Mawimbi Ya Redio Ya Ajabu Kutoka Anga Za Juu Yagunduliwa

Yaani kutokana na jina unalotumia hapa Jf nikajua unayajua haya mambo lakini niliposoma changisho lako nimechoka lol. Kama kitu huna knowledge nacho ni vyema kuuliza ukaelekezwa kuliko kubisha. Kuna kitu kinaitwa light years; tunapima umbali wa nyota tokea tulipo ( duniani) kwa kasi ya mwanga. Utakapohitaji ufafanuzi zaidi uliza

Sent using Jamii Forums mobile app
naomba nielekeze kuhusu light years

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kha!!! Sasa kama wamefanya vingi ndio watuletee upuuzi kama huu tuukubali!!? Wakeup hivi unajua miaka 1.5b au tunachekeshana tu!? Kama hunielewi ni bora ukaacha ku quote comments zangu. Ni bora ukabaki na low thinking yako.

Unaambiwa 1.5b year kwa speed ya mwanga. Hivi unajua speed ya light!?
Speed ya light ni 300,000km/s.
Sasa zidisha kwa hiyo miaka 1.5b.
Kama siyo kutishana tu ni nini.
Mara wanakuambia Aliens mara Nibiru nk.
Huu ni uongo watu wenye akili tunajua.
Ni hila za mabeberu.Tupo katika vita vya kiuchumi.Watanzania tusitishwe!
 
Mawimbi ya redio ya ajabu kutoka anga za juu yagunduliwa na darubini Canada

Source: Mawimbi ya redio ya ajabu kutoka anga za juu yagunduliwa

Wataalamu wa anga za juu wamefichua kwamba walinasa mawimbi ya redio ya ajabu ambayo yalikuwa yanatoka mbali sana katika anga za juu.

Mawimbi hayo yalinaswa na darubini ya kufuatilia mawimbi ya redio ambayo ipo Canada na yanaaminika kutoka kwenye mfumo wa nyota na sayari ulio mbali sana.

Chanzo halisi cha mawimbi hayo ya redio bado hakijabainika na wala wataalamu hao hawajafahamu sifa kamili za mawimbi hayo.

Miongoni mwa mawimbi hayo ya redio ya kasi sana (yanayofahamika pia kama FRBs kwa maana ya Fast Radio Bursts), ambayo yalinaswa mara 13, kulikuwa na mawimbi yasiyo ya kawaida yaliyokuwa yakijirudia tena na tena. Yanaaminika kutoka kwenye chanzo kimoja umbali wa takriban miaka 1.5 bilioni kwa miaka ya kasi ya mwanga.

Tukio kama hilo limewahi tu kuripotiwa mara moja tu awali, na darubini tofauti.

"Kufahamu kwamba kuna nyingine imepatikana ni jambo linalodokeza kwamba kunaweza kuwa hata na zaidi," amesema Ingrid Stairs, ambaye ni mtaalamu wa fizikia ya anga za juu katika Chuo Kikuu cha British Columbia (UBC).

"Na tukiwa na mitambo zaidi ya kuimarisha nguvu za mawimbi hayo na pia vyanzo vingi, basi tunaweza tukafahamu na kutanzua kitendawili hiki cha anga za juu - tujue mawimbi haya yanatokea wapi na nini chanzo chake."

Kituo cha kutafiti anga za juu cha CHIME, kinachopatikana katika Bonde la Okanagan katika eneo la British Columbia, kina antena nne (waya maalum za kupokelea mawimbi ya sauti) za urefu wa mita 100 ambazo hufuatilia anga ya kaskazini kila siku.

Darubini iliyotumiwa ilianza tu kufanya kazi mwaka jana, na iliyanasa mawimbi hayo 13 ya redio karibu mara moja, pamoja na mawimbi hay ya kujirudia.

