Maxence Melo: JamiiForums imefanikiwa kujenga Fikra Mbadala kwa watanzania wengi

Mkuu mimi nakupongeza kwa unachofanya si haba ila angalia upande huohuo wa kufuta nyuzi , Kuna kitu mimi inanitatiza hasahasa jukwaa la siasa ambapo waanzisha mada wanakuwa walewale siku zote Ina maana hamna wengine wenye mawazo mbadala was kuanzisha nyuzi ? Au ndio zinazofutwa ? Mimi namshauri kwa kuwa JF Kuna watu wa aina mbalimbali na weledi mbalimbali watu wengine pia mada zao ziachiliwe zisifutwe tupate , mawazo ,elimu ,teknolojia ,ujuzi , maarifa , mwelekeo kutoka kwa watu tofauti tofauti , sio kila siku mada za akina johnthebaptist , Mayala , ninachosema wadau wengi wapewe nafasi kuanzisha mada tupate maarifa mapya , sio kila siku walewale Tena wanna mwelekeo wa Lumumba , mimi mwenyewe mada zangu nyingi sana hufutwa sawa Kama Kuna mapungufu zifuatwe sikatai lakini inatia shaka , wakati wa Jiwe mada nyingi zilifutwa na Sasa pia pia , hivi na awamu bado ni tishio kwenu . Kuna siku nilioosti kuhusu ajira 6000+ nikaweka attachment ya ilani ya CCM kuzalisha ajira milioni saba ikafutwa shida nini? Mnatishwa vizuri na sisi members tujue , lakini naomba watu wengi wafunguke nyuzi nyingi ziachwe hewani ili tujue mengi, tujifunze mengi kutoka kwa wenzetu sio kila siku walewale . Mimi nimejifunza mengi sana hapa JF ndio napenda watu wengi wapate tupate mengi pia , mawazo yangu tu hayo samahani kama nitakuwa nimekukwaza .
Chief Kabikula, sidhani kama tatizo ni kufutwa kwa nyuzi. Ninaweza kujenga hoja kwamba wale waliokuwa wakitoa nyunzi zenye mashiko wali-withdraw!

Sijasikiliza mahojiano hayo ya Bw Melo, lakini hata bila kusikiliza huyu ndugu ni mmojawapo ya mashujaa wa zama hizi! Hongera sana Bw Melo.

Kwa mfano, JF ndio jukwaa pekee au mojawapo ya majukwaa machache yaliyoendelea kutoa nafasi kwa wadau kuelezea fikira zao kwa kiasi fulani cha uhuru wakati wa enzi za "New Stone Age" (enzi za Shujaa wa Afrika).

Lakini hata kabla ya zama za "New Stone Age", wadau wengi waliokuwa wakibandika mada fikirishi au kuchangia mada fikirishi walikuwa wameishaanza kukaa pembeni na kubakia ku-peruzi tu. Mtakumbuka hata baadhi ya vigogo walijiunga kwa utambulisho wao halisi (mfano Mama Prof Tibaijuka, Mwigulu Mchemba, nk). Sababu kubwa iliyochangia wadau wenye fikira pevu kukaa pembeni na kuwa wasomaji tu, ni baada ya Lumumba kufungulia jeshi ya Lumumba Buku 7 Club! Hawa walivamia jukwaa kweli kweli kiasi cha kugeuza JF-Siasa kuwa jukwaa la matusi na utoto.

Kuna watu hata kama wanatumia IDs fake lakini conscience zao zinawazuia kuwa sehemu ya mijadala ya kitoto! Kwa maneno mengine ile hadhi ya JF kwa kiasi fulani ilishushwa na mkakati wa watawala kwa kufungulia jeshi lao kugeuza mijadala fikirishi kuwa mipasho ya uswahilini.

Kimkakati, watawala walifanikiwa sana.
 
Hongera sana Melo! Swali langu ni je, siku Melo hayupo,JamiiForums itaendelea kusimama?

Kwa maneno mengine,Melo umeandaa au unaandaa mbadala wako?

Nasema hivi kwasababu, ili legacy yako ya kuanzisha JamiiForums idumu, itakuwa ni pale tu ambapo JamiiForums itaendelea kuwepo na kusimama imara uwepo au usiwepo.
 
Aki
Hongera sana Melo! Swali langu ni je, siku Melo hayupo,JamiiForums itaendelea kusimama?

Kwa maneno mengine,Melo umeandaa au unaandaa mbadala wako?

Nasema hivi kwasababu, ili legacy yako ya kuanzisha JamiiForums idumu, itakuwa ni pale tu ambapo JamiiForums itaendelea kuwepo na kusimama imara uwepo au usiwepo
Akikujibu nitag
 
Miaka 10 ya mafanikio hongera sana Jf... labda kuna kitu gani kipya sasa tutarajie huko mbele..maono mapya..Pia swali kwa Jf je imefanikiwa kufikisha ujumbe kwa vijana mashuleni na vyuoni ili nao wawe wabunifu kama jamii forum?au huu ugunduzi wa max unaonekana kwa vijana nao wakaweza kufanya kitu sio lazima kifanane na jf hata kwenye fani zingine pia na hii yote ni katika kulikomboa taifa letu litoke kwenye umaskini huu hasa vijijini.
 
Back
Top Bottom