MoDs:
Kwa heshima na taadhima ninaomba mniruhusu kutumia ukumbi huu, japo hata kwa muda mfupi tu kumzungumzia ndugu yetu Mac na mchango wake mkubwa anaoufanya kimya kimya hapa JF.
Wengi wetu tunaoishia hapa kwenye 'ukumbi wa siasa' inawezekana kabisa tusiwe na habari na kazi mhimu anayoifanya, tena kwa ufanisi mkubwa ndugu huyu katika jamvi lile la "Nafasi za Kazi (Vacancies)." Ameifanya kazi ile kwa 'dedication' ya hali ya juu sana, kiasi kwamba utadhani labda ni mwajiriwa.
Kwa wale wenzetu ambao bado wamo kwenye pilkapilka za kutafuta kazi, au mmo mbioni kubadili kazi, tambueni kuwa huduma hiyo ipo hapa na inafanyika kwa ufanisi mkubwa. Tembeleeni huko mara kwa mara.
La kushangaza ni kwamba sijawahi kumsikia Mac akiingia kwenye ukumbi huu wa siasa, lakini huwezi kumkosa kwenye nafasi za kazi.
Heko Mac, kwa kazi yako nzuri, na mafanikio yako yaongezeke 2008.