Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, ahojiwa kwa tuhuma za kula njama za kutaka kumuua Cyprian Musiba

Tiisii ya sasa ni mizinguo sana. Yan badala kuwa tumia watu wa maana wanamtumia huyo andazi Musiba.
 
Yaani yeye visa vya wengine kutekwa, kupigwa risasi n.k ndiye kinara wa kukanusha kwamba sio kweli, cha ajabu yeye kalalamika tu gazetini Watu wameanza kuhojiwa.
 
Mbona wanamsakama sana Max jamani au kuna agenda nyingine tusiyoijua?pole sana Max na hili litapita.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anahojiwa na ofisi ya Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai ( DCI) Jijini Dar Es Salaam muda huu.

Maxence anahojiwa muda mchache baada ya magazeti ya leo ya Tanzanite na Fahari Yetu kuandika kwamba Maxcence Melo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, TCRA, Balozi Emmanuel Nchimbi na Benard Membe wanapanga njama za kumuua Cyprian Musiba.

Maxence anahojiwa chini ya wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Jones Sendodo.

Mbali na Maxence Melo, Magazeti ya Tanzanite na Fahari yetu, yamedai kwamba Mkakati huo wa kumuua Musiba unapangwa pia na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Watumishi wa Jeshi la Polisi Nchini na Kigogo wa CCM.

Wengine walio kwenye mkakati huo wa kutaka kumuua Musiba ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil Dkt. Emmanuel Nchimbi, Benard Membe, Ofisi ya DDP, Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Kipingu.

Magazeti hayo yamedai watumishi wa TCRA wamefunga account za Mitandao ya Kijamii ya Musiba na kufuatilia Mawasiliano yake.

Gazeti hilo limedai pia kwamba watu hao wanajipanga kifungua kesi nne, Mbili mahakama kuu na mbili mahakama ya Kisutu. Mbali na kesi pia kwamba wana mpango wa kuondoa uhai wake.

Pia Magezeti hayo yamedai kwamba hili Genge linalotaka kumtoa uhai wake, lilikuwa na mkakati wa kuhakikisha wanamuondoa rais Magufuli kupitia baadhi ya wajumbe wanaoingia katika mkutano mkuu wa CCM (NEC) na Kamati kuu(CC), ili asiweze kuendelea na kipindi chake cha pili cha Urais.

Cyprian Majura Musiba ambaye alikuwa Mtangazaji wa zamani wa runinga ya Channel Ten na radio ya Magic FM, ni Mkurugenzi wa kampuni ya CZI na Mhariri wa magazeti ya Tanzanite na Fahari yetu.

Tutaendelea kuwajuza.

======

UPDATES; 1445HRS

MAXCENCE MELO AACHIWA BAADA YA KUHOJIWA NA OFISI YA DCI KWA SAA NNE

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo ameachiwa bila masharti yoyote na Ofisi ya DCI baada ya kuhojiwa juu ya tuhuma zilizotolewa na magazeti ya Fahari Yetu na Tanzanite kuwa anashirikiana na Polisi, TCRA, Bernard Membe, Balozi Emmanuel Nchimbi, Kanali Iddi Kipingu na Wakili Jonathan Mndeme kupanga njama za kumuua Ndg. Cyprian Musiba. Maxcence amekuwa mtu wa kwanza kuhojiwa saa chache baada ya gazeti kutoa habari hizo.

Amehojiwa kwa Masaa Manne.

Dar es Salaam
11.07.2019


View attachment 1151111View attachment 1151112
Hii nchi bhana juzi juzi tu JPM ametoka kulalamikia magazeti kwamba baada ya kuandika habari za Serengeti National Park kupewa tuzo wakaandika habari za kubaka.. Kwenye hili gazeti leo habari za uwekezaji za Pm zimewekwa chini tena kwa maandishi madogo halafu habari za mbakaji wa habari Cyprian Musiba zimepewa kipaumbele. Zilongwa mbali zitendwa mbali
 
KUNA MTU ANAPENDA SANA HADITHI ZA AINA HII NA KUNA WALIOMJULIA WANAKULA TU HELA ZA KODI ZETU, WAITARA ALIJIPATIA CHEO KIRAHISI SANA ALIPO CLAIM HUKO KUNAKO KWAMBA MBOWE ANATAKA KUMUUA.
 
Haya ni maajabu, kuwa washirika wake Maxence Melo ni Jeshi la Polisi, TCRA, Balozi Emmanuel Nchimbi na Benard Membe.

Ngoja tuone upande wa Cyprian Musiba mashahidi wake ni kina nani.
Yaani Musiba hata hahangaiki, Jamhuri ndio inafungua mashtaka! Wengine wakituhumiwa au kuchafuliwa, wanaambiwa NENDA MAHAKAMANI. Ila Musiba akiwatuhumu wengine, mara moja wanahojiwa!! Jamani Mungu anawaoneni, Ohooo, yaani mnajisahau hivyo?
 
Back
Top Bottom