Mawazo yakinifu kuhusu Kivuko (MV kigamboni na MV magogoni)

Unasemaje Juu ya maoni yaliyotolewa kuhusiana na pantoni zetu nchini?

  • hayana umuhimu

    Votes: 0 0.0%
  • mengineyo

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    8

Siadavy

Member
Mar 6, 2012
6
0
:welcome:Habari zenu wadau,
Napenda kuchukua nafasi hii, kutoa maoni yangu kuhusiana na pantoni zetu za Dar na hata za mikoani.
Wahusika mpatapo mawazo haya ni vema mkayafanyia kazi kwa yale mtakayoona yana tija.

Maoni
1. wahusika ni vyema kutoa elimu ya kuyatumia jaketi okovu(LIFE JACKET) na vifaa vingine vilivyopo ndani ya pantoni kwa ajili ya kujiokoa endapo kutatokea tatizo.

Maelezo:
pantoni zetu zina vifaa vingi tuu kwa ajili ya uokoaji endapo kutatokea tatizo pantoni ikiwa katikati ya bahari au ziwa. kwa hili nawapongeza sana wahusika ila JE MNAUHAKIKA KILA ANAYEINGIA NDANI YA CHOMBO HICHO ANAUELEWA WA KUTUMIA VIFAA HIVYO???? AU Tunangoja hadi litukie tukio ndipo muanze elekeza abiria jinsi ya kutumia????? Bila shaka kuna tatizo hapa.

Nini kifanyike

Ndani ya pantoni zetu hapa tanzania, nyingi zina radio au screen. napendekeza ziwepo picha zinazoonesha kwenye screen zikimuelekeza abiria jinsi ya kutumia vifaa vile, au kama hakuna screen basi mtangazaji awe anatangaza kila mara abiri aingiapo kwenye pantoni. kuliko kumlipa mtu kila siku anasema tuu karibu kwenye pantoni yetu, karibuni kwenye pantoni yetu. tena kwa shifti, tuwape kazi zaidi ya kutoa elimu kwa kuelekeza abiria. Mfano mzuri ndugu zangu, uingiapo ndani ya ndege :plane:, kabla ya ndege kuondoka kuna muhudumu huwa anatoa maelekezo jinsi ya kutumia zile life jacket na nini cha kufanya endapo kunatatizo litajitokeza. vivyo hivyo natamani kwenye pantoni ifanyike.

Ni vizuri tunavyoweka matangazo mengine kwenye screen zile hata kama hizo screen zilitolewa na wanaoweka matangazo na imani hawataweza kukataa na hata hivyo haidhuru chochote tukiongeza matangazo au onyesho la jinsi ya utumiaji wa life jacket, boya etc.

2. Kuhusu kufanya service ya pantoni na vifaa hivyo vya uokoaji.

maelezo

Kuwepo na ratiba (schedule for service) ya kufanyia service pantoni yenyewe na siyo kusubiri hadi iaribike ndipo ifanyiwe matengenezo. ikiwepo ratiba inatangazwa inabandikwa na kutangazwa ili kukumbusha watu siku fulani pantoni haitafanya kazi kuanzia masaa fulani hadi fulani ili kuwafanya abiria nao wajipange kutokana na usumbufu utakaotokea. na ni matumaini yangu mda utakaopanga utazingatia huduma. namaanisha usiathiri kwa kiasi kikubwa
sana. kwa hapa kwa kweli mtaangalia jinsi ya kufanya.

Kuhusu service ya life jacket boyas, etc
Hivi ndugu zangu toka pantoni inunuliwe jamani kuna hata siku moja mlisha wahi kuangalia yale maboya, life jacket ziko katika hali gani??? Ni wazi mnajua kabisa kuna panya ndani ya pantoni na life jacket ikiliwa na panya, ina maana imeshatoboka. na hivyo haitaweza kutumika endapo kuna ajali imetokea. HIVI JAMANI TUNAKWENDA WAPI???
Okay nimekaa na kusema sina budi kuongea na kutoa maoni yangu. naomba jamani tusingojee litokee ndipo tuanze kusema yes maboya yalikuwa ya kutosha na hata life jacket zilikuwa za kutosha ila yalikuwa hayana upepo au yalikuwa yameliwa na panya. Mimi naangalia mbele sana, nikitafakari hata zile funguo zinazofunga yale makabati ya hivi vifaa sina uhakika kama wahusika wanajua zilipo. au tutaanza kuulizana funguo:A S-key: ziko wapi wakati wa ajali au hata kusema kofuli alifunguki kwa sababu ya kutu siku ya ajali. Mimi naamini tulikuwa tumelala na sasa kwa kutumia maoni yangu naomba tuamke. tufanye kazi kwa kufikiria endapo ikitokea hili tunaweza okoa abiria???? siyo kungoja itokee alafu ndipo tujifunze.

Kwa kifupi
Pantoni zifanyiwe service mara kwa mara na siyo kusubiri iharibike. ila ratiba ya service itangazwe kwa abiria siku mbili kabla.
Vifaa vya uokoaji vifanyiwe service(kujazwa upepo au kuzibwa kwa yale yaliyotoboka). makabati yawe yanafunguliwa na kuhakikisha funguo zipo sehemu rahisi kupatikana wakati wa ajali au tatizo


3. Kuwepo na sehemu ya kuweka maoni ndani ya pantoni au mtu wa kusikiliza abiria wakiwa ndani ya pantoni.

Maelezo


wahusika najua kuna watu wana kero nyingi sana kuhusu wahudumu wanaohudumu ndani ya pantoni. wale jamaa utafikiri hicho chombo tunapanda bure au tumeomba msaada kwa himaya yake.
ni hivi
- Nikianza kabisa na sehemu ya kukata tiketi
Mfano huu ni wa kweli na mimi binafsi ndiye mlengwa, imenikuta wikii hii na ndipo nikasema sina budi sasa kuongea.
nimetoa elfu mbili akaangalia akasema badilisha hiyo hela. mimi nikaiangalia nikifikiri nimetoa hela mfukoni ikachania au nini tatizo ila sikuona tatizo na wakati naiangalia waliokuwa nje waka guna, mmoja akaropoka kwa sauti akasema hela hii inatatizo gani au una gundu la nyumbani kwako. mwingine akasema hizi hela unaweka kwa nyumbani mwako au zinaenda benki. ila mimi sikuongea chochote nikaingiza mkono mfukoni nikatoa elfu tano. unajua akanijibu nini. sina chenji. kwa kweli nilijisikia vibaya nikamuuliza. dada nimekupa elfu mbili umesema nibadilishe hela, nimekupa elfu tano unasema sina chenji. unataka nifanyeje. akajibu kwa ubabe. Nimeshakuambia sina chenji unanilazimisha katafute huko kwa wengine. niliondoka nikaenda upande wa pili nikampa ile elfu mbili akapokea akanipa chenji.
natumai unaweza ona jinsi gani hawa tunaowaweka pale watuhudumie wanavyosahau wajibu wao na kujiona wamefika. nikasema laiti kungekuwa na mtu anasikiliza malalamiko ya abiria nikifikisha kwake ila hakuna na kama yupo hawekwi wazi kwa hiyo hatujui wapi kufikisha hivyo unakuta mtu analalamika tuu na kubaki na kero yake.

- Tuende kwenye pantoni yenyewe. (rubani na jopo lote linalokuwepo kule juu)
Unakuta pantoni umeshafunguliwa kuingia. ila pantoni inaweza chukua hata nusu saa inasubiri tuu. sasa ukiuliza inasubiri nini hujui. ila kwa vile abiria hata kama anauzika hawezi sema lolote basi utakuta kule juu wana piga story :lol: na mda watakao wao ndio wanaanza kuondoa. JAMANI WAHUSIKA KILA MTU HUWA ANA RATIBA YAKE MUHIMU SANA NA KASHAPANGIA MDA WAKE. WEWE UNAPOKUWA MZEMBE UNASABABISHA MADHARA MENGI SANA. SIJUI KAMA HUU NI UNGWANA.
ni kweli kuna wakati pantoni inasubiri meli ipite huwa wanatoa taarifa au watu wasogee watoke mlangoni, ila kuna wakati huwa tuu wameamua kukaa kimya, kama vile umeomba lift gari ya mtu. atasimama anapotaka na ataondoka katika mda anaotaka. huwa siyo ungwana. wengine ni wagonjwa, wengine wanawahi kazini, au hospitali. yapo mengi ila wenzangu hawajali. na si hawajali bali hakuna wa kuwakumbusha endapo kuna kitendo kama hichi kinatokea. siku ingine masikini, utakuta mtu kasimama chini pale pana jua au mvua anajua ni dakika 5 tuu navumilia nitakuwa nimeshavuka. kumbe tunasema mawazo yako siyo yao. wenzako wanachapa stori tuu.

Nini kifanyike
Kurekebisha hili natumai kungekuwepo na sehemu ya maoni, au muhusika atakaye unganisha baina ya abiria na chumba cha rubani juu nafikiri itasaidia au tubuni njia nyingine ilimradi hili tatizo tulitokemeze. mi nafikiri kuna siku UPOLE/UKIMYA :A S embarassed: WA MTANZANIA UTAFIKA MWISHO, Na watachoka kunyanyasika na siku moja wataamua kupanda wote juu na kuleta fujo. kuepusha hili tutumie UVUMILIVU wa mtanzia vizuri. acheni kunyanyasa abiria wa pantoni wapeni haki zao. sijaongelea lugha ya matusi huwa inatumika sana kwa pantoni hasa ukiwa kwenye pantoni ndogo. wadau wanaweza ongezea kwa hilo ila la msingi tuchukue hatua.

haya ni baadhi tu ya kero ebu ruhusu watu watoe maoni yao ndipo mtakapopata yanayojiri.:juggle:

yapo mengi ila hapa nitawachosha . tuzikatie haya na ndipo nitakuja na mengine kama la kuboresha sehemu za abiria kusubiria pantoni nakadhalika. :focus: WAHUSIKA MKIONA YAPO YANAYOWEZA KUFANYIWA KAZI NA MKIONA NI YANAUMUHIMU CHUKUENI HATUA. ILA SI KILA MAONI LAZIMA YATEKELEZWE. NI USHAURI TUU.
:closed_2:
 
We in Africa do prefer reactionary measures to precautionary ones! Who cares in Africa....!
 
Ndugu yangu zaleoleo acha uvivu. si kushangai kwani ndio utamaduni wetu waafrika. (wavivu kusoma sana) Hapo katika message kuna vipengele vifuatavyo. kwa kifupi, maelezo zaidi,nini kifanyike na maoni namba. we soma unachotaka kusoma ukiona hujaelewa kuna maelezo zaidi au huna mda tafuta sehemu imeandikwa kwa kifupi. otherwise acha wenye kusoma wataisoma na wahusika wataipata tuu hata kwa rumors.
 
I am so grateful kwamba kuna mtu mwingine ambaye ameona mapungufu mengi yaliyopo kwenye vivuko vyetu. At one point, i thought of finding a signing sheet, getting people signatures atleast 200 then nizipeleke SUMATRA au Ujenzi maana ni kama Ferry hakuna utawala..kila mtu anajiamulia la kwake. Leo mnakimbizwa mchakamchaka kesho wanalala.
Nadhani suala zima la management lina shida. Nimekuwa nikiwafuatilia wale captains, it seems as if they are not answerable to anyone, hivyo hufanya wanavyojisikia. Wakiamua kuchelewa kuanza huduma asubuhi basi hiyo foleni siku hiyo balaa. Mbaya zaidi ni pale wanapoamua kutegeana au huwa wakicheleweshewa malipo yao ya kufanya night shift wanafanya kazi KIZEMBE basi tabu kweli kweli kwa wasafiri. Nimekuwa nikitamani kuwaripoti mahali husika lakini nikiangalia mfumo mzima wa utawala pale ferry naona captains wanajitawala wenyewe.

Ndio maana Mheshimiwa waziri alipoongea juu ya kupandisha gharama za kivuko, wananchi walikuja juu...nadhani hawakuwa wakilalamikia ughali wa malipo peke yake per se bali huduma mbovu ambazo haziboreshwi. Service haimeet expectations kabisa.

Kuhusiana na wahudumu, nimepata experiences kadhaa mbaya, moja ni nilikuwa na 10,000 na sikuwa na fedha nyingine yoyote ile, nilipowapa dirishani walinipa noti za 1000 kama sita hivi halafu hiyo 4800 iliyosalia walinipa coin za 200..nilitoka na lundo langu la kutosha. Wanahitaji training ya customer service, hawako friendly kabisa.
Ingesaidia zaidi kama wangeweka wakata tiketi wanne au zaidi maana watu ni wengi sana kuliko uwezo wao wa utendaji hivyo kusababisha mlolongo mrefu wa watu.


I am also concerned kuhusiana na tabia ya kuweka mafuta kwenye panton saa saba mchana hivyo kusababisha panton kusimamisha kazi zake. Hivi haiwezekani kufanya utaratibu wa kuzijaza early in the morning au usiku?


Unakuta panton imepark tu, ukiuliza unaambiwa mara mafuta au service..saa saba mchana? wengine wanasema wanabania mafuta..sijui..ila ingependeza kama wangetumia muda mwingine ili yatumike muda wote.

La mwisho, kuna dada mtangazaji ana either sauti kali sana au anaweka microphone karibu sana na mdomo while at the same time anaongea kwa nguvu. Japo tunashukuru kwa maelekezo yake lakini ile sauti huwa inakera kwa kweli...wangefanya survey ya hili wangeshangaa kujua watu huwa wanakerwa kweli..dada akianza tu..gumzo zinaanza. Either apunguze nguvu kwenye kutoa sauti au apunguze ukali na kuongea kwa middle/low tone.

Niishie hapa kwa sasa...Ila nashukuru kwa kuileta hii mada, hope wahusika wataiona na kuifanyia kazi.
 
Nadhani chimama nitakutafuta tuunde tume ya ku draft barua nzuri na kuifikisha mahali husika.kwani hizi ni dhama za uwazi na ukweli. tutaenda na kujitambulisha na kufikisha malalamiko yetu kama abiria. kwa sasa tuwape muda. kama hakuna mabadiliko tutajipanga kijana. Kero kwenye pantoni zimezidi sana. Tumechoka.
 
Huyu ni PhD student! Sampling frame yako ni wana JF? Go back to your supervisor so that he/she can advise you to make your research question clear.

Nyie ndio mnakuja kuwa ma Dr feki.
 
Back
Top Bottom