Mawazo mchanganyiko juu ya kuongeza ajira kwa vijana

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Nchi nyingi duniani zinakabiliwa na janga la ukosefu wa ajira kwa vijana,mfano nchi ya Nigeria ambayo nusu ya watu wake ni vijana wenye umri kati ya miaka 15-35 inakabiliwa na ukosefu wa ajira ya zaidi ya vijana 11.1 milioni. Halikadhalika nchi za Afrika ya Kusini, Kenya, Uganda na zingine nyingi.

Tatizo la ajira kwa Tanzania ni la kihistoria,na serikali ya awamu ya sita inajitahidi kukabiliana nalo kwa njia tofauti.Njia ya kurasimisha shuguli za wajasiria mali kwenye kilimo,ufugaji,na biashara ndogo ndogo kama kuwa na vitambulisho kwa wamachinga,pamoja na shughuli za wasanii zimeleta tija na vijana wengi wanafaidiaka kutokana na mbinu hii ya serikali.Hata hivyo juhudi hizi zimepunguza na sio kumaliza janga la ukosefu wa ajira.

Kukabili janga la ukosefu wa ajira mbinu tatu hutumika,ambazo ni kutengenza hitaji la ajira(labor demand), kutengeneza waajiriwa (labor supply) na kuimarisha mfumo wa ajira (labor market intervention). Tanzania inahitaji mbinu zote tatu kuhakikisha inakabili janga la ajira.

Makala hii itajikita katika kuonesha ni wapi serikali na wananchi kwa ujumla wawekeze kutengeneza ajira kama mbinu kuu ya kumaliza tatizo la ajira nchini.

Miradi ya Kilimo na Ufugaji wa Pamoja
Changamoto za mitaji,masoko na teknolojia zinaweza kutatuliwa kwa kuwajumuisha watu pamoja.Kilimo cha pamoja kinaweza kuwawezesha wakulima kupata tija kupitia kilimo na kuifanya kazi ya kilimo kama ajira kama zilivyo ajira zingine. Wataalamu kutoka nyanja mbalimbali wanauwezo wa kukusanya mtaji na kuanza kilimo katika ngazi ya chini na kukua haraka. Mifano ipo ya watu kununua heka tano kwa Tsh 500,000 kwa maana ya kila heka moja kwa Tsh 100,000 na kulima vitunguu na kukua mpaka kufikia umiliki heka 100 na kuondokana na umaskini.Ipo mifano hai kama hii kwenye wakulima wa mboga mboga na matunda ambao wamejumuika pamoja kupata mitaji na nguvu kazi kukabili umasikini

Miradi ya Viwanda vya Pamoja
Tunarudi pale pale changamoto kubwa ni mtaji,lakini kwenye suala la viwanda changamoto nyingine ni ujuzi.Tunalotatizo la kundi kubwa la vijana kupitia mfumo wa masomo ambayo kwa namna moja au nyingine yanawapelekea kuwaza kuajiriwa na sio kufungua karakana kwa ajili ya kutoa huduma kutokana na ujuzi alio nao.Sera nzuri za viwanda pamoja na elimu bora hasa ya ufundi ni njia pekee ya kufanikisha hili.Mifano ipo ya nchi kama China,Ujerumani pamoja na nchi zingine ambazo zimepiga hatua kwenye viwanda.

Mfumo mzuri wa uanzishaji wa biashara
Mfumo uliopo kwa sasa hivi unahitaji mwananchi kulipa tozo mbalimbali kama vile Brela,Manisapaa,TRA na zingine kabla ya kuanza biashara.Mfumo huu sio rafiki kwani gharama hizi ni sehemu ya kikwazo wa vijana wanaoingia kwenye biashara.Kuikabili changamoto hii ni pamoja na Serikali kuwapa vijana wanaomaliza vyuo na kutokuwa na kazi wenye nia ya kuanzisha biashara mfumo mzuri kodi(Tax heaven).Mfumo huu unahitaji udhibiti mkubwa wa serikali ili kuhakikisha msamaha wa kodi unawanufaisha wakusudiwa na ni wa muda maalumu.

Mfumo wa Utambuzi wa Vyeti kama dhamana
Kwa idadi ya wahitimu na changamoto za ajira zilizopo,ni wazi kuwa serikali ikishirikiana na taasisi binafsi wanaweza kuongeza thamani ya cheti cha kuhitimu cha kijana kwa kukitumia kama dhamana ya mkopo usio na riba ili kutengeneza ajira au kujiajiri.Hili linaweza kufanywa na bodi ya mikopo ya vyuo vikuu,kwa kuwakopesha wahitimu mitaji kulingana na kazi mradi zao.(Proposals)

Miradi mipya ya Kimkakati
Miradi ya Umeme,miradi ya ununuzi wa ndege za mizigo,ujenzi wa bomba la mafuta,miradi ya Mwendokasi pamoja na miradi ya SGR inaweza kuongezewa fedha kwa lengo la kuongeza wigo wa kuajiri vijana kwa lengo lakuwapa ujuzi na kuwapatia mitaji.
Kusamahe malimbikizo ya kodi kwa kampuni ndogo.
Zipo kampuni binafsi ambazo zilifanikiwa kupata msamaha wa malimbikizo ya kodi uliotolewa na Raisi 2018.Kutokana na taarifa kutowafikia wenye makampuni ni wazi uwa zipo pia kampuni ambazo hazikuweza kuwasilisha taarifa ili zifaidike na mpango huuu na kuanza tena biashara.

Wakaguzi binafsi (Private Inspectors)
Tasisi za Umma kama EWURA,OSHA,TRA,TAEC,NEMC,na zingine ziweke mfumo wa kuajiri wakaguzi binafsi ambao watapewa kamisheni kwa kazi wanazofanya.Mfumo huu unafanywa na OSHA.Kiwango cha ufanisi katika mfumo huu kiboreshwe.

Mfumo wa Kuhitimu katika kazi za Serikali
Utumishi wa Umma unahitaji kuhitimu ili kupisha waajiriwa wapya,wastaafu wengi wamekua wakiongezewa muda wa kufanya kazi huku kundi kubwa la vijana wakiwa mtaani bila ajira.Gharama za kuongeza mikataba kwa wastaafu zinatosha kuajiri vijana wapya zaidi ya watatu.

Uthibiti wa ajira
Ajira ambazo zinazowezekana kufanyika na watanzania ni vema zikafanywa na watanzania kwa lengo la kuwapa ujuzi na kubakisha fedha ya ndani

Kama una wazo la namna ya kukabiliana na janga la ajira nchini na duniani naomba uchangie hapa.

Ahsante
 
Sawa mkuu me naunga mkono hoja yako. Ila jamani anayejua ajira zitatoka lini aniambie maana me nimesoma kozi ambayo siwezi kuajiriwa na taasisi binafsi yaani Ni lazima Tu niwe katika mamlaka ya hali ya hewa. Sasa ukiniambia niende sekta nyingine utakuwa umenionea Sana yaani nitajuta kupoteza miaka yangu shuleni Ili tu nikaitafute taaluma ambayo baadae inaonekana Ni upuuzi
 
Sawa mkuu me naunga mkono hoja yako. Ila jamani anayejua ajira zitatoka lini aniambie maana me nimesoma kozi ambayo siwezi kuajiriwa na taasisi binafsi yaani Ni lazima Tu niwe katika mamlaka ya hali ya hewa. Sasa ukiniambia niende sekta nyingine utakuwa umenionea Sana yaani nitajuta kupoteza miaka yangu shuleni Ili tu nikaitafute taaluma ambayo baadae inaonekana Ni upuuzi
Umesoma nini nikushauri cha kufanya
 
Sawa mkuu me naunga mkono hoja yako. Ila jamani anayejua ajira zitatoka lini aniambie maana me nimesoma kozi ambayo siwezi kuajiriwa na taasisi binafsi yaani Ni lazima Tu niwe katika mamlaka ya hali ya hewa. Sasa ukiniambia niende sekta nyingine utakuwa umenionea Sana yaani nitajuta kupoteza miaka yangu shuleni Ili tu nikaitafute taaluma ambayo baadae inaonekana Ni upuuzi
Pole sana ndugu yangu. Mimi kuna mtoto wa mama yangu mdogo nilimshauri akasome education ila yeye anasema ndoto yake ni kuwa Lawyer nikamwambia sawa kila la kheri mdogo wangu.
 
Back
Top Bottom