"Tumegundua mawimbi ya pili yanayojirudia ambayo yanafanana na yale ya kwanza," Shriharsh Tendulkar wa Chuo Kikuu cha McGill, Canada amesema.

"Hili linatufahamisha zaidi kuhusu sifa za mawimbi haya ya kujirudia yakiwa kama kundi."

FRBs ni mawimbi mafupi, yenye nguvu sana ya redio ambayo yanaonekana kana kwamba yanatokea katikati ya mwendo nusu wa umbali wote wa vitu vyote vilivyopo (nyota na sayari na anga) kwa makadirio ya wanasayansi.



Kufikia sasa, wanasayansi wamegundua mawimbi takriban 60 ya redio ya pekee yanayokwenda kwa kasi sana, na mawimbi mara mbili yanayojirudia.

Wanaamini kwamba kunaweza kuwa na mawimbi ya redio ya FRBs maelfu yanayopita angani kila siku.

Mawimbi haya yanatolewa na viumbe wa anga za juu?
Kuna nadharia kadha kuhusu nini huenda kikawa chanzo cha mawimbi haya.

Moja ni kwamba huenda kukawa na nyota ya nutroni ambayo ina nguvu nyingi sana za sumaku na ambayo inazunguka yenyewe kwa kasi sana. Nyota za nutroni ni kitu kwenye anga za juu ambacho si kikubwa sana (nusu kipenyo chake ni kilomita 30 hivi) na kina uzani wa juu sana, na kimeundwa na nutroni (neutron) ambazo zimebanana sana).

Kuna baadhi ya watu, ingawa wachache, ambao wanasema kuna uwezekano mawimbi hayo yakawa yanatokana na chombo cha anga za juu pengine kutoka kwa viumbe wanaoishi anga za juu, au mawimbi yenyewe yawe ni chombo hicho cha anga za juu.
 
mkuu naomba nielekeze kuhusu light stars

Sent using Jamii Forums mobile app
Ingawa ni mada ndefu kidogo ila nitafupisha ili tuwape nafasi ma wajuzi wengine watoe michango yao. Kwanza tambua kuwa kuna billions of stars katika universe ambazo zinatoa electromagnetic radiations na mwanga. Kwa jicho LA kawaida tu bila msaada wa darubini tunaweza kuziona nyota zaidi ya 6000 juu ya uso wa dunia ambazo zinatoa hizo nguvu nilizozisema hapo juu.
Mwanga huu husafiri umbali mkubwa sana na unafika duniani just as a tiny friction of light kiwango kidogo sana. Kiasi cha mwanga uzalishwao na nyota inategemea na hali joto ya nyota yenyewe (temperature of the star). Kwa mfano nyota ambazo zimepowa (cooler stars) huzalisha mwanga unaoonekana ni mwekundu. Na zile ambazo zina joto kali (hotter stars) huzalisha mwanga unaoonekana wa blue au mweupe na unasafiri umbali mkubwa sana kwenye high frequency. Na nyota hizi huonekana kwa urahisi hata zikiwa mbali tofauti na hizo zinazozalisha mwanga wenye rangi tofauti tofauti.
Kiufupi nyota kubwa hutoa kiwango kikubwa cha mwanga kuliko zingine
Nadhani nimejaribu kukujibu kutokana na swari lako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu weka hapa ulichowahi kugundua tupime hiyo akili yako. Nijuavyo mimi mtu anayekula ugali hana akili.
Duh! Ha ha ha! Ugali utangazwe kitu hatari kwa maendeleo ya ubongo and therefore, taifa.
 
naomba nielekeze kuhusu light years

Sent using Jamii Forums mobile app
Light years ni symbol au unit inayotumika kupima umbali ambao mwanga unasafiri katika utupu ndani ya mwaka mmoja. Wanasayansi hutumia kasi ya mwanga kwa mwaka (light years away) kupima umbali wa sayari na nyota (all space objects) tokea hapa duniani
Wanatumia kipimo hiki kwasababu nyota na sayari zipo katika umbali mkubwa sana na huchukua muda mrefu kwa mwanga uzalishwao ktk nyota hizo kutufikia.
Mwanga husafiri kwa umbali wa 300,000km kwa sekunde (300,000km/s) au 9 Trillion km kwa mwaka. Kwahiyo tunapotumia very powerful telescopes kuziangalia nyota na sayari zilizombali maana ake tunaziona katika muda uliopita (Actually We are looking back in time).
Kwa mfano; jua letu ndio nyota iliyokaribu sana na dunia na nyota hii ipo umbali wa 93 million miles away from the earth. Na mwanga wake huchukua dakika 8 kutufikia. Kwahiyo unapoliangalia jua sasa hivi jua kuwa hivyo ndivyo lilivyokuwa dakika 8 zilizopita (Au huo mwanga unaokufikia sasa hivi umezalishwa na jua dakika 8 zilizopita).
Nyota hupatikana katika magrupu yanayoitwa Galaxy na galaxy iliyokaribu kabisa nasi inaitwa Andromeda na ipo katika umbali wa 2.5millions light years away. Kwahiyo tunaiona galaxy hii ilivyo kwa miaka 2.5 Millions iliyopita.
Nadhani nimekuelewesha na kukuongezea kitu mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kha!! Huoni sababu hapo nimeweka!!? Mtu anakuambia eti source ya mawimbi hayo mpaka kuja kutufikia ni miaka 1.5billion. Huoni huu ni upuuzi na ujinga wa hali ya juu!? Hivi billion unaijua wewe kweli!?
Sekunde 1.5b ni sawa na miaka 1141.5525114.
Waache propaganda zao za kizamani.
Malizia 1.5 Billion light years sir!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ukweli ni kuwa tusijidai kuwa eti sayari dunia hii tuliomo ndo sisi viumbe hai huenda huko kwenye sayari zingine kibao kuna vuimbe hai na ambapo kutufikia au kuwafikia ni vigumu.uwezo wetu unagota mahali fulani.Mungu yupo
 
Hapa ukweli ni kuwa tusijidai kuwa eti sayari dunia hii tuliomo ndo sisi viumbe hai huenda huko kwenye sayari zingine kibao kuna vuimbe hai na ambapo kutufikia au kuwafikia ni vigumu.uwezo wetu unagota mahali fulani.Mungu yupo
Hili lipo wazi mkuu na hata vitabu vya dini vinadhihilisha hili. Biblia inaposema "Na Mungu akamshusha chini pamoja na malaika waasi theruthi moja" maana ake kuwa kuna sehemu walikuwepo hao malaika waasi.
Haya ma space objects kwa jina jingine yanaitwa the heaven bodies na haya majiumbo yote yanapatikana ndani ya kitu kinachoitwa the Universe. The universe comprises of millions of galaxies and still expands. Ndani ya hizo galaxies kuna mabilion ya nyota na hizo nyota zinazungukwa na quintillions of planets. JE WADHANI VIUMBE VIPO KWENYE SAYARI IITWAYO DUNIA TU?
Sisi binadamu ni carbonic beings na kuna viumbe vyenye mifumo yao mingine ya kuconsume energy ambao sisi binadamu atufahamu na ndio hao tunawaita kiujumla kama Aliens.
So kuwepo kwa spiritual beings ambao ndio Angels na majini ni ushuhuda tosha kuwa there is an intelligence out there some where in the universe.
Wacha niishie hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Physics ndio somo pekee ambalo wagunduzi wake walikuwa wanauwawa na watawala enzi hizo kumbuka akina Galilei Galileo. Zile formula walizotoa miaka mingi iliyopita ndiyo ulikuwa unafeli shuleni baada ya mwalimu wako failure kukufundisha bila kudirive formula. Be careful concerning physics.

Science haidanganyi watu wanakesha maabara wewe unakesha kusikiliza propaganda za wanasiasa.
 
Kha!!! Sasa kama wamefanya vingi ndio watuletee upuuzi kama huu tuukubali!!? Wakeup hivi unajua miaka 1.5b au tunachekeshana tu!? Kama hunielewi ni bora ukaacha ku quote comments zangu. Ni bora ukabaki na low thinking yako.

Unaambiwa 1.5b year kwa speed ya mwanga. Hivi unajua speed ya light!?
Speed ya light ni 300,000km/s.
Sasa zidisha kwa hiyo miaka 1.5b.
Kama siyo kutishana tu ni nini.
Mara wanakuambia Aliens mara Nibiru nk.
Huu ni uongo watu wenye akili tunajua.
Usiseme watu wenye akili mnajua wakati hamjaweza kugundua hata zipu ya suruali.

Wameshakuambia kuwa inaonekana ni mawimbi yanayotoka kwenye mfumo mwingine wa nyota. Na ujue kutoka umbali wa Nyota moja mpaka nyingine ni umbali mrefu kwa matrilio ya maili.
Hata kutoka Dunia hii kwenda sayari nyingine ni mamilion ya kilometres sembuse kutoka mfumo mmoja kwenda mwingine.

Wenzetu wako mbali sana kisayansi na kiteknolojia hata kama hatuwapendi.

Miaka mia moja iliyopita pangetokea mtu akawaambia watu kuwa kunauwezekano wa kuwasiliana na mtu kwa video call na kuonana nadhani huyo mtu angepigwa mawe na kuitwa ndoto za mchana.

Wazungu wana siri nzito sana kuhusu hii dunia ndio maana wanafanya tafiti nyingi sana anga za juu wakati sisi tunabaki kupinga tu bila utafiti hata ziwani.

Mfano tu Ziwa Tanganyika tunaambiwa lina kina kirefu sana na mauzauza mengi lakini hatuna wanasayansi waliofanya utafiti kujua hayo maizauza ni nani hasa na yanatokana na kitu gani!! He,kuna viumbe wengine wanaoishi huko ziwani au ni kitu gani? Watu wanaogopa kulogwa mpaka wanasayansi wa kiafrika ni waoga.Akishapata uprofesa wake anataka kula bata na familia yake.

Ni wazi kuwa kuna viumbe wengi sana huko kwenye mifumo mingine mbali na huu mfumo wa Nyota unaoitwa Jua wenye sayari Tisa kubwa.
Mifumo mingine ndiyo inayosababisha Jua na sayari zake vinaelea angani.
Nyota zote unazoziona angani ina mifumo kama lilivyo jua.

Wazungu wanajua kuwa kuna nguvu ya zaidi na ina ujuzi zaidi kuliko wanadam kisayansi ndio maana wanahangaika kutafiti huyo mtaalam mkuu ni nani na yuko wapi?

Sisi tumelala tu na kupinga bila utafiti.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawimbi kutoka anga za juu: Nadharia tano kuhusu chanzo chake

Source:Ujumbe kutoka anga za juu?

Mawimbi ya redio kutoka mifumo ya nyota na sayari iliyo mbali sana na dunia imenaswa na darubini Canada.

Mawimbi hayo ya redio yaendayo kwa kasi sana (yanayofahamika pia kama FRBs kwa maana ya Fast Radio Bursts) yanapofika kwenye darubini zilizo duniani huangaza kwa milisekunde chache, na kisha kutoweka.

Wataalamu wa anga za juu wamekuwa wakipokea na kutambua mawimbi kama hayo mara kadha katika kipindi cha miaka kumi iliyopita - na wiki hii wametangaza kugundua mawimbi zaidi.

Miongoni mwa mawimbi yaliyonaswa ni mawimbi adimu, ambayo hujirudia badala ya kuangaza mara moja pekee.

Bado haijabainika mawimbi haya hasa yanatoka wapi. Kuna nadharia tano kuu kuyahusu, ambazo tunaziangazia hapa
1. Nyota inayozunguka kwa kazi

Nyota zinapolipuka na kuangamia, masalio yake yanaweza kuwa nyota za nutroni ambazo zinazunguka kwa kasi sana.

Nyota ya nutroni huwa ni nyota ambayo ina nguvu nyingi sana za sumaku na ambayo inazunguka yenyewe kwa kasi sana. Nyota za nutroni ni kitu kwenye anga za juu ambacho si kikubwa sana (nusu kipenyo chake ni kilomita 30 hivi) na kina uzani wa juu sana, na kimeundwa na nutroni (neutron) ambazo zimebanana sana).

Wataalamu wa anga za juu wanaamini kwamba nyota hizo zinazopatikana eneo lenye nguvu nyingi za sumaku zinaweza kutoa mawimbi kama hayo ya redio.

"Kitu kama nyota ya nutroni kinalingana vyema kabisa na tukio hili kwa kweli," anasema Dkt Ingrid Stairs, ambaye ni mtaalamu wa fizikia ya anga za juu katika Chuo Kikuu cha British Columbia (UBC) mjini Vancouver, Canada.

"Lakini fizikia inayotumika ndipo kuzalishwe mawimbi haya ya kasi yenye nguvu sana ya redio ni jambo ambalo kufikia sasa hatujalifahamu."

2. Kuungana kwa nyota mbili

Tukio la kugongana kwa nyota mbili za nutroni kunaweza pia kusababisha mawimbi kama hayo.

Kwa mujibu wa Shriharsh Tendulkar ambaye ni mtaalamu wa anga za juu wa Chuo Kikuu cha McGill jijini Montreal, Canada hii ni moja ya nadharia kuu zinazotumiwa kueleza tukio hili.

Lakini hili linaeleza maana tu wakati ni mawimbi yanayotolewa mara moja tu, kwani nyota zote mbili huangamia baada ya kugongana.

"Ni tukio la maangamizi - haliwezi kueleza mawimbi ya redio ya kasi yanayojirudia," anasema.

Mengi ya mawimbi ya redio ya kasi ambayo yamenaswa na darubini katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita ni mawimbi ambayo hutokea mara moja tu na kutoweka.

Lakini kina mawimbi mara mbili ambayo yamenaswa ambayo ni tofauti - ni mawimbi ambayo yanaangaza na kujirudia mara kadha. Kwa mawimbi hayo, nadharia hii ya kuungana kwa nyota haiwezi kutumika kuyaeleza.

3. Blitzar

Blitzar ni nyota ya nutroni ambayo inazunguka yenyewe kwa kasi sana, na kwa sababu ina uzani mkubwa sana, inaporomoka yenyewe na kuacha kitu kama shimo ombwe, ambalo kwa Kiingereza huitwa 'black hole'. Tukio hilo la kuporomoka kwa nyota hiyo linaweza kuzalisha mawimbi hayo.

Pia, tukio hili mwisho wake huwa ni kuangamia kwa nyota hiyo, na kwa hivyo hilo haliwezi kutumiwa kueleza mawimbi hayo yanayojirudia.

4. 'Black hole'

Mashimbo ombwe ya anga za juu, au Black hole yametumiwa sana katika nadharia nyingi - kuanzia kwa nyota ya nutroni kutumbukia kwenye shimo ombwe la anga za juu hadi kwa shimbo lenyewe kuporomoka au kitu kisichofuata fizikia ya kawaida (dark matter) kugonga shimo kama hilo au kutumbukia eneo kama hilo.


5. Viunge wa anga za juu

Ingawa baadhi wanaamini mawimbi haya ni ya kawaida tu na yanatokana na maumbile, kuna wengine wanaoamini huenda ni ishara za shughuli ama juhudi za viumbe wengine wanaoishi maeneo mengine anga za juu.

Au pengine mawimbi yenyewe yawe ni chombo hicho cha anga za juu?

Dkt Stairs anasema uwezekano wa hili kutokea ni nadra sana.

"Mawimbi haya hutokea kote anga za juu na kutoka maeneo ya umbali tofauti - ni lazima yawe yanahusishwa na mifumo tofauti ya nyota na sayari," aliambia BBC.

"Kwa kweli, haiwezekani kwamba kunaweza kuwa na falme au himaya au jamii za viumbe wa anga za juu ambao wote wanaamua kutumia njia moja ya mawasiliano (kutuma mawimbi ya redio) - ni jambo ambalo kwa kweli uwezekano wake ni finyu mno."
 
Kha!! Huoni sababu hapo nimeweka!!? Mtu anakuambia eti source ya mawimbi hayo mpaka kuja kutufikia ni miaka 1.5billion. Huoni huu ni upuuzi na ujinga wa hali ya juu!? Hivi billion unaijua wewe kweli!?
Sekunde 1.5b ni sawa na miaka 1141.5525114.
Waache propaganda zao za kizamani.
Sio propapaganda ..iz hevenly body wanazipima wanazipima kwa Light Years ..maana yake ..walijaribu kuangalia Distance kati ya Sisi na Jua ni kilomita Milion 150 ..lakini mwanga wa Jua unachukua Dk8 tu kutufikia ..kwa iyo wakitaka kupima distannce ya Star wanatumia Kipimo cha light year distance amabayo mwanga unaweza kusafili ndan ya Mwaka ..kwa iyo Light year 1 sawasawa na 10 Trilion km
 
Usiseme watu wenye akili mnajua wakati hamjaweza kugundua hata zipu ya suruali.

Wameshakuambia kuwa inaonekana ni mawimbi yanayotoka kwenye mfumo mwingine wa nyota. Na ujue kutoka umbali wa Nyota moja mpaka nyingine ni umbali mrefu kwa matrilio ya maili.
Hata kutoka Dunia hii kwenda sayari nyingine ni mamilion ya kilometres sembuse kutoka mfumo mmoja kwenda mwingine.

Wenzetu wako mbali sana kisayansi na kiteknolojia hata kama hatuwapendi.

Miaka mia moja iliyopita pangetokea mtu akawaambia watu kuwa kunauwezekano wa kuwasiliana na mtu kwa video call na kuonana nadhani huyo mtu angepigwa mawe na kuitwa ndoto za mchana.

Wazungu wana siri nzito sana kuhusu hii dunia ndio maana wanafanya tafiti nyingi sana anga za juu wakati sisi tunabaki kupinga tu bila utafiti hata ziwani.

Mfano tu Ziwa Tanganyika tunaambiwa lina kina kirefu sana na mauzauza mengi lakini hatuna wanasayansi waliofanya utafiti kujua hayo maizauza ni nani hasa na yanatokana na kitu gani!! He,kuna viumbe wengine wanaoishi huko ziwani au ni kitu gani? Watu wanaogopa kulogwa mpaka wanasayansi wa kiafrika ni waoga.Akishapata uprofesa wake anataka kula bata na familia yake.

Ni wazi kuwa kuna viumbe wengi sana huko kwenye mifumo mingine mbali na huu mfumo wa Nyota unaoitwa Jua wenye sayari Tisa kubwa.
Mifumo mingine ndiyo inayosababisha Jua na sayari zake vinaelea angani.
Nyota zote unazoziona angani ina mifumo kama lilivyo jua.

Wazungu wanajua kuwa kuna nguvu ya zaidi na ina ujuzi zaidi kuliko wanadam kisayansi ndio maana wanahangaika kutafiti huyo mtaalam mkuu ni nani na yuko wapi?

Sisi tumelala tu na kupinga bila utafiti.


Sent using Jamii Forums mobile app
True 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom