Mawazo yenu waungwana "je, kuna uhusiano wowote kati ya kumpenda mtu kwa dhati na kukumbuka siku yake ya kuzaliwa?"

NYANGONGO

Member
Feb 14, 2013
16
17
Ndugu na marafiki zangu naombeni tubadilishane mawazo katika hili katika familia yangu hakujawahi kuwa na umuhimu wowote ule wa siku hii ya kuzaliwa, kuanzia kwa wazazi mpaka mimi na ndugu zangu.

Aghalabu hutokea hata mimi mwenyewe kukumbuka siku hii ikiwa imekwishanipita kwa wiki kadhaa tatizo ninaloliombea ushauri ni mtu ninaempenda tena sana kwa dhati ya moyo wangu anatokea katika familia ambayo siku hii ndio kila kitu.

Ninapotokea kusahau siku yake hii, anaumia sana na kufikia hata kujiuliza kama upendo wangu ni wa dhati kwake, "inawezekanaje nisahau siku yake ya kuzaliwa?" nami huishia kushangaa tu iweje imuumize kiasi hicho ikiwa hata yangu mwenyewe sikumbukagi na ni yeye ndie huwa akinikumbusha.
"Ni kweli jambo hili ni kubwa kiasi hiki, na ni kweli linapaswa kuhusianishwa na jambo zito kama "upendo wa dhati"
 
Sasa ndugu lazima uendane na situation kiukwel watu wengi hata nkiwemo mm sku yako ya kuzaliwa n lazima mpenz wako ainogeshe na kuna baadh ya watu hushindana kuwa wa kwanza kumuwish na vtu vingine sasa ndugu inabd ujifunze kutilia maanan hata kama hukufanya hvo kabla inabd ujue upo kwenye mahusiano,
 
Pole mkuu ukweli ni kuwa havina mahusiano bali ni hulka na nafasi ya kufanya hivyo kama anakwazika kwa jambo dogo hivyo ni kipimo cha baadaye cha mahusiano yenu kaa mguu nje mguu ndani jitathimini kama utammudu moyo wako uamue sasa
 
Kuna demu mmoja aliniambia vitu vidogo vidogo kama kukumbuka siku yake ya kuzaliwa ndo mapenzi yenyewe

Ile kauli mpaka leo ninayo kichwani japo me sio mfatiliaji sana wa mambo ya happy birthday ila nadhani ni kitu muhimu sana

Kwanza inaonyesha unajali
 
Back
Top Bottom