Mawazo ya wana CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawazo ya wana CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BabaH, Mar 29, 2008.

 1. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kweli viongozi wa CCM ni wapumbavu wa hali ya juu sana, nasema haya nikinukuu, maelezo yaliyotoka kwenye hazeti la mwananchi

  Kutokana na hatua ya Mbunge Mkono, walisema hakuna sababu ya kumtuhumu kwa ufisadi, kutokana na kutumia sehemu kubwa ya mapato yake kuwapelekea wananchi maendeleo ya haraka kupitia elimu

  Wabunge hawa wanadiriki kusema hata kama Mkono ni Fisadi asichukuliwe hatua yoyote, hivi hawa ndo wabunge wetu?
  Wanajua huyo Mkono kaiba kiasi gani za walipa kodi na katumia kiasi gani kudanganyia??
  Je kuna sheria inayosema kuwa mwizi akiiba pesa na akazitumia kwa mambo yake ya kujiimalisha kisiasa jimboni kwake kwa kusaidia wananchi kwa asilimia fulani ya pesa za ufisadi then tunamuacha??

  Mwandishi anaripoti tena.....
  Wajumbe hao walisema hatua ya Bw. Mkono kujitolea kujenga shule kama hizo ni moyo wa kuiga, kwani hata kama alizipata bila halali lakini amezileta kwa wananchi badala ya kujali tumbo lake, kwani hata angekula au kuzipeleka nje asingeulizwa.

  Vigogo wa CCM hapa wanadiliki kuwaeleza Watanzania kuwa hakuna Fisadi hata mmoja hatakayechukuliwa sheria, hii inajionyesha wazi wanaposema kuwa hata kama Mkono angazi pesa hizo hakuna ambaye angemuuliza

  Je hizi ni fikra kabisa za wabunge, na haya ndo maneno wanayoyataoa kwa wananchi wao? Na kwa maneno haya tunaweza kuelewa kuwa yawezekana kamati zinazoundwa na Mkuu wa kaya ni feki kwa sababu NEC wao wanajua hata ukiiba pesa hakuna lolote

  Haya na 2010 wanashinda tena, NDIVYO TULIVYO HIVI NA TUNAKUBALI TUUUU
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  DUUUUU! It is very very very interesting BabaH! Siamini... labda mwandishi aliwasikiliza vibaya!!! Na kama ni kweli basi kwa asilimia 100 leo naamini pasi na shaka kuwa CCM NI CHAMA CHA MAJAMBAZI... Du... ngoja nikanywe maji kwanza kwani nimepata mshtuko si wa kawaida!!!!
   
 3. t

  think BIG JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 236
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mawazo ya wabunge ni julimsho la mawazo ya waTanzania. Upuuzi huo uko si kwa viongozi au wabunge tu bali kwa Taifa zima la Tanzania. Unapoona Mbunge au Waziri anaongea upuuzi kama huu, basi ujue uzao wake wote (ama anaowawakilisha) nao unaupuuzi kama huu kwenye mbongo zao! Wahenga husema "mtoto wa nyoka ni nyoka".

  Kama unabisha waulize wakazi wa Monduli (.. na zulia lao jekundu) au wakazi wa kiteto (.. walipoamua bila kufikiri).

  Siku wananchi wakiamua kutofikiri kama Viongozi wao, basi viongozi wetu watabadilika! Tulionyesha mfano pale tulipokataa mawazo na fikira za wabunge wetu (kupitia kura za REDET), na matokeo baada ya hapo tumeona "RICHMOND" ilivyoshughulikiwa Bungeni ... na sasa tunasubiri EPA ...

  Ni mimi na wewe wakuondoa "upuuzi" huu na wala si CCM kama chama!!
   
 4. a.9784

  a.9784 Senior Member

  #4
  Mar 29, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani Mkono na wewe ni fisadi,chama basi kinanuka mafisadi,hadi wana sisiem wenzako wanalijua hilo.Kazi ipo wana JF.

  Kuna mtu mmja namfahamu,naamini na wengine wanamfahamu pia kwamba alikua jambazi sugu,ilitokea siku moja akaiba dau kubwa na alipofanikiwa kupata lile bulungutu aliamua kuokoka na kununua vyombo vya muziki wa injili.

  Je Mkono anaweza kulinganishwa na huyu?
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa wamewadharau watanzania hadi kufikia kuhalalisha ufisadi kwa kutafutia sababu mbadala ? Tanzania tuna elekea kubaya .
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0

  Mkuu Think Big,

  Ujumbe wako ni mzito sana, yaaani viongozi wetu wakiwa wapumbavu, basi sisi wananchi ndio wapumbavu kuliko wao maana tunajua kuwa ni wapumbavu, halafu tunawachagua anyways, baadaye tunakuja kujaribu kuvikimbia vivuli vyetu huku Jambo Forums!
   
Loading...