Maxence Melo (Mac): A Vote of Confidence

Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
7,458
8,521
MoDs:
Kwa heshima na taadhima ninaomba mniruhusu kutumia ukumbi huu, japo hata kwa muda mfupi tu kumzungumzia ndugu yetu Mac na mchango wake mkubwa anaoufanya kimya kimya hapa JF.

Wengi wetu tunaoishia hapa kwenye 'ukumbi wa siasa' inawezekana kabisa tusiwe na habari na kazi mhimu anayoifanya, tena kwa ufanisi mkubwa ndugu huyu katika jamvi lile la "Nafasi za Kazi (Vacancies)." Ameifanya kazi ile kwa 'dedication' ya hali ya juu sana, kiasi kwamba utadhani labda ni mwajiriwa.

Kwa wale wenzetu ambao bado wamo kwenye pilkapilka za kutafuta kazi, au mmo mbioni kubadili kazi, tambueni kuwa huduma hiyo ipo hapa na inafanyika kwa ufanisi mkubwa. Tembeleeni huko mara kwa mara.

La kushangaza ni kwamba sijawahi kumsikia Mac akiingia kwenye ukumbi huu wa siasa, lakini huwezi kumkosa kwenye nafasi za kazi.
Heko Mac, kwa kazi yako nzuri, na mafanikio yako yaongezeke 2008.
 
hata miye namuunga mkono.. anatusaidia sana kujua wapi pa kukimbilia "kikiota nyasi"... keep up the good work!
 
Hata mimi nimepata kazi serikalini kwa kusoma matangazo ya huyu bwana. Hongera sana. maana kwa sasa najiandaa kuwa fisadi. Kule nilikokuwa nisingeweza kuwa fisadi!

Hongera Max, nitakukumbuka katika ufalme wangu!
 
Hongera sana MAc. Anatufundisha tuwe na moyo wa kujitolea bila kuangalia tunanufaika na nini. Mungu akuzidishie pale ulipopungukiwa.
 
FD ulipataje hiyo kazi serikalini wakati Ghasia na circular yake ndio inatamba sasa hivi???............ama kweli ndg yangu umeshakuwa kafisadi fulani (joke)
 
Kalamu hapo kwa kweli umegonga panako penye..... Mac, kazi yako kwa kweli ni nzuri na imesha na inaendelea kutusaidia wana jamii wote.... Keep up the good work ndugu yangu!!!
 
Mac , Tuko wote mzee. Tunajali sana kazi unayoifanya.
FD .. kama alivyouliza Ogah .. sema Mzee imekuwaje ..? au ilikuwa kabla ya circular ya ghasia?
 
kuna watu wanajituma mpaka unashangaa. Bila kulazimishwa wala kulipwa. Hongera sana ndugu yangu.

Tusimsahau pia brazamen kule kwenye mambo ya kikubwa, naye anajituma sana, tumpongeze pia. teh teh
 
Brazameni anaelewa kwamba tunautambua mchango wake .. na kuuthamini, kiasi kwamba akienda likizo kidogo inabidi tuanze kufuatilia ana matatizo gani. Kam kipindi hiki katuacha solemba.....
 
kuna watu wanajituma mpaka unashangaa. Bila kulazimishwa wala kulipwa. Hongera sana ndugu yangu.

Tusimsahau pia brazamen kule kwenye mambo ya kikubwa, naye anajituma sana, tumpongeze pia. teh teh

Lo! Sasa unaharibu... (Just kidding)

Kudos Mac
 
Mac anatuonyesha mfano mzuri hapa JF; kuwa tunao watu ambao hujali maendeleo ya wenzao pia bila kujali kujinufaisha kwao binafsi. Ni mfano unaofaa kuigwa.
 
FD ulipataje hiyo kazi serikalini wakati Ghasia na circular yake ndio inatamba sasa hivi???............ama kweli ndg yangu umeshakuwa kafisadi fulani (joke)

Mkuu Ogah,

Kweli nimeanza kuwa FISADI sio uongo. Ila mimi nafanya ufisadi kwa kuangalia opportunities zilizopo na kuzifanyia kazi!, nimeweka miradi ya maana kwa kutumia cheo changu!. Yap! nifanyeje, mie siwaibii nyinyi hata kidogo.

Karibu tule sehemu yetu!
 
Mac , Tuko wote mzee. Tunajali sana kazi unayoifanya.
FD .. kama alivyouliza Ogah .. sema Mzee imekuwaje ..? au ilikuwa kabla ya circular ya ghasia?

Misterdennis,

Kabla ya hapo. Siku hizi ukianza kuandaa watoto wako waje wawatawale watoto wao inabidi uwe na hela. Kupata hela inabidi UIBE au uwe na miradi ambayo unapata tenda kwa kutumia jina lako. Watu wanapeana bongo.

Hope umeelewa.

Fisadi Daima
 
FD, Nimekupata mzee .... Zikiwa nyingi (tenda) and your hands are full, tuambiane mzee ili tunufaike wote.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom