Mawazo yenu: Kutokana na uzoefu wangu wa kupeleka watu machimbo, nataka kuandika kitabu

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
929
1,276
Wakuu habari zenu, kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na kupeleka watu machimbo ya maeneo ya biashara, nimeweza kugundua biashara nyingi za kawaida tu, zikiwa na faida nzuri tu, sasa nataka kuandika kitabu ambacho kitakuwa na mambo yafuatayo.

AINA YA BIASHARA: Hapa nitafafanua aina za biashara mbali mbali za mitaji midogo na zenye faida kubwa au faida nusu kwa nusu, pia biashara za mitaji ya Kati na faida zake.

MACHIMBO YA HIZO BIASHARA: Hizo biashara ni wapi utapata kwa Bei rahisi, ubora wa hizo biashara na aina nyingine za utapeli kwenye machimbo ya biashara.

BEI ZA MANUNUZI NA FAIDA YAKE: Nitafafanua hizo biashara Bei zake, manunuzi, na faida utakayopata.

MAWASILIANO AU DIRECTION YA MACHIMBO: nitaweza kuwapatia mawasiliano ya machimbo husika ya biashara,kwa maana unaongea moja kwa moja na muhusika mkuu na kuweza kupanga mipango,hata Kama upo mkoani atakutumia.

KUKUUNGANISHA NA MFANYABISHARA ANAYEUZA REJA REJA: Hapa nakusudia kuweza kukupa mawasiliano ya mmachinga anayeuza reja reja juu ya biashara unayohitaji kuifanya ili kuweza kupata uzoefu na changamoto.

KUKUPA CHANGAMOTO NA MAFANIKIO YA HIZO BISHARA: Hapa nitaweza kukueleza changamoto juu ya hizo biashara na fursa zake, kifupi nitafanya utafiti wa kutosha juu ya bisahara husika.

BEI YA KUUZA KITABU: Sitouza kwa hard copy, nawaza niuze kwa soft copy kupunguza gharama kwa wateja, ili masikini Kama mimi aweze kupata mawazo ya biashara.

JE NIUZE BEI GANI?? Bei ni 2000 au mnasemaje wadau maana lengo ni kusaidiana tu, nipate hata pesa ya maji tu. Si mnajua mizunguko ya kufanya utafiti sio mchezo.

HUDUMA YA ESCORT: Hapa atakayenunua kitabu na kuona kuwa bado anapata ugumu wa kutenda, nitampa huduma ya escort kuanzia mwanzo hadi mwisho.

MENGINEYO: Kama kuna kipengele nitakuwa nimekisahau au unataka nikiongeze naomba mchango wako, lengo ni kuboresha ili mtu apate mwanga zaidi.

NB: Naomba ushirikiano wenu kwa michango ya ushauri ili niweze kufanikisha jambo hili, wafuatao nawahimiza Sana na pia nitawatafuta nisikie maoni yao, GLOBAL CITIZEN na wengine.....
 
TEMBO WANGU,
Haya yote uliyoeleza ni mambo yanayobadilika kila kukicha (hayako static). Chimbo zuri la leo linaweza kuwa sehemu mbaya kabisa ya biashara kesho. Biashara ya bidhaa A leo ikiwa nzuri, kesho inaweza kugeuka na kuwa mbaya sana. Mimi nakushauri ufanye kitu kama consultation ya face to face.

Mteja anakuja anakuelezea lengo lake, unampa option unazoona zitamfaa na usaidizi anaohitaji na kukulipa kulingana na makubaliano yenu. BTW kama unajua mambo mengi namna hiyo kwa nini usifanye mwenyewe hizo mishe? Umekosa mtaji? Umekosa muda? Huna motivation?
 
Haya yote uliyoeleza ni mambo yanayobadilika kila kukicha (hayako static). Chimbo zuri la leo linaweza kuwa sehemu mbaya kabisa ya biashara kesho. Biashara ya bidhaa A leo ikiwa nzuri, kesho inaweza kugeuka na kuwa mbaya sana. Mimi nakushauri ufanye kitu kama consultation ya face to face. Mteja anakuja anakuelezea lengo lake, unampa option unazoona zitamfaa na usaidizi anaohitaji na kukulipa kulingana na makubaliano yenu. BTW kama unajua mambo mengi namna hiyo kwa nini usifanye mwenyewe hizo mishe? Umekosa mtaji? Umekosa muda? Huna motivation?

Sina cha kuongezea umeongea yangu n mimi yooooote
 
TEMBO WANGU,
Nimependa wazo lako. Lifanyie kazi aisee. Hiyo 2k ya kitabu ni fair kabisa.

Ila hapo ulipotaja "escort" mweee nikagutuka kidogo 😂. Wazee wa kupenda mambo yale wanajua "huduma ya escort" inamaanisha nini. Usijali lkn nimekuelewa maana yako vilivyo.
 
Naendelea kupokea comment zenu,......wengine wanasema eti kwanini usifanye mwenyewe hizo mishe, nilichogundua kuwa Kuna tofauti Sana Kati ya mtafutaji na mtu anayeishi kwa Dada yake...hawa wawili mawazo yao yanatofautiana Sana....lakini yote ni mawazo naendelea kuyapokea.
 
TEMBO WANGU,
Haya yote uliyoeleza ni mambo yanayobadilika kila kukicha (hayako static). Chimbo zuri la leo linaweza kuwa sehemu mbaya kabisa ya biashara kesho. Biashara ya bidhaa A leo ikiwa nzuri, kesho inaweza kugeuka na kuwa mbaya sana. Mimi nakushauri ufanye kitu kama consultation ya face to face.

Mteja anakuja anakuelezea lengo lake, unampa option unazoona zitamfaa na usaidizi anaohitaji na kukulipa kulingana na makubaliano yenu. BTW kama unajua mambo mengi namna hiyo kwa nini usifanye mwenyewe hizo mishe? Umekosa mtaji? Umekosa muda? Huna motivation?
Bora uanzishe blog,you tube,website, social media accounts.Habari inayofanana unaitupia note huko.
 
Kitabu hicho kikiwa tayari niarifu ninunue, kwanza hela yenyewe ni rafiki kwa mwenye nia ya kujua angalau kwa kuanzia ktk biashara husika. Mengine mtu atajiongeza mbele ya safari.

Suala la kubadilika kwa fursa si neno maana utakuwa unatengeneza toleo jipya kulingana na mabadiliko ya wakati husika. USINISAHAU KUNIARIFU KIKIWA TAYARI.

Tunapoteza hela ktk mambo mengi yasiyoupa ubongo chakula lakini bado wajumbe wanaona kama wanaibiwa mchana kweupe wao kukupoza kwa maji kidogo.
 
Back
Top Bottom