Mawazo ya Kukanyagwa

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,554
1,382
Wale waliobahatika kusikiliza vipindi vya Mazungumzo Baada ya Habari vya miaka ya sitini hadi themanini watakumbuka Mzee Paul Sozigwa alivyokuwa anaonya vikali tuachane na "Mawazo ya kukanyagwa". Je, ilikuwa kazi bure? Maana haya mawazo ya kukanyagwa yameshamiri sana Tanzania ya leo. Nitoe mifano.

Nilikuwa Dar Januari na nikanunua viatu vizuri sana vya ngozi, 100%, made in Tanzania, sehemu za Salasala. Bei ilikuwa elfu hamsini. Siku mbili baadaye nilifika kwenye duka la viatu Mlimani City na nikaona viatu kama nilivyonunua, vimetoka Uturuki, na bei laki 3. Nikamwuliza dada muuzaji aangalie nilivyovaa akakubali ni vizuri kama alivyokuwa anauza. Nikamwuliza mbona haweki dukani kwake hivyo vya Tanzania pia? Akajibu watu hawatanunua. Hii ni matokeo ya watu kujaa mawazo ya kukanyagwa.

Nikiwa kwetu nakunywa Serengeti Light. Ni nzuri sanana. Ukipenda zenye kilevi zaidi na zimegemwa Tanzania zipo, na ni nzuri sana. Lakini utakuta hata viongozi wanadhani bia za nje, na hasa za Ulaya kama Heineken, ni nzuri zaidi. Watu mara oh, Calsberg, mara Windhoek. Ni mawazo ya kukanyagwa. Sana.

Maji mazuri sana tunayo, mfano ya Kilimanjaro, lakini mawazo ya kukanyagwa hufanya wengine watamani imported drinking water. Hata ya kutoka nchi kama Singapore ambapo wanasafisha maji yaliyotumika vyooni na kuyasambaza tena.

Chimbuko la kushamiri kwa haya mawazo ya kukanyagwa ni kujidharau wenyewe. Ndiyo maana tunaona mwajiriwa yoyote toka nje ni bora zaidi yetu. Mawazo ya kukanyagwa sana!

Paul Sozigwa alikuwa apigana na haya mawazo kwa kutumia kauli mbiu iliyokuwa inatangazwa mara kwa mara RTD isemayo: "Umma wa kijamaa.... una nguvu zisizo kifani! Wavivu, wanyonge na wapinzani wa nguvu hizo hukanyagwa na kupondwapondwa wasionekane asilani!" Kulikoni tuliotesha mbaazi lakini tunavuna mbigili?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom