Mawazo yanaua tuyaepuke

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,482
11,833
Mawazo ni mlundikano wa matukio kwenye akili, yanaweza kuwa ni matukio mema au mabaya ila matukio haya huwa yanajirudia rudia kiasi cha kumfanya muwazaji kushindwa kuendelea na mambo mengine,mfano unampenda msichana/mvulana fulani jinsi utavyomuwaza utawaza mbinu za kuweza kumteka ili awe wako na mengine kama hayo ila tukirudi kwenye mawazo mabaya tuchukulie umeachwa na unae mpenda utakaa na kuwaza kuwa muda huu yupo na mtu mwingine wanafanya mapenzi utaumia utashindwa kufanya ya maana kwa ajiri ya mawazo.
Mawazo huweza kusababishwa na mambo mengi sana;
  • Kufukuzwa kazi.
  • Kuachwa na mpenzi.
  • kutengwa na familia.
  • Mauzi na karaha kutoka kwa marafiki/majirani
  • Kushindwa kujikimu kimaisha.
  • Kupata maambukizi ya magonjwa makubwa kama VVU/UKIMWI
na mambo mengine mengi ambayo humtokea mtu bila kutegemea ambayo yanapelekea moyo kujeruhiwa vibaya na kuleta simanzi.

stress.n.jpg

Kutokana na mawazo mwingine anaweza akashindwa kulala, wengine wanashindwa kabisa kula ila wengine inakuwa tofauti wao wakiwa na mawazo wanakuwa na tabia ya kufanya mambo kupitiliza utakuta mwingine anakula au kunywa pombe kupita kiasi,asilimia kubwa ya watu walioathiriwa na mawazo hujikuta wanafanya mambo ambayo baadae hujikuta wanajuta sana,wengine hufanya mambo ambayo yanastaajabisha sana,mambo ya aibu.Chanzo kikiwa ni mawazo, muda mwingine mawazo yanaweza yakamfanya mtu akatamani ata kuuondoa uhai wake.
menshealth11.jpg

Kuna wengine hujaribu mbinu mbali mbali ambazo si sahihi ili kuondoa ama kupunguza mawazo,eti mtu anaamua kunywa pombe,au kufanya ngono sana ili tuu apunguze mawazo ila matokeo yake mambo umgeukia na kujikuta amepata matatizo makubwa sana.Mawazo mabaya sana, sana.Kuna wengine wanalala sana pindi wawapo na mawazo hivyo shughuLi zinasimama anashindwa kufanya kazi vizuri kila mtu ana mawazo ila kuna utofauti wa kiwango cha athari za mawazo wengine wanaathirika sana wengine wana weza kukabiliana na mawazo hivyo wanaweza kuwa na mawazo na usiwatambue kuwa wana mawazo ila wengine wanaweza kuwa na mawazo ukamtambua, kakondeana watu wote tukajua kuwa furani kuna jambo lina
mtatiza.
business-man-heavy-stress-rock-28158774.jpg

Ila chanzo kibwa cha yote hayo ni mtu kutokukubari matokeo,si kukubaLi tuu bali wengi kushindwa kutumia hili neno hapana au pengine wao hawapendi kuambiwa hapana sasa ili kuzuia athari za mawazo jifunze kusema hapana na kukubari matokeo pindi unapoambiwa hapana ndio ukubali pindi unapokataliwa kwa jambo lolote lile iwe umekataliwa kwenye mapenzi, kazi, nk. Vile vile unaweza kupata mawazo kwa kushindwa kwenda na muda ndio muda ni muhimu sana ishi maisha kama uliyokuwa unaishi shule hakikisha unakuwa na ratiba ya siku nzima katika hiyo ratiba ondoa mambo yote yasiyo yamsingi hii itakufanya ufanye kazi zako kwa umakini mkubwa.
RIzNkmh.jpg

Mawazo huwaathiri watu wa rika zote ata watoto pia nao wanawaza tena wana waza sana pengine kulingana na watu wazima,mtu mwenye mawazo ni kawaida sana kuwa na uso wenye huzuni, mara nyingine hukosa kabisa furaha,mawazo yana athiri sana ila ni vigumu sana kugundua kuwa unaathiriwa na mawazo ila asilimia kubwa sana ya watu tunaopishana nao mitaani wanaathiriwa na mawazo.
child_cry_crying_tears-800x430.gif

Wengine kutokana na mrundikano wa mawazo hujikuta wanashindwa kujizuia huanza kububujikwa na machozi,wengine hulia kwa sauti,wengine huugulia moyoni na matokeo yake hujikuta wanapoteza kilo nyingi sana kwenye miili yao ila tukumbuke kuwa kilio hujireta chenyewe kamwe mtu hawezi kujizuia kulia hivyo inapotokea ukajisikia unataka kulia lia sana lia hadi machozi yakauke kwa kufanya hivyo utakuwa umejipunguzia mawazo kwa kiasi kikubwa sana.​
fanya yafuatayo pindi unapopatwa na msongo wa mawazo...
  1. Epuka marafiki wabaya.
  2. Tafuta mtu mzima mwenye busara umuombe akushauri juu ya jambo linalokutatiza.
  3. Epuka kabisa matumizi ya vilevi eti ili upunguze mawazo badala yake vilevi vinaweza kukuongezea matatizo.
  4. Tumia muda mwingi ukiwa na familia yako.
  5. Fanya utalii wa ndani {tembelea mbuga za wanyama ama makumbusho}
  6. Usiendeshe vyombo vya usafiri kwa muda mrefu/usiendeshe kabisa.
hollis-talking-family.jpg

Itaendelea......
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom