Mawazo shindani hujenga busara na kupunguza kushindwa kwa jamii na nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawazo shindani hujenga busara na kupunguza kushindwa kwa jamii na nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jun 18, 2012.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naandika si kwa sababu nitashikilizwa na wenye mamlaka ya wingi au wachache kwa wingi lakini wengi wa hoja, nataka nisikike ili busara ikatumike kukubali mawazo bora katika bajeti hii, kushindanisha mawazo ni kuruhusu fursa ya kupata matokeo bora katika jambo jema tulilopanga kulitekeleza na si sawa na kushindanisha wanamieleka ambao mshindi huchukua tuzo yote. Kwenye kushindanisha hoja hakuna mshindi wala mshindwa, mshindi ni wote.

  Chonde sana Wabunge wa CCM nyie ndie wenye nchi, nyie ndie watawala kauli zenu zaweze kuleta neema, hoja zenu zaweza kuogopwa, na kivuli chenu chaweza kuwa neema kwa wanyonge na waliowengi . Msiwashambulie wenzenu kabla ya kuwatathmini, chukueni muda kutafakari mazingira wanayoishi watanzania waliowengi, kuweni watulivu ili utulivu huo utumike kusahihisha makosa ya nyuma na ya sasa.


  Tusiwanyonge watanzania wenzetu wenye hoja kwa nguvu ya wingi wetu, tusiuwe kauli tetezi, tuzipambe kwani nia yao si kutafuta umaarufu kwa sasa wao tayari ni maarufu kupita kiasi na sauti zao zisipo sikika bungeni zitatafutwa na wenye kiu nje ya bunge, gharika hilo halina ukuta wa Berlin, madhara yake hayazuiliki.

  Kwa kuwa imeandikwa upande wa wanyonge ndio upande wake Baba sioni nani huyo tena mwenye nguvu kuzuia ahadi yake Baba kwa waja wake. Kutokupigania wanyonge ni kuchelewesha ahadi yao kutoka kwa Baba kuelekea nchi ya Kanani.

  Ninaona kila kukicha wakina Steve Biko wengi wanazaliwa na kuongezeka katika kuendesha vuguvugu la kupinga ukosefu wa uadilifu ndani ya mipango yetu. Siku ile yaja ambapo sauti za wanyonge zitatoa maelekezo kwa wachache. Kwa kuwa ni lazima tufike huko iwe na isiwe tujisahihishe ili tufike kwa mwafaka na si kwa vurugu. Kamwe Bunge lisije kuwa chanzo cha kuamsha hasira za watanzania kwa sababu eti hamkutekeleza `wajibu wenu hiki kitakuwa ni kiroja cha karne
  Unganisheni mema ya CDM na mema CCM mtuvushe kanye dhahama hii ya kupanda kwa gharama za maisha


  Nawatakia kazi njema
   
Loading...