Mantombazane
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 579
- 367
Mimi ni wakala wa Maxmalipo na Selcom. Kusema kweli huduma za Maxmalipo zimekuwa ni hafifu na dhaifu sana ukilinganisha na Selcom. Mfano unapo nunua umeme kwa njia ya Selcom hadi raha. Ukiandika namba ya mita na kiasi mashine inakuletea kwanza taarifa za mteja ikiwemo jina, namba ya mita na kiasi ulichotaka. Ukiona ni sahihi unakubali na kuweka namba ya simu kisha namba yako ya siri na muda sio mrefu risiti inatoka na wakati huo huo sms inaingia kwenye namba ya simu uliuoiandika. Hii inasaidia hata kama mteja yuko mbali au amepoteza risiti.
Ukija Maxmalipo kusema kweli ni shida. Hawakupi taarifa za mteja, hawatumi sms lakini pia inachukua muda mrefu sana kusubiri muamala mmoja ni kama mtandao wao uko very slow. Mara nyingi nimejaribu kuwakumbusha kwa simu na kupitia ukurasa wao wa FB lakini sioni mabadiliko. Kusema kweli wao wana huduma nyingi kuliko wenzao lakini inaonekana wamejitanua sana wakasahau kuboresha huduma. Kama wakala naandika haya siyo kwaajili ya kuwapigia debe Selcom ila nawakumbusha na wao kwani wote nawahitaji. Zamani walipoanza walikuwa vizuri sana. Ukifanya muamala wa umeme wanatuma na sms kwenye simu lakini sasa kwakweli huduma hiyo hakuna tena sijui wamezidiwa?!.
Jingine ni kuwa ukipata tatizo la mashine ukienda ofisini kwao kwakweli wanasumbua sana ni kama vile wana fundi mmoja tu. Unakuta wakala analazimika kwenda kwao zaidi ya mara mbili kufuatilia huduma za kiufundi.Ukienda kufuatilia mabango ya matangazo kila mara hawana mpaka tunaingia gharama za kulipa watu watuangikie mabango ya matangazo. Hii ni tofauti na Selcom. Nawaomba Selcom wasije wakalewa sifa wakaanza kufanya makosa wanayofanya wenzao. Kinachokera Maxmalipo ni kuwa hawasikii na wala hawajali tunapotoa maoni na malalamiko. Badilikeni jamani ulimwengu huu wa sasa sio wa kusubiri.
Mnisamehe bure kwa kuwakera lakini ninataka biashara iwe rahisi kwasababu tumetumia gharama kubwa kuwa mawakala hivyo tunahitaji kufanya biashara kurudisha gharama na faida.