Maxence: Ahsante Mungu, ahsante watanzania!


Status
Not open for further replies.
Maxence Melo

Maxence Melo

JF Founder
Staff member
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,815
Likes
3,671
Points
280
Maxence Melo

Maxence Melo

JF Founder
Staff member
Joined Feb 10, 2006
2,815 3,671 280
Wana JF,

Kwanza namshukuru Mungu kwa kutupa fursa ya kuishi tena (2nd chance) mimi na mdogo wangu. Mungu yu mwema kwetu.

Katika ajali hii, huwezi kutarajia kuwa tumetoka tukiwa hai na tunaendelea vema kama tulivyo sasa.


Aidha, nawashukuru wote waliotoa pole zao kwetu via JF na kututakia kupona haraka. Tunashukuru sana na tunazidi kufarijika kwa ushirikiano wenu katika maombi (na baadhi walituma michango itusaidie katika matibabu). Moderators, shukrani kwa kuendelea kulisimamia jukwaa hili kwa weledi mkubwa.

Napenda kuwashukuru wanasiasa; ndugu Zitto Kabwe, Dr. Faustine Ndugulile, Ndugu Hussein Bashe na Dr. Mary Mwanjelwa - ambao wameonyesha kujali tangu tunapata ajali hadi sasa (wanatujulia hali tunavyoendelea); hii inatia moyo na kuonyesha kujali kwao kwetu. Mungu awazidishie muendelee kuwa na moyo huu.

Shukrani zetu ziende kwa wana JF wa Nzega, Mwanza na Dar; ambao wamekuwa nasi bega kwa bega tangu siku ya ajali. Ni wengi lakini inakuwa vigumu kuwataja kwenye shukrani zetu hizi bali tunapenda wafahamu kuwa tunawashukuru sana.

Tunawashukuru sana wengine wote ambao kwa njia tofauti wamekuwa wakitaka kujua tunaendeleaje kiafya na kuwajuza hapa; kutokana na mazingira tulikuwa tunashindwa kuwajibu wote lakini wengi tumewajibu kuwafahamisha kilichotokea na tunavyoendelea.

Ndugu zangu, tupo hai kwa mapenzi ya Mungu tu!

Nini kilitokea?
Inakuwa vigumu kuelezea kwa kirefu kilichotokea. Kuwa ni mwendo kasi? Sijui. Kuwa ni mkono wa mtu? Pia sijui. Kuwa ni bahati mbaya? Naweza kusema hivyo! Hatumlaumu yeyote katika hili na hatumnyooshei kidole yeyote. Kwa dereva yeyote anafahamu nini kinaweza kutokea pale 'Steering Rod' inapokatika ukiwa katika mwendo zaidi ya spidi 80.

Yapo mengi yanaweza kuhisiwa, yapo mengi yanaweza kusemwa lakini ambacho tunaweza kukiri ni kuwa Mungu yu mwema kwetu.

Hali yetu:
Baada ya ajali, mdogo wangu ambaye pia ni member wa JF kama Chachu Ombara, alibainika kuvunjika mfupa wa kati ya kiwiko na bega mkono wa kushoto na sasa amefanyiwa upasuaji na madaktari bingwa Muhimbili, anaendelea vema.

Binafsi nilibainika kuwa na uvimbe kidogo kwenye ubongo upande wa kulia; naendelea vema namshukuru Mungu.

Mwisho:
Ushauri wangu kwa wanaoendesha magari, wasafiri kwenye ruti ndefu na hata katika hali ya kawaida:
- Kabla ya safari yoyote mwite Mungu na ujikabidhi kwake, atakuitikia kwa namna ya kipekee
- Unapoendesha, funga mkanda. Hata kama umekaa siti ya nyuma (katika gari binafsi).
- Ukiwa barabarani (dereva), jitahidi kuzingatia alama za barabarani; wajali madereva wengine kama ambavyo ungependa wakujali.

Nasikitika kuwa huenda nisijibu maswali ambayo labda yanaweza kujitokeza kutokana na kuwa nina matatizo ya kuumwa kichwa (kilijigonga sana chini wakati gari linapinduka) lakini naamini nikikaa vema nitarejea na aidha kujibu au nikiwa nimechelewa nitatuma PM kwa mhusika.

