Mawazo ya kuoa mtumishi ni Unga wa maisha au kasumba mpya ya mjini

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,607
9,811
Habari zenu wadau

Kuna hilo jambo limekuwa likishika kasi kwa sasa hivi hususani kwa vijana ambao ni wajiriwa na wadada ambao ni wajiriwa

Jambo lenyewe ni kuhusu kaingia katika ndoa, ukikuta Kijana ajaoa ukimuliza mpango wake wa kuoa anakwambia anatafuta mfanyakazi mwenzie, hili suala hata kwa wadada ni hivyo hivyo

Ukiuliza kwanini anataka mfanyakazi mwenzie majibu yao ni kusaidiana maisha na kupunguza ukali wa maisha


NJOO KWENYE UHALISIA SASA

ukija katika jamii ndoa ambazo zinaongoza migogoro ni za hawa watumishi

Ndoa ambazo zina matatizo mengi ya maendeleo ya familia kiuchumi na kijamii ni ndoa za hawa watumishi


Yani unakuta mama mtumishi baba mtumishi hawasomeshi wala nini na wana miaka zaidi ya mitano lakini bado wapo nyumba ya kupanga, usafiri bado wanatumia wa umma hawana hata pikipiki, wote benki wana madeni huu ni mfano tu


Sasa ndio nauliza hivi kuoa mtumishi au kuolewa na mtumishi ni uoga wa maisha au kasumba

Karibuni wadau
 
hyo ndo habari ya mjini asee, mi mwenyewe nawinda mtumishi hapa. . . upate mwalimu au mjeda. . . .swaaf
 
Ni kasumba potofu, binsfsi huwa naipinga kwani naamini mkioana mmoja si mtumishi wa serikali au kampuni imawapa wepesi wa mmoja kusimamia miradi mtakayoianzisha.
Pia mkioana watumishi wote asilimia kubwa ndiyo maana ndoa zimekuwa hazina amani kwani kila mmoja anaona anakipato hivyo hawezi babaishwa na mwenzake. Hata wakiachana.
Ni mtazamo wangu katika hilo
 
Ubinafsi... kuwa na mipango ya muda mfupi ambayo siyo endelevu... hawataki kuchangia gari wanataka kila mtu awe na lake, hawataki kuchangia ujenzi wa nyumba wanataka kila mtu ajenge yake... hawataki kuunganisha kipato na kuwa kimoja wanataka kila mtu afuge zake...
 
Kuna wakati ukiwa mvivu wa kufikiria unaona ni sahihi kuoana watumishi kwa watumishi ila ukiwa unatazama mbali utapenda uwe na mke/ Mme ambae anakazi tofauti na yako
 
nipo hapa mkuu maana nimekosa mume kisa sina degree
Aaaaahh!!! unabaguliwa Miss? achana nao hata usijisikie vibaya. Waendelee kupigwa doro maofisini huko, makato ya mishahara yenyewe ndo hayo yanapanda kila siku!

Uzuri tusio na madigrii ndoto yetu kuu huwa ni mafanikio ya kiuchumi, wao ndoto yao kuongeza elimu tu!

Karibu tujenge familia bora...
 
Nilishawahi kufikilia kuwa baadhi ya matatizo ya wanandoa watumishi hasa mwanamke anapokuwa mtumishi.. huwa yanasababishwa na mwanamke kupenda au kujari kazi kuliko hata mme kwa sababu kazi inautaratibu wa kuenda na mda na inamfanya mtu kuwa mtumwa...mfano kazini mwanamke anahitajija kufika saa mbili na huenda kuna majukumu ambayo mme wake angehitaji amtimizie asubuhi hiyo,labda kumuandalia jambo Fulani.hapo ni lazima mwanamke atasema anawahi kazini kwa kauli hiyo tu tayari tatizo litakuwepo ingawa mwanaume hata ongea chochote lakini kwa kuwaza itakuwa 'INA maana kazi ni muhimu kuliko Mimi Mme wake'
Lakini pia kuna suala LA mgegedo..unakuta mmoja yuko off kazini Siku hiyo na anahitaji morning glory lakini mwezake Yuko zam ofisini...sio rahisi kukupa ndoa wakati kazi imebana tayari hilo ni tatizo.. Hapo hapo ndio maana wafanyakazi wengi wanamichepuko kwa sababu kazi huwa inachukuwa sehemu ya maisha ya ndoa na tendo kwa ujumla..
Kwa Mimi kwa vile sio muajiliwa,nikipata muajiliwa sawa ila nikipata mwenye kipaji cha biashara nitafurahi zaidi
 
Back
Top Bottom