanya haya kwasababu wanajua, kwa ujinga wetu, hatuwezi kuungana kuwaonyesha sisi wateja ndio kila kitu.

Wabongo wanaamini, likikukuta, hilo haliwahusu. Yaani hatuna akili ya kujiongezea kujua kesho inaweza kuwa ni zamu ya mtu mwingine.

Sometimes I wonder if we deserve to be called human beings.

Someni mawazo haya ya wenye kufikri sawa sawa.

Screenshot_20211103-183509_Twitter.jpg
 
Tigo na Voda wanafanya haya kwasababu wanajua kwa ujinga wetu, hatuwezi kuungana kuwaonyesha sisi wateja ndio kila kitu
Halafu JF ndo wangeamua kusema hata usipotembelea JF kimpango wako nadhani la kupoteza ukilinganisha na mitandao ya simu
 
Naunga mkono hoja

P
 
Naunga mkono hoja
P
Siyo yuda kama wewe kisa kufuata ganda la ndizi.
 
Naunga mkono hoja
P
Mkuu kuna deal la U dc , nikuunganishe na waziri wa Local gvt ?
 
Kabisa. tiGO yaani hawana hata aibu!! Waziwazi kabisa namna hiyo!! Potelea mbali, contacts zote nimehamishia google account, line ya tiGO imeungana na takataka zingine, kiberiti kimeshughulika!!

Next. Watu wa tiGO sitopokea simu zenu tena
 
Back
Top Bottom