Asanteni sana.

Maxence

-----> Toka kwa Moderator<----------​

=================== (Angalizo)

Tokana na maoni ya wengi ya wadau wa Jukwaa La Siasa kutokua na taarifa hii mbaya ya Ajali ilipokua imetangazwa hapa, mtuwie radhi Moderators kwa maamuzi ya kuhamishia habari hii Jukwaa La Siasa toka habari na hoja Mchanganyiko.

Habari hiyo ya ajali ilipostiwa hapa na inapatikana kwenye kiunganisho hiki kilicho ambatanishwa - Maxence Melo apata Ajali mbaya Maeneo ya Nzega.

================= (Kuhusu Michango)

Tumefikiwa na taarifa kuwa kumekua na members wakiuliza na kuhamasisha kuwekwe taratibu za Kuchangisha pesa kama Mchango wa Kumkabidhi Maxence Melo kama njia ya kuweza kumsaidia katika wakati huu mgumu.

Kwa kutumia Uzi huu wa Max; kwa member yeyote mwenye nia ya kutuma mchango tafadhali atumie njia zilizoelezwa katika kiunganisho hiki ambatanishwa - Link. Aidha kwa wale ambao wangependa kutuma kwa E-Money mnaweza kutumia namba zifuatazo:-

Vodacom (Mpesa) - 0755 642 929
Airtel (Airtel Money) - 0784 526 444
Tigo (Tigo Pesa) - 0713 444 649
 

Attachments:

VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
5,988
Likes
7,898
Points
280
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
5,988 7,898 280
Tunamshukuru Mungu kwa ajili yako Mwanangu Maxence Melo. Uwe na afya njema na uzidi kututumikia. Be blessed my son! Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
Last edited by a moderator:
Cathode Rays

Cathode Rays

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
1,742
Likes
210
Points
160
Cathode Rays

Cathode Rays

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
1,742 210 160
Dear Maxence Melo and Chachu Ombara,

It was everybody's wishes and prayers that you recover and it is a big relief to see you here once again

Second chance in life.....Glory and honour to most higher God
 
Last edited by a moderator:
Mr Rocky

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
15,198
Likes
600
Points
280
Mr Rocky

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
15,198 600 280
Pole sana mkuu Maxence Melo na Chachu Ombara. Mungu yupo upande wenu na atawajalia uponaji mwema muweze kurudi kwenye majukumu ya kawaida. Poleni sana wakuu na sifa na utukufu anastahili Mungu pekee
 
Last edited by a moderator:
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
10,441
Likes
1,399
Points
280
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
10,441 1,399 280
Mungu yu mwema, tunamshukuru kwa ukarimu wake wa kutuwekea hai wewe na mdogo wako! tutazidi kushukuru tena na tena!
 
Ablessed

Ablessed

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2013
Messages
4,620
Likes
120
Points
145
Ablessed

Ablessed

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2013
4,620 120 145
Aisee ilikua ajali kubwa sana jamani yaani gari limeharibika kiasi hiki hata huwezi amini kama kuna aliyetoka hai humo. Kweli Mungu ni mwema na lizidi kuinuliwa jina lake. Hongera sana kwa kupata second chance ya kuishi . Nimestuka sana kuiona gari iko hivi. Ama kweli Mungu ni mkubwa, nakuombea tu upone kabisa na urudi ktk afya yako ya mwanzo.
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,850
Likes
3,632
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,850 3,632 280
Maxence Melo and Chachu Ombara,
Mungu aendelee kuwaponya na kuwarudishia afya ya awali...
Pamoja!!
 
Last edited by a moderator:
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
8,679
Likes
5,731
Points
280
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
8,679 5,731 280
Nimefarijika sana kusikia kutoka kwenu! Na la kufurahisha kabisa ni kuwa mna mtanguliza Mungu mbele! Basi Mungu azidi kuwatangulia na kuwapa maisha marefu!
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,273,856
Members 490,528
Posts 30,493,607