Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, ahojiwa kwa tuhuma za kula njama za kutaka kumuua Cyprian Musiba

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,876
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anahojiwa na ofisi ya Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai ( DCI) Jijini Dar Es Salaam muda huu.

Maxence anahojiwa muda mchache baada ya magazeti ya leo ya Tanzanite na Fahari Yetu kuandika kwamba Maxcence Melo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, TCRA, Balozi Emmanuel Nchimbi na Benard Membe wanapanga njama za kumuua Cyprian Musiba.

Maxence anahojiwa chini ya wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Jones Sendodo.

Mbali na Maxence Melo, Magazeti ya Tanzanite na Fahari yetu, yamedai kwamba Mkakati huo wa kumuua Musiba unapangwa pia na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Watumishi wa Jeshi la Polisi Nchini na Kigogo wa CCM.

Wengine walio kwenye mkakati huo wa kutaka kumuua Musiba ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil Dkt. Emmanuel Nchimbi, Benard Membe, Ofisi ya DDP, Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Kipingu.

Magazeti hayo yamedai watumishi wa TCRA wamefunga account za Mitandao ya Kijamii ya Musiba na kufuatilia Mawasiliano yake.

Gazeti hilo limedai pia kwamba watu hao wanajipanga kifungua kesi nne, Mbili mahakama kuu na mbili mahakama ya Kisutu. Mbali na kesi pia kwamba wana mpango wa kuondoa uhai wake.

Pia Magezeti hayo yamedai kwamba hili Genge linalotaka kumtoa uhai wake, lilikuwa na mkakati wa kuhakikisha wanamuondoa rais Magufuli kupitia baadhi ya wajumbe wanaoingia katika mkutano mkuu wa CCM (NEC) na Kamati kuu(CC), ili asiweze kuendelea na kipindi chake cha pili cha Urais.

Cyprian Majura Musiba ambaye alikuwa Mtangazaji wa zamani wa runinga ya Channel Ten na radio ya Magic FM, ni Mkurugenzi wa kampuni ya CZI na Mhariri wa magazeti ya Tanzanite na Fahari yetu.

Tutaendelea kuwajuza.

======

UPDATES; 1445HRS

MAXENCE MELO AACHIWA BAADA YA KUHOJIWA NA OFISI YA DCI KWA SAA NNE

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo ameachiwa bila masharti yoyote na Ofisi ya DCI baada ya kuhojiwa juu ya tuhuma zilizotolewa na magazeti ya Fahari Yetu na Tanzanite kuwa anashirikiana na Polisi, TCRA, Bernard Membe, Balozi Emmanuel Nchimbi, Kanali Iddi Kipingu na Wakili Jonathan Mndeme kupanga njama za kumuua Ndg. Cyprian Musiba. Maxence amekuwa mtu wa kwanza kuhojiwa saa chache baada ya gazeti kutoa habari hizo.

Amehojiwa kwa Saa Nne.

Dar es Salaam
11.07.2019

Zaidi, soma Tuhuma za mauaji: Nimehojiwa na Polisi, nimetimiza wajibu wangu


IMG_20190711_132040_578.jpg
IMG_20190711_132045_835.jpg
 
Ajabu kabisa!!!

Musiba mbona haojiwi kwa tuhuma anazotoa dhidi ya watu wengine?!

Mpaka hapa watu mnahitaji ushahidi gani kujua ni nani yuko nyuma ya Musiba?

Kuhusu Mello,kwa mtazamo wangu, huenda JF ndio chanzo cha yote haya na sasa wanamtafutia sababu tu.

Maajabu ni pale mtuhumiwa mmojawapo(Jeshi la Polisi/Polisi) kuwa ndio mchunguzi kwa maana ya mtuhumiwa anajichunguza!!!

Vituko Bongo haviishi!!!!!

Last but not least,Melo,unaweza kuwashinda watu hawa mahakamani, lakini kamwe usifikiri huo ndio utakuwa mwisho wa mchezo.

Kuanzia sasa kuwa makini kuliko wakati wowote ule.